Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amefichua mruko mkubwa wa gharama katika mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu jijini Arusha, uliopangwa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2027. Katika ripoti yake ya mwaka wa fedha 2024/2025 iliyowasilishwa leo Machi 30, 2026, CAG amebaini kuwa wakati wataalamu walikadiria mradi huo kugharimu shilingi bilioni 187, mkataba wa ujenzi ulisainiwa kwa shilingi bilioni 338.54.
Tofauti hiyo ya shilingi bilioni 151.54 ni sawa na ongezeko la asilimia 81 ya makadirio ya awali, jambo ambalo limezua maswali mazito ya kiukaguzi kuhusu usimamizi wa fedha za umma na uhalali wa mchakato wa zabuni. CAG amesisitiza kuwa mabadiliko hayo makubwa ya gharama kati ya hatua ya usanifu na hatua ya utekelezaji yanaashiria udhaifu katika tathmini ya awali na yanaweza kuisababishia serikali hasara ya kutopata thamani halisi ya fedha.
Ripoti hiyo inahoji vigezo vilivyotumika kuhalalisha nyongeza ya mabilioni hayo ya fedha, ikitaka kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji kwa waliohusika na mchakato wa ununuzi.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu amependekeza mamlaka husika kufanya mapitio ya kina ili kubaini sababu za kitaalamu zilizopelekea mkataba huo kusainiwa kwa bei ya juu kiasi hicho, huku akionya kuwa hali hiyo inahatarisha ufanisi wa miradi mingine ya kimkakati nchini.
Aidha amesema wizara husika kutoa ufafanuzi wa kina juu ya mruko huo wa gharama. Inasisitizwa kuwa, ili kulinda kodi za wananchi, ni lazima taratibu za ununuzi wa umma zizingatie uhalisia wa soko na kuzuia mianya ya ubadhilifu inayoweza kujificha nyuma ya dharura ya ujenzi wa miundombinu ya michezo.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dkt. Charles Kichere, leo Machi 30, 2026 amewasilisha ripoti kuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo amesema deni la Serikali limeongezeka hadi kufikia Tsh. trilioni 110.05 kutoka Tsh.trilioni 97.35 ambapo deni hilo limechangiwa zaidi kwa kuongezeka kwa mikopo ya nje na kushuka kwa thamani ya shillingi dhidi ya dola za Marekani.
Dkt. Kichere amesema ““Ongezeko hili limechangiwa zaidi kwa kuongezeka kwa mikopo ya nje pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani ambapo kushuka kwa thamani kumechangia ongezeko la deni la Tsh. trilioni 2”
“Tathmini ya uhimilivu wa deni imebaini kuwa deni la Serikali bado lipo ndani ya viwango salama vinavyokubalika Kimataifa huku thamani ya sasa ya deni lote la umma kwa pato la Taifa ikiwa ni asilimi 40.7 chini ya ukomo wa asilimia 55 na deni la nje kwa pato la Taifa likiwa ni asilimia 24.9 chini ya ukomo wa asilimia 40”
#MillardAyoUPDATES
@Rydx_017@athanas_pius@Balyx_@MissChelsea1221@DullahTheking2 Mabillion ya Kodi za watanzania yanapotea ATCL, ni kwanini Serikali isiamue kutumia Ubia katika hili kama ilivyofanya kwenye Bandari, lengo ni kuongeza ufanisi wa huduma na kuokoa fedha za Umma
VIDEO:
Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Profesa Haji Semboja ameeleza kuwa miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na umma si jambo geni nchini Tanzania akirejea historia ya ushirikiano wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) ndani ya sekta za nishati na uziduaji (madini, mafuta na gesi) nchini Tanzania, akielezea mageuzi yake tangu mipango isiyo rasmi ya katikati ya miaka ya 1980 hadi kufikia mifumo ya kisasa ya kisheria.
Prof. Semboja ameyasema hayo akizungumza wakati wa Kongamano la Kitaifa kuhusu Ubia (PPP) katika Sekta ya Nishati ambalo limeangazia mada: Nafasi ya PPP katika Upatikanaji wa Nishati ya Uhakika chini ya chini ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa (FYDP IV). Kongamano hilo lililoratibiwa na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) limefanyika leo Machi 30, 2026 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Prof. Semboja ameangazia jinsi taifa lilivyotoka katika ushirikiano uliotawanyika na kuelekea katika mifumo rasmi ya kitaasisi, akitumia ushiriki wa wazalishaji binafsi wa umeme (IPPs) wakati wa majanga ya nishati kama mfano mkuu wa jinsi uwekezaji binafsi unavyoweza kusaidia maendeleo ya kitaifa.
Mbali na umeme, Prof. Semboja ameeleza mifano mbalimbali ya ushirikiano kama vile Mikataba ya Ugawanaji wa Uzalishaji (PSAs) katika sekta ya mafuta na gesi, na jukumu la mashirika ya umma kama TPDC na NDC katika kusimamia rasilimali hizi.
Aidha, amesisitiza mabadiliko ya kimkakati kuelekea katika upanuzi wa vyanzo vya nishati, kwa kuachana na utegemezi wa umeme wa maji pekee na kuelekea kwenye gesi asilia na nishati jadidifu kupitia ushiriki ulioimarishwa wa sekta binafsi.
TANZIA: Aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Kilwa Kusini kupitia Chama cha CUF, Seleman Said Bungara maarufu kwa jina la Bwege, amefariki Dunia, Machi 30, 2026 akiwa hospitali ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Enzi za uhai wake Bwege amewahi kutumikia vyama vya Siasa vya CUF, ACT Wazalendo na hivi karibuni ilidaiwa alikuwa mbioni kujiunga na CHADEMA, ingawa mchakato rasmi wa kukabidhiwa kadi ya chama hicho ulikuwa haujakamilika.
Zaidi https://t.co/BZu1vVM7Wc
#JamiiForums #RIPBwege
TAKUKURU imebaini mtandao wa uhalifu wa kifedha uliohusisha kughushi kadi za benki na kusababisha upotevu wa zaidi ya Sh.bilioni 147.5 kutoka kwenye akaunti za wateja bila ridhaa yao.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, amesema uchunguzi umeonesha kuwa fedha hizo zilichotwa kupitia miamala ya malipo ya huduma na bidhaa kwa kutumia jumla ya kadi 1,551 za wateja kutoka mataifa 11.
Imeandikwa| Mwandishi Wetu
Tembelea https://t.co/kwAYTrP3RO kusoma gazeti lako au wasiliana nasi 📞+255 745 -700 710 au 0677- 020 701 kwa maelezo zaidi.
#NipasheDigital #NipasheMwangaWaJamii #miaka30yakupashahabari
Government debt has reached Sh110 trillion as of June 30, 2025, rising by Sh12.7 trillion, or 13 percent, within a single year, a report by the Controller and Auditor General (CAG) has revealed.
https://t.co/ahYqXlTNwa
Jeshi la Polisi mkoani Geita limesema
hakuna mtu aliyekuwa ndani ya maduara manne ya madini yaliyotitia katika Mgodi wa Msasa uliopo Kata ya Runzewe Magharibi wilayani Bukombe, hivyo hakuna madhara ya kibinadamu.
Polisi wamesema mmoja wa wakaguzi alibaini kibanda kilichokuwa karibu na maduara hayo kimeanza kutitia, hivyo akatoa tahadhari kwa wenzake waliokuwa ndani ya eneo hilo na kufanikiwa kutoka nje salama.
VIDEO:
📍IKULU DSM - Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), CPA Charles E. Kichere ya Mwaka 2024/2025 iliyosomwa leo Machi 30, 2026, Ikulu Dar es Salaam imebainisha kuwa Kampuni ya Ndege ya ATCL imeendelea kupata hasara, ambapo kwa mwaka 2024/25 imepata hasara ya Bilioni 191.19
CAG Kichere amesema hasara hiyo ni ongezeko la asilimia 108, huku akibainisha kuwa hasara imefikia jumla Bilioni 748, toka Shirika hilo kuanzishwa licha ya kupatiwa ruzuku na Serikali kwa ajili ya mishahara na gharama za uendeshaji
Kikao cha 356 cha Baraza la uongozi cha @ilo.org kinaendelea hapa Geneva. Kama nchi mwanachama, Tanzania 🇹🇿 inashiriki kikao hicho. Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano Bi.Zuhura Yunus (Kati). Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara hiyo Bi. Chiku Kiguhe. Kulia ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Mashirika ya Kimataifa Balozi @HoyceTemu
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Francis Chalamila, leo Machi 30, 2026 amewasilisha taarifa ya mwaka ya utendaji kazi wa TAKUKURU kwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo amesema wamebaini kasoro kwenye matumizi ya rasilimali za umma katika utekelezaji wa miradi 913 ya maendeleo na tayari miradi 66 kati ya hiyo imeanzishiwa uchunguzi.
Chalamila amesema “TAKUKURU ilifuatilia matumizi ya rasilimali za umma katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ipatayo 1864 yenye thamani ya Tsh trilioni 14.3, miradi 913 imebainika kuwa na kasoro na miradi 66 kati ya hiyo imeanzishiwa uchunguzi”
“Tumebaini kuwepo kwa usimamizi dhaifu wa mikataba unaosababisha miradi kutekelezwa kwa kutozingatia matakwa ya mkataba husuika , Wakandarasi kulipwa fedha kwa miradi ambayo haijatekelezwa, kutokatwa kwa kodi ya zuio katika baadhi ya miradi, ubora wa vifaa usioridhisha na kutozingatiwa kwa sheria ya manunuzi ya umma”
“Dosari hizi zimekuwa zikijirudia, nawakumbusha wenye dhamana ya kusimamia miradi hii ikiweno Makatibu Wakuu wa Wizara, Makatibu Wakuu wa Mikoa , Wakuruyenzi wa Hlamshauri na Viongozi wa Taasisi za Umma kuimarisha usimamizi wa miradi ili kuondoka na dosari zinazojirudia kila mwaka”
#MillardAyoUPDATES
Breaking News:
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilwa Kusini Seleman Bungara (Bwege) amefariki Dunia mchana huu, akiwa kwenye Hospitali moja ya binafsi huko Kigamboni, Dar es Salaam,
Jambo TV imezungumza na Abbas S.A. Bungara ambaye ni Kaka wa marehemu, ambapo amesema marehemu alifikishwa Hospitalini hapo kwaajili ya kufanyika Dialysis kama ilivyokuwa ikifanyika kawaida, na ndipo umauti ulivyomfika,
Amesema kwa sasa mipango ya mazishi inaendelea, na taarifa zaidi zitatolewa hapo baadae ila msiba (kwaajili ya watu kuhani) ni Temeke nyumbani kwa Abbas Bungara,
Enzi za uhai wake marehemu Bwege amewahi kutumikia vyama vya siasa vya CUF, ACT Wazalendo na hivi karibuni alitangaza kujiunga na CHADEMA, ingawa mchakato rasmi wa kukabidhiwa kadi ya chama hicho ulikuwa haujakamilika.
NB: Jambo TV itakuletea taarifa zaidi kuhusiana na msiba huo.
Rais Samia Suluhu Hassan amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba kuyataja mashirika na taasisi zinazofanya vibaya zaidi katika ripoti ijayo ili zione aibu.
Waislamu nchini Saudi Arabia wamekamilisha siku 30 za mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan leo Alhamis, Machi 19, 2026 hivyo kesho Machi 20, 2026 itakuwa Eid ul-Fitr.
Ibada ya Eid Nchini Saudi Arabia inatarajiwa kufanyika dakika 15 baada ya jua kuchomoza kesho Ijumaa ikiwa ni mwanzo wa sherehe ya Eid Al-Fitr ya wiki nzima katika Ufalme huo.
#KitengeUpdates
🌍 #Cybiant highlights how strategic Public-Private Partnerships (#PPP) drive Tanzania’s Vision 2050. Through training and stakeholder engagement, they strengthen governance, build capacity, and enable sustainable infrastructure and economic growth.
🔗 https://t.co/DhKgik1KtK