Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kinatoa shukrani zake za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia magari mawili (Toyota Land Cruiser Hardtop) yatakayorahisisha utekelezaji wa majukumu ya Chama.
Ikulu, Dar es Salaam, 16 Mei, 2026.
Nimekutana na kufanya mazungumzo na Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote pamoja na ujumbe wake.
Alhaji Dangote ni mmoja wa wawekezaji wakubwa Tanzania ambapo kiwanda chake cha saruji (Dangote Cement) mkoani Mtwara kinakuza uchumi wetu kupitia biashara ya saruji, ajira kwa Watanzania na kukuza sekta fungamanishi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma tarehe 26 Juni, 2025. Pamoja na mambo mengine kesho Mhe. Rais Dkt. Samia atahutubia nakuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Safarini kwa treni kutoka Dar es Salaam kuelekea Jijini Dodoma, ambapo pamoja na majukumu mengine, kesho Ijumaa Juni 27 nitahutubia na kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulihutubia na kulifunga Bunge la 12 siku ya Ijumaa tarehe 27 Juni, 2025.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya ndugu zetu 28 na majeruhi 8, vilivyotokana na ajali ya barabarani iliyotokea jana usiku katika Mlima Iwambi, kwenye Barabara Kuu ya Tanzania - Zambia, Mkoa wa Mbeya.
Ninawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone haraka. Aidha, ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Juma Homera, familia zote za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyenzi Mungu awajalie subra na uvumilivu.
Ninawasisitiza madereva kuendelea kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani. Nimeliagiza Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu sheria za usalama barabarani, na pia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kuendelea kuboresha hali ya barabara zetu, hasa maeneo yenye changamoto kubwa zaidi, kwa usalama wa watumiaji wote wa barabara.