Not a single word about Lissu since his detention in April. Not a single visit to court or Ukonga prison. In fact, you celebrated backlashes vs CDM, hoping you’ll become leading opposition nonsense. And now you, @zittokabwe, pretend to care? You’ve become a disgraceful conman.
Siasa ya ukombozi ni harakati takatifu ya kupigania haki, utu na uhuru wa watu. Haipaswi kabisa kubadilishwa kuwa biashara ya udalali au njia ya kujinufaisha binafsi. Ndani yake kuna maumivu, vifo, na mateso ya kweli ya wapigania haki. Ni jambo la kusikitisha kuona watu wanaojitokeza leo wakitafuta uhalali wa kisiasa tena, ilhali jana walishirikiana na watesi na wakatili. Ushirikiano huo hauwezi kufutwa kwa maneno matamu , kwani ni doa katika historia ya ukombozi.
Mtu yeyote ambaye hakusimama upande wa haki wakati ulipohitajika, bali akajitahidi kuzima sauti za waonewa, ni mtesaji na muuaji kama wale tunaowalaumu leo. Sasa wanarudi kwa mbinu mpya kama “drones” zinazojaribu kutua kwa ujanja lakini ukweli unabaki pale pale, hawa ni wanafiki wanaojificha nyuma ya kivuli cha siasa.
Ukombozi wa kweli hauwezi kuletwa na walafi wa mamlaka, bali na watu waaminifu kwa misingi ya haki, uadilifu, utu wa mwanadamu. Tunapaswa kukemea tabia hizi, kwani hii haipaswi kuwa tabia ya Nchi yetu na watu wake.