Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, kilichotokea usiku wa kuamkia leo Novemba 27, 2024.
Ninatoa salamu za pole kwa familia, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wananchi wa Kigamboni, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema.
Amina.
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo tarehe 09 Novemba, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
Bw. Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali.
Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema.
Amina.