Aliepitishwa kugombea Ubunge Tanga mjini ni mtu ambae alipata kura 80 tu za Wajumbe katika ya kura 10,176/= zilizopigwa.
Yaani 1%!!! Na bado tutaendelea kuaminishwa kuwa Viongozi wanapatikana kwa kupigiwa kura?? 😳
"Nzi ana bidii ya kuhamisha vimelea vya ugonjwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Nyuki ana bidii ya kukusanya poleni kutengeneza asali. Uchaguzi ni wako kuwa Nyuki au kuwa Nzi." ~Togolani Mavura.
Mikataba ya MANGUNGO katika jina la UWEKEZAJI
1.Waarabu wa familia ya kifalme Dubai, (DP WORLD) wamepewa kuendesha bandari ya Dar es Salaam kwa mikataba ya kiduanzi unaotajwa miaka thelathini
2.Waarabu wa familia ya kifalme ya Dubai (Blue Carbon LLC) wamepewa kusimamia na kuhifadhi misitu ya Tanzania. Hii ni hekta milioni 8.1 (8% ya ardhi yote)
3.Watu kutoka Russia, (ROSATOM) wamepewa ardhi yenye tani milioni 139 wachimbe madini nadra ya kimkakati ya uranium huko Namtumbo, Ruvuma.
4.Watu wa Australia (URANEX) wamepewa ardhi nzuri wachimbe madini nadra ya kimkakati na graphite Mkoa wa Lindi. Kampuni zao tatu zitauza madini nje
5.Watu wa Canada (BARRICK GOLD) wanaondoka na dhahabu. Hawajajenga hata smelters moja. Wanaacha mashimo na watu wetu kupigwa risasi nyingi.
6.Waarabu familia ya kifalme Dubai (OBC) wameongezewa ardhi 1,500km² kutoka 4,000km² zilizokuwa kwa Maasai wao wamebaki na 2,500km²
7.Watu kutoka Netherlands (SHELL) na Norway (EQUINOR) wamepewa kuchimba gesi asilia katika bahari kuu kusini, eneo la Likong’o, Lindi, Tanzania
8.Waarabu wa Dubai, Emirates National Group (ENG) wamepewa kuendesha huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Jiji la Dar es Salaam.
9.Watu wa France, Maurel & Prom, wanazalisha gesi asilia, 641 billion cubic feet, Mnazi Bay, Mtwara, ambayo ni 48% ya pato la gesi asilia Tanzania kwa sasa.
10.Kandarasi ujenzi Bwawa la Nyerere (JNHPP) alipewa Egypt. Kandarasi ya ujenzi wa SGR alipewa China na Turkey. Waswahili mtapewa Kanda Bongoman.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
@Rap_Mastory @KingPablotz Kiongozi.... Pale Urusi kuongea mambo ya mapenzi ya jinsia moja ni katazo je kwa namna hii unaweza sema hakuna kuhamasisha UPINDE.... Basi mimi nitakuwa niko dunia ya jangwa
@Sadamkidunda21 @KingPablotz Kipande kile Kile kina amua maisha ya watu wengi kuamini kikandwa na kukanada mwanaume mwenzio ni jambo la kawaida.... Je unataka kusema hii movie haina uhalisia wa kuhamasisha UPINDE 🤕
"Kukikucha wanaamka wema na waovu, waadilifu na wahalifu, werevu na wapumbavu, matajiri na maskini. Ili maisha yaende, tunapaswa kuamka wote kwa pamoja ili maisha yaweze kuwa na maana na msawazo. Tungekuwa tunaamshwa kwa zamu ingekuwaje? Tuvumiliane tu maana tunahitajiana."
ILIMCHUKUA Yesu miaka 30 kujulikana anafanya nini. Majirani huenda walianza kuamini kijana hana ‘maisha’ na huenda angeishia kurithi randa na misumeno. Ilipotimia 30 kila kitu kilibadilika. Historia tunayoifahamu aliijenga ndani ya miaka 3.
Kwa miaka takribani 20 hatuambiwi Yesu alikuwa wapi na anafanya nini. Hata hivyo tunachoweza kujifunza ni kwamba mambo makubwa hayahitaji papara. Kutokujua ufanye nini baada ya chuo ni sehemu ya safari. Kustukia miaka inaenda na huna cha kuonesha ni sehemu ya safari. Usipoacha kujifunza, kukosea, kuanguka na kuamka tena, kuumia na kutibu majeraha, wakati wako utafika na yote uliyojifunza yatakupa matokeo yakayokushangaza.
Saa nyingine unahitaji miaka 10 ya kujifunza jambo gumu unalokuja kulisema kirahisi, kwa dakika chache, likamgusa mtu na ukalipwa vizuri. Saa nyingine unahitaji hasara ya miaka 15 kwenye biashara ili ujifunze aina ya watu wa kushirikiana nao, namna ya kutengeneza mfumo utakaokupa faida itakayobadilisha maisha yako. Ukiongea na wengi waliofanikiwa kihalali unagundua nyuma ya kicheko cha mafanikio yanayoonekana ni ya muda mfupi kuna machozi mengi na jasho jingi lisiloonekana.