Hii Nguvu Kubwa Kwa Kiwango Hiki Kwenda Kumkamata Mhe. @HecheJohn Mnafikiri Inaweza Kututishia?
Polisi Tumieni Nguvu Hizi Kupambana na Mafisadi Wa Nchi Wanaokula Rasilimali zetu, Acheni Kutumika Mnaumiza Taifa Letu, Chuki Inaongezeka Sana, Afande IGP Tambua Jeshi la Polisi Linaharibikia Mikono Mwako Rasmi.
Makamu Mwenyekiti CHADEMA akamatwa na Polisi. CHADEMA ilikuwa ifanye mkutano leo KARIAKOO , TAARIFA ya Mkutano ilipekekwa Wiki Moja Iliyopita na Mkutano ulianza kutangazwa. Leo Mchana Polisi wameleta barua kuzuia mkutano kufanyika Kariakoo. Makamu Mwenyekiti Kamanda John Heche alienda eneo la mkutano kuendelea na mkutano, alipofika Polisi walimzuia na wamemkamata na kwenda naye pasipo julikana, tunafuatilia , habari zaidi tutawaleteeni muda sio mrefu.
"Shida sio kwamba watu wetu wanaenda kuumizwa, shida ni kwamba twende ili tupate ruzuku, hiyo ruzuku inafika Masas? Na hayo maisha ya watu? Maisha ya watu kumbe ni ruzuku kwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi?
Nilidhani kwenye uchaguzi ni kwenda kutafuta viongozi! Kumbe kuna watu wanawaza pesa, hawajali watu kufa (kwenye uchaguzi), ndiyo hivyo? Hakuna mabadilko, hakuna uchaguzi" @TunduALissu
Masasi, Mtwara, leo, Aprili 07, 2025
#NoRefomsNoElection #NIMO
Unakua na serikali inasema zao la mkonge limekufa!!! Wameua mashamba yote ya Lindi na Mtwara, Tanga uzalishaji unasuasua.
Wakati huo huo tunaagiza magunia ya kubeba korosho kutoka India kwa mabilioni ya shilingi.
Unawezaje kujenga ajira kwa watu wako kama huwezi hata kuzalisha magunia ndani ya Nchi yako?
Katibu Mkuu wa Chama Mhe. @jjmnyika amefungua mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa Chama na Mabaraza wa Mikoa na Kanda ya Magharibi leo tarehe 08 Aprili 2025. Mafunzo hayo yatakuwa ya siku mbili Aprili 08 - 09, 2025.