Tundu Lissu amepewa namba ya mfungwa ambayo ni 623.
Ukisoma Luka 6:23 inasema “Furahini siku ile na kuruka-ruka, kwa kuwa, tazama, thawabu yenu ni kubwa mbinguni, maana, baba zao waliwatenda manabii vivyo hivyo.”
Kila kitu kinachotokea kwenye maisha ya Tundu Lissu ni kusudi la MUNGU tusihuzunike sana.
USHINDI UNAKUJA NA HAUPO MBALI.
GOOD MORNING.
REPOST 200
#FreeTunduLissu
“Waheshimiwa Majaji nashukuru kwa fursa ya kuzungumza. Naomba mnisikilize kwa makini kama ambavyo mmenisikiliza kwa makini mwaka mzima. Naomba pia m’rekodi proceedings kama mlivyo’rekodi vizuri mwaka mzima na nusu. Leo Waheshimiwa majaji ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kosa la uhaini. Ndiyo kosa kubwa Kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano. Ndiyo kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa la uhaini. Kwa siku 577 nimeitwa mhaini. Kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) ambapo adhabu yake inaeeza kuwa ni KIFO. Baada ya siku 577 baaada ya wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’inia juu ya kichwa changu. Leo Waheshimiwa Majaji mmeniita MCHOCHEZI. Kosa ambalo wala halijapangiwa adhabu. Unaona hapa, wakili mkuu wa serikali anahangaika kutafuta hii adhabu yake ni nini., anasema nipewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine, nihukumiwe kifungo cha miaka mitano gerezani. Hii maana yake ni nini Waheshimiwa Majaji? Waheshimiwa majaji mmesema wenyewe hakukuwa kosa. Kwa hiyo nimekaa gerezani siku 577 bila kosa lolote. Kuna kitu kimoja hamjakisema nitakisema kwa ajili ya kumbukumbu za Mahakama. Ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa kesi ya kisiasa. Kugeuza Mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa, it’s an obvious political persecution. Kwa sababu ni political persecution inabidi vi’sababu vitangenezwe vya kumfunga huyu mgomvi wetu. Vi’sababu vya kumfunga huyu mpinzani wetu. Hili kosa la UCHOCHEZI ni kisa ambalo ninyi Waheshimiwa Majaji mmelitengeneza. Mimi nilishitakiwa kwa UHAINI na kusambaza taarifa za uongo. Mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, mmenipa. With all due respect mmefanya hivyo kwa sababu za kisiasa na kwa maelekezo ya kisiasa tu. Ni kama mmeambiwa, huyu mtu hana kosa lakini tafuteni kosa lingine dogo, isije ikaonekana serikali imepata aibu. Mimi ninajua mtani’hukumu. Na mnaonekana tayari mnayo hukumu, l feel it in my heart.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, O6 November 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
Kwa walimwengu shujaa ni yule mwenye nguvu na asiyetoa chozi wakati wa uchungu
Asiyekosa au anayeonekana mtukufu kwa walimwengu ushujaa kuweza na sio kuthubutu
29.10.2025 💔❤️🩹
@zoetjesheeftX Apa anazungumzia haki gani Hali ya Kuwa waligawana kitambo uko Kila mtu akaishi na hamsini zake! Kuna baadhi ya wanawake kichwani wanafunza tupu