Moja ya mambo nimejifunza in a hard way, ni nadra watu kuhahirisha mambo yao kukusaidia.
You will be there starving, wakati Kaka yako anamalizia ujenzi wa apartment na anasema hana hela, na hakuna kitu utamfanya, ni hela yake.
Just survive to treat people the same 😆😆
Nimetimiza AHADI YANGU KUCHANGIA CHADEMA 1M baada ya kufikisha MILIONI 300 (NIMEFIKISHA JUMLA 7M NDANI YA SIKU 46).
Niliacha kuenda KANISANI na kuwa muumini WA HAKI.
SADAKA yangu siku zote ni kuchangia WAPIGANIA HAKI.
Nilianza kampeni hii ya kuichangia chadema kwa kuchangia 1M siku 46 nyuma.
Nikaja kuanzisha challenge kwa wapenda HAKI WENZANGU kwamba tukifikia MILIONI 100 basi nitachangia tena 2M Nilifanya hivyo.
Nikaongeza challenge kwa WAPENDA HAKI kama tutafikia MILIONI 200 basi nitachangia tena MILIONI 3 nilifanya hivyo.
Kisha nikaongeza Challenge kama tutafikia MILIONI 300 basi nitachangia tena MILIONI 1 leo nimefanya hivyo.
Mpaka sasa nimechangia jumla ya MILIONI 7 ndani ya siku 46.
Lengo la hii kampeni ni kukusanya MILIONI 334 bado milioni 33 kwasasa tunaweza kufikia.
Kuchangia CHADEMA kwangu ni SADAKA baada ya ibada KAMILI YA KUPIGANIA HAKI.
Kama ulichangia basi fanya KUCHANGIA TENA NA TENA kama nilivyofanya mimi.
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
REPOST 500
Huyu anaitwa Jackson yupo Oysterbay polis kitengo( SIBER)
ndio aliusika na utekaji wa ndugu yetu peter mushi na kumweka kwenye gari aina ya crown na kuondoka naye.
mpaka sasa ni siku ya 11 @tanpol wamekaa kmy na bila kutoa ushirikiano kwa familia💔
Naomba Retweet🙏
Mpaka sasa tumefikisha 3,246,642.
Mungu awabariki sana.
Bado milioni 1,753, 358 ili tutimize lengo la kupata milioni tano. Tuendelee kutuma michango yetu kwa ajili ya Bibi yake Deusdedith Soka ili aweze kupata mahitaji muhimu ikuwemo Bima ya afya.
Mpesa : 0740498941
Jina: Theresia Soka.
Mzee @freemanmbowetz
Wanyama wa porini huua/kupigana kwa sababu zinazohusiana na mahitaji ya kuishi: chakula, kujilinda, kulinda watoto au eneo. Simba anawinda kwa ajili ya chakula siyo mateso, chuki, kisasi
Binadamu ni viumbe katili zaidi ya wanyama. Binadamu anaweza kumdhuru mwingine kwa sababu ya chuki, ubaguzi, tamaa, kulipiza kisasi, madaraka au kwa sababu anaona mwingine hafai kuishi
Kutoka Mikocheni kwenda ilipo Mahakama Kuu ya Tanzania ni umbali usiozidi 5KM. Kutoka Mikocheni kwenda Rufiji ulipo mradi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) ni umbali wa 260KM
Unaweza kusafiri kwenda mkoa mwingine kwa zaidi ya saa tano kuhudhuria shughuli za Serikali katili ya CCM lakini huwezi kutumia dakika 10 kutoka kwako kwenda Mahakama Kuu katika kesi ya TAL?
Huwezi kwenda safari ya 5KM kumuona Mwenyekiti wako wa chama, aliyerithi kiti chako katika uchaguzi HURU na HAKI lakini unaweza kwenda 260KM kuungana na watesi wa Mwenyekiti wako?
Nini muhimu zaidi kwako? Ni wewe ulitueleza miradi ya maendeleo haiwezi kuwa mbadala wa haki za binadamu. Leo kuna watu wanatekwa na kupotezwa, wanashtakiwa kwa ugaidi na uhaini. Hujui?
Lakini umechagua nini? Nimekusikiliza ukisema “mradi wa JNHPP usichukuliwe kisiasa kwa kuwa ni mradi unaokwenda kusaidia uchumi”. Umesahau ulitueleza nini kuhusu miradi ya MAGUFULI?
Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kwa sasa ni ‘mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya CHADEMA - ni kutokana na hiki kinachoitwa ‘ustaafu’ wa uenyekiti wa CHADEMA Taifa
Kwa maana kwamba, Freeman Mbowe yupo katika kundi sogozi la WhatsApp na mengine (kama yapo) ambayo wajumbe wa kamati kuu wanajadili kwa hisia zao tofauti masuala mbalimbali ya chama
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu CHADEMA huwezi kwenda Mahakamani katika kesi ya kiongozi wa chama, lakini unaweza kwenda katika shughuli zinazoongozwa na mwenyekiti wa CCM
Freeman Mbowe umesahau, wakati ukishtakiwa kwa makosa ya uongo ya UGAIDI, Tundu Lissu alikuwa Belgium akijiuguza majera ya risasi. Aliomba kukutana na Rais alipokuwa Brussels
Pamoja na mambo mengine waliyokubaliana, alisema Mwenyekiti Freeman Mbowe aachiwe ndiyo tufungue ukurasa mpya. Tundu Lissu alitujulisha mwenyewe hayo alipozungumza na umma.
Tundu Lissu akiwa na siku 500 gerezani. Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe hujawahi kukanyaga Mahakamani kuanzia Kisutu hadi Mahakama Kuu hata kwa bahati mbaya.
Saa 24 baada ya Mahakama Kuu kusema Tundu Lissu ana kesi ya kujibu katika mashtaka ya UHAINI ya uongo na uzandiki, Freeman Mbowe unaibuka katika shughuli za Serikali ukiwa na MAWAZIRI.
Mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CHADEMA umekataa kabisa kuhudhuria shughuli zozote za CHADEMA lakini unaweza kuhudhuria shughuli unazoalikwa na WATAWALA KATILI wa CCM.
Unahudhuria shughuli za Serikali umeongozana na mawaziri wa Serikali katili ya CCM wakati ambao wanachama na wafuasi wa CHADEMA kwa mamia wamekamatwa na kushtakiwa kwa UGAIDI?
Mzee Freeman Mbowe umesahau haraka. Kuna watu walifungwa gerezani, wengine sasa ni walemavu, wengine sasa ni marehemu kwa sababu ya kupigania jina lako ukiwa kiongozi wa chama chetu.
Umesahau, wakati unakamatwa na Serikali katili ya CCM, 2021, wanachama wa CHADEMA walikwenda kuonyesha ‘solidarity’ na wewe pale KISUTU. Walikamatwa, wakashtakiwa, wakafungwa
Najutia zile siku nilisimama nawe, kukutetea na kunadi jina lako kwa nia njema kabisa nikifikiri unapambania uhuru, haki na mabadiliko ya kweli. Haikuwa hivyo. Ulitudanganya tukishindwa.
Nasema kwa kuwa kwa hiari yangu, niliamua kusimama nawe, kukunadi katika mazingira ambayo ilionekana ni kama kuuza kitimoto Mecca. Lakini sikutarajia tukishindwa, tuisaliti CHADEMA
Wengine sasa tumeelewa kwa kuchelewa sana. Hii chuki haiwezi kuwa ya kushindwa uchaguzi. Lazima kuna mafekeche mengine. Kuna kingine kimeujaza chuki moyo wako. Je, kuna mrija, umekatwa?
Najutia kumpa mtoto wangu jina lako, Freeman.
‼️VIDEO YA CCTV CAMERA IKIONYESHA UTEKAJI KARIAKOO‼️
Huyu kwenye video Anaitwa Peter Richard Mushi ni fundi simu Kariakoo
alipigiwa simu tarehe13/8/2026 na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mteja anahitaji kutengenezewa simu
Alimwelekeza alipo lakini mteja akataka ndugu peter amfuate maeneo ya china plaza alipofika china plaza
Alikutana na huyo mteja aliyekuwa anampigia simu kumbe hawakuwa wateja bali ni watekaji 💔 walikuja na gari toyota crown rangi nyeupe aina plate namba ndugu wamezunguka vituo vyote vya police hospitali zote mochwari zote bila kupata majibu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 254
Anasimama Wakili wa Serikali Ignas Mwinuka anasema Presidential Affairs Act kifungu cha 9 kinasema wito wa summons maana yake unamlazimisha shahidi kufika.
Kifungu hicho cha 9 kinasema anakisoma. Kwahiyo kwa mujibu wa kifungu hiki Mahakama haina mamlaka kutoa wito wa ku compell Rais kufika Mahakamani.
Naomba kuwasilisha.
Anasimama Wakili mwingine wa Serikali Job Mrema nae, anasema naomba kuunga mkono hoja.
Jaji Ndunguru : achana na mambo ya kuunga mkono hoja, Nenda kwenye hoja
Mrema anasema Section 24 ya TISS CAP 406 kinasema kuhusu protection of source of information.
Yaani usiri wa taarifa kwa kuzingatia mshitakiwa ametaja baadhi ya mashahidi mfano DGIS yaani Mkuu wa Usalama wa Taifa aje hapa Mahakamani. Anataka kupata taarifa kwa mashahidi hawa ili apate kujitetea.
Sasa kwa cheo cha shahidi huyu anafungwa na masharti ya sheria hii hata akija hapa hataweza kusema kila kitu. Na sio sahihi kabisa. Kuna limitation kwa mujibu wa sheria.
Kifungu hicho kimeweka penal sanctions yaani kutoa ushahidi huo ni kosa kubwa la kisheria.
😂😂 Lissu alisema mmeyataka mtayapata. Ngoja tuendelee.
Job Mrema anaendelea kusema naomba kufanya marejeo kwenye shauri la criminal appeal Jacob Tiifunga vs Republic Criminal Appeal No. 185/1980. HC Tanzania at mwanza. TLR.
Mahakama ilisema a trial magistrate has descretion to call witness yaani Mahakama ina uwezo wa kukataa shahidi kuitwa. Lakini kwa mujibu wa msingi uliotengenezwa kwenye kesi hii ni kuweka sababu. Sasa sisi tunasema sababu tulizotoa kuanzia shahidi namba moja SAMIA hadi namba 7 mashahidi wasiitwe kwenye shauri hili kwa sababu tulizozieleza na ni hoja yetu kuwa mnayo mamlaka ya kukataaa. Ni hayo tu.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mshtakiwa kama anacho cha kusema
Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji kabla sijaanza naomba kidogo kufanya consultation na Mawakili wangu kabla sijaanza, 5 minutes its enough...
Mawakili wa Lissu wakiongozwa na Dr. Nshala, Jebra, Matata, Paul Kisabo, Deogratias Mahinyila, Madeleka namuona Wakili Kisabo amesimama akimuonyesha Mhe. Lissu sheria kwenye laptop, Lissu anasoma na wanaendelea kujadiliana.
Wamemaliza kujadiliana
Mhe. Lissu anasema
Kuhusu hoja ya mimi kuwataja mashahidi wangu ninaotegemea kuwatumia kwenye kesi hii. Katuga amesema hoja hii na ukweli ni kwamba toka Kisutu hoja hii ilikuwa na shida.
Mgogoro specific ni kwamba Hakimu Mkuu Mkazi Franco Kiswaga baada ya mtuhumiwa kumwambia kuwa ana mashahidi na kuanza kuwataja akakataa kuwarekodi hao mashahdi.
Na hoja yake ilikuwa ni hao utaenda kuwataja Mahakama kuu. Mimi siandiki utaenda kuwataja Mahakama Kuu.
Baada ya shauri kuletwa hapa Mahakama Kuu Waheshimiwa Majaji nilileta hoja kwamba utaratibu mzima wa committal proceddings ulivurugwa kwa makusudi na nikawaambia majina ya mashahidi wangu wa utetezi yalikataliwa.
Nililileta mbele yenu na mkasema wenyewe kuwa utakapofika wakati wa kujitetea utaapata fursa ya kuandaa utetezi wako. Na mkasema niawatajie majina mnaotaka niwaite.
Nikawatajia na Mkaandika kwenye rekodi.
Katuga akasema ukurasa wa 186 wa proceedings orodha ipo na mliwaandika wenyewe Majaji.
Jambo hili sio la leo. Lipo kwenye rekodi za Mahakama hii, anachotaka Katuga mfanye ni mjikane wenyewe.
Anataka mjioneshe kuwa hamna akili sasa hiyo ni juu yenu sio kwasababu majina ya mashahidi hayajawahi kutajwa.
Yalitajwa Kisutu, yakatajwa kwenu na leo nimerudia tena.
Amueni mtanipa haki hiyo ya kupata mashahidi au mjikane.??
Mimi napendekeza msijikane, msikubali huo mwaliko wa kujikana. Vinginevyo kosa kubwa kuliko zote Mahakama hii itathibitisha kuwa haina uwezo wa kutenda haki tena kwenye Kesi ambayo adhabu yake ni kifo, mtaonesha kuwa hamna uwezo wa kutenda Haki na mtageuzwa Kangaroo Court. A court of star Chamber Court.
Hoja ya kifungu cha 281 na 314(2) mlishaandika majina ya mashahidi last year. Has already been taken by your own order.
Part 255 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
‼️VIDEO YA CCTV CAMERA IKIONYESHA UTEKAJI KARIAKOO‼️
Huyu kwenye video Anaitwa Peter Richard Mushi ni fundi simu Kariakoo
alipigiwa simu tarehe13/8/2026 na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mteja anahitaji kutengenezewa simu
Alimwelekeza alipo lakini mteja akataka ndugu peter amfuate maeneo ya china plaza alipofika china plaza
Alikutana na huyo mteja aliyekuwa anampigia simu kumbe hawakuwa wateja bali ni watekaji 💔 walikuja na gari toyota crown rangi nyeupe aina plate namba ndugu wamezunguka vituo vyote vya police hospitali zote mochwari zote bila kupata majibu
Dunia nzima inajua Tundu Lissu hana kesi ya kujibu, na kwamba hapakuwahi kuwa na kesi ya uhaini.
Lissu anatakiwa kuwa huru kwakuwa si mhalifu. Sio kwa sababu ya huruma za waliompa kesi ya uongo.
Free Tundu Lissu Now!