#TANZIA Aliyewahi kuwa Golikipa wa timu ya Yanga SC, Clause Kindoki, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kufuatia ajali ya gari, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa.
Kindoki aliichezea Yanga SC kati ya mwaka 2018 na 2020 chini ya kocha Mwinyi Zahera, ambapo alijizolea sifa kwa uwezo wake langoni na kuwa mmoja wa makipa wa kigeni waliokumbukwa zaidi na mashabiki wa klabu hiyo.
Marehemu pia anatajwa kuwa chanzo cha umaarufu wa jina la utani "Jimmy Kindoki", lililoibuka kutokana na kiwango chake bora cha uchezaji akiwa golini. Mashabiki na wadau wa soka wameendelea kutoa salamu za pole kufuatia kifo chake.
#EastAfricaTV