SIMBA SC 🔴 mnajua nini Wachezaji? Ni kwamba historia huandikwa na Mashujaa, waliopigana vyema vita na kusimamia vyema misingi na sababu ya kuingia vitani, Watu hufariki, Maua hunyauka, Mapenzi hupotea ila historia haifutiki kamwe, nimesafiri na hizi timu wengi wakijua ni kutoka Tanzania husema “Mnatokea Taifa la Mwalimu Nyerere?”
Mnajua nini Wanaume? Mwalimu amelala usingizi wa Milele tangu miaka 26 iliyopita kwenye ardhi ya Wazanaki pale Butiama, ila heshima yake inadumu milele, tangu aliposimama kwenye podium pale New York basi kilichobaki ni historia, Wanaume mnajua nini? Historia ni kwa ajili ya Washindi tunapaswa kuacha historia kwenye ardhi ya Marafiki wa Mwalimu.
Wanangu mnajua nini? Mnaweza kuwa Wadogo kiumri wengine, mnaweza kutokuwa na uzoefu na Fainali ila Simba Sports ni kubwa sana, nembo yake inapaswa kupiganiwa vyema huku Kaskazini Mashariki mwa Bahari ya Mediterranean, tunaingia uwanjani usiku wa leo kwa heshima ya bendera, kwa historia ya Taifa tukufu la Tanzania, kwa heshima ya Wapambanaji wote waliozikwa kisa Mama Tanzania.
Niaminini Mimi, tumebeba hatma ya Mama Muuza Ndizi soko la Kiwira, mkoani Mbeya! Tumebeba hisia za Mmiliki wa Kibanda Umiza huko Tandahimba, Mtwara! Tunamnyima usingizi Muha wa Kigoma na hana raha Mdigo Muungwana kutoka Pwani ya Kaskazini Mashariki mwa Bahari ya Hindi, kwa heshima ya Chief Mirambo wa Tabora basi tuingie uwanjani kulipigania Taifa hili.
Tunapotembea kuelekea Fainali tutazame Makaburi ya Ndugu zetu Azam FC, tutazame makaburi ya KMKM na JKU, kaburi la Young Africans na Coastal Union, tupite pia tukitazama Makaburi ya timu zote kutoka Global South, Waungwana kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara ambao hawakuweza kufika fainali, hii sio kwa ajili ya wetu ni kwa ajili ya wengi kwa heshima ya Kusini mwa Afrika.
Mnajua kwanini tunacheza soka? Ni kwasababu tunaipigania nembo kifuani ili Mashabiki watukumbuke kwa majina Mgongoni, tunaenda Uwanjani Wanaume tena mbali na nyumbani, tukacheze mechi ya mpira wa miguu, yes Play the Game, not the ocassion, inawezekana Wanaume, hatukosei tunajifunza, hatupotezi tunajifunza, kwa heshima ya bendera jioni ya leo.
MUNGU IBARIKI SIMBA, MUNGU IBARIKI TANZANIA 🇹🇿
@kenxbil5424 @A_team_21 @HumansNoContext Hvi hii twitter tumejaa waTanzania tu nn 😅😅 (kila kona), nimeona hii post nikawaza mbona Tz hawa wapo tele, kufungua comment nakuta comment ya mTanzania.
@BosnjaninTvrtko@FPLMattW Yes he surely will, I have owned him for the past 10 GWs too to totally understand what you saying. I still transfered him out though. The greater the risk the bigger the reward.
@Aaqni7130@ThePeakSanti Bro id Raya played, through his distribution we couldn't be in a position where we faced either of the two savea that Ramsdale saved. And probably the game couldve ended 3~0. Its all about starting from the back and distributions and the calmness he brings to the defence.