Ndugu wanachama wa CHADEMA na Wapenzi wa Demokrasia Nchini.
Chama chetu kimefunguliwa rasmi kufanya shughuli za siasa. Hii ni fursa muhimu katika kuendelea na mapambano ya haki, uhuru na uwajibikaji katika Taifa letu.
Lakini ukweli usioepukika ni huu
hatuna ruzuku hata ya SENTI MOJA.
Hii ina maana kwamba uhai, nguvu na uendelevu wa CHADEMA uko mikononi mwetu sisi wenyewe.
Hatuna budi kuchukua jukumu.
Hatuna budi kusimama.
Hatuna budi kuchangia.
Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA.
Usione mchango wako ni mdogo.
Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki.
Tujenge utamaduni wa kuchangia bila kusukumwa. Tujenge tabia ya kusaidia chama kila wakati. Hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli wa kisiasa na kiutendaji.
Mimi nipo, na nimeanza.
Na wewe pia ni wakati wako sasa.
Chukua hatua.
Anza kuchangia.
Simama na CHADEMA.
Kwa pamoja, tutakijenga chama imara na Yaifa lenye HAKI.
Tuchange tu kwa namba maalumu za CHAMA na Akaunti za Benki ili kujenga uadilifu wa Taasisi Imara.
Mikakati zaidi inakuja baada ya vikao kuanza.
Asanteni.
Mwanangu Magesa alikuwa na shida ya tumbo. Awali aliambiwa ana vidonda vya tumbo.
Kuna nyakati tumbo likimshika alikuwa hawezi hata kutembea.
Siku moja alizidiwa. Tukakimbia hosp.
Niliitwa pembeni Daktari akaniuliza: "Magesa ni nani yako?" Nikamjenga!
🧵🧵
That BBC documentary came to remind us yet again that WE SHOULD NOT STOP TALKING ABOUT IT. And that we should keep talking and sharing widely until they can't hide their faces anymore, until they can't run away from justice.
Miili ya mamia ya Watanzania iliwekwa ktk frigde za mortuary wakiwa hai..na wengine walizkwa katika makaburi ya halaiki wakiwa hai.
Imagine waliteseka kiasi gani kabla hawajafa?
Hatutasahau Octoba 29!
Tunataka uwajibikaji.
Miezi mitatu sasa maumivu, huzuni, masikitiko, maombolezo bado vipo na vitaendelea kuwepo maana kupotozewa ndugu, jamaa au rafiki si kitu chepesi. Wanataka muda upite tusahau ila 2910 haitosahaulika. Waliondoka kwaajili yetu nasi tufanya sahihi kwaajili yao. Wapumzike Salama 🙏🏽
VIDEO:
Abate wa Abasia ya Ndanda, Christian Temu, amewataka waumini wa Kikristo na Watanzania wenye mapenzi mema kuacha uoga na badala yake kuwa wajasiri katika kusema na kusimamia ukweli na haki, akisisitiza kuwa ujasiri si jambo la hiari bali ni wajibu wa kiimani.
Akizungumza leo Jumamosi, Januari 10, 2026, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Kumbukumbu ya Mashahidi wa Pugu na kufunga Mwaka wa Jubilei Kuu 2025, Abate Temu amesema kuwa amani na haki ni matunda ya Kimungu ambayo binadamu anapaswa kuyatetea bila hofu yoyote.
"Mkristo atambue kwamba kuwa mtu muoga sio option (hiari), sio jambo la kuchagua. Tunaalikwa na kusukumwa tuwe watu wajasiri tunaopenda kusema ukweli na kuzungumzia masuala ya haki bila kuogopa, kwa sababu haki na amani ni matunda ya Kimungu," amesema Abate Temu mbele ya maelfu ya waumini waliojitokeza katika Kituo cha Hija cha Pugu.
Kiongozi huyo wa kiroho amehimiza waumini kuwa na ujasiri wa kutaja haki ya mtu kwa jina lake kuanzia ngazi ya familia, parokia, majimbo, hadi ngazi ya Taifa. Amewapongeza viongozi wa dini na watu wenye mapenzi mema ambao wameendelea kusimama imara kutetea haki na amani ya kweli licha ya shinikizo (presha) zilizopo ndani ya jamii.