Because foolish people take risks without fully understanding the consequences.
Highly intelligent people often overanalyze. They map every possible obstacle, calculate every risk, and eventually convince themselves the road is too dangerous to take.
Foolish people, and even intelligent people who temporarily stop overthinking na “kujitoa akili,” tend to move faster, take more shots, and sometimes achieve more because they are willing to act while others are still calculating.
Sometimes success rewards courage before intelligence.🤣
MUNGU WA MASIMULIZI?
Huyu mtoto hapa ni pure, hana influence yoyote ya story za Mungu.
Akikuzwa na familia za Wahindi, atakuja kuamini kuna Miungu 1,000,000.
Akikuzwa na Wakristo, atakuja kuamini kuna Mungu mmoja mwenye nafsi tatu ambaye nafsi yake moja ilikuwa incarnated kama mwanadamu kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu kisha ikauawa na mwanadamu. Ataamini pia kuwa hatuwezi kwenda mbinguni pasipo kumkiri mwanaye ambaye ni nafsi yake ambaye ni yeye.
Akikuzwa na Waislam, atakuja kuamini kuna Mungu mmoja asiyekuwa na story za nafsi wala hana mtoto. Ataamini Mtume ndio Nabii wa mwisho na kwamba anapaswa kufuata alichokisema, ikiwemo kwenda Arabuni kwa ajili ya Hija.
Akikuzwa na Wakatoliki atakuwa Mkatoliki; Walutheri atakuwa Mlutheri; Washia atakuwa Mshia; Wasuni atakuwa Msuni; waabudu sanamu ataabudu sanamu.
Akikuzwa kwenye familia za Wachina, atakuja kuwa Atheist asiyekuwa na story zozote za Yesu wala Mtume wala aliyewatuma. Akijitahidi sana ataabudu deities.
Akidondoshwa kule Ugiriki ya zamani, atakuja kuamini wakina Zeus, Hera, Poseidon, Athena, Apollo etc. ndio Miungu.
Akikuzwa kule Misri ya zamani, atakuja kuamini Osiris, Isis, Horus, Seth, Ptah, Re · Hathor, Anubis, etc. ndio Mungu.
Akikulia Babeloni ataamini Marduk ndio aliumba ulimwengu baada ya kuua wazazi wake Apsu na Tiamat na kutumia miili yao kutengeneza Mbingu na Dunia. Story za kuumba kwa neno siku saba hazitakuwa zake.
Akikulia kwa wale Bushman tuliowaangalia kwenye ile movie ya the Gods Must be Crazy, atatembea mpaka mwisho wa Dunia kwenda kuzika chupa ya soda iliyodondoshwa kwenye eneo lake kwa kuamini ni laana kutoka kwa Mungu.
Alikulia porini anakointeract na wanyama tu, hatokaa awe na mawazo ya Mungu wala biashara ya maisha baada ya kifo.
Chochote atakachokuzwa nacho huyu mtoto kupitia masimulizi ya jamii yake ndio kitakuwa imani yake na wote wanaoamini tofauti atawaona kama ama wamechanganyikiwa au wamepotoka.
Mungu wa masimulizi.
@Dennysswai@zittokabwe@UhtredBebenberg@DrTaxs Alichagua njia ambayo wenzie walipita hawakufanikiwa na aliambiwa akashupaza Shingo, so kinachotafutwa hapa tumuone muungwana kwakukili alikosea lakini history inamkataa, ni swala la muda tuu atachagua njia tunazozikataa next time
“Aisee, nimetoka kuongea na wenye nyumba hapa nimepata ufafanuzi kidogo kuhusu hili tukio. Wenyewe wanasema hivi;
“1. Sio kweli kwamba nyumba yao inaungua, hayo ni majungu tu ya majirani zao wanaowaonea wivu kwa sababu wao ndio wenye nyumba bora mtaani
“2. Kile kinachoitwa "moshi", kiuhalisia ni mvuke utokao kwenye sauna yao ya ndani - kwa mara nyingine tena wanapenda kukumbusha kwamba nyumba yao ni bora zaidi mtaani
“3. Aidha, walikua wanachoma nyama yenye mafuta ndani - kwa hiyo mafuta yakidondoka kwenye moto ndio inaonekana kama moto ni mkubwa, na moshi wa hapa na pale unaweza kuonekana. Wanawaambia majirani kwa ukarimu kabisa wakaribie kula, waache majungu kwa sababu wao hawana nyama.
“4. Nasikia watoto wananong'ona nong'ona kwamba majirani wakija waje na maji, sasa sijajua kama ni ya kunywa au ya kunawa”