(Alivyokuwa mjengoni utamsikia anasema "vijana wajiajiri serikali haina ajira"
Kaja kutia Nia "vijana mnipe nafasi nitaenda kuwasemea muajiriwe hii nchi ni Tajiri sana"
Ndugu mtia Nia hii sio 2005 ni 2025)
Mwenyekiti NETO-Paul Joseph Kaheza✍️
@NETO_TANZANIA inatamani na inashauku ya kupata majibu yatakayoweza kuponya mioyo yao iliyovunjika kwa muda mrefu, tunafahamu serikali uwezo wa kuajiri inao na haitakuja na visingizio visivyokuwa na msingi wowote katika Taifa, hii italeta tafsiri mbaya na italeta sintofahamu
Saa chache zinaelekea kutamatika na sasa @NETO_TANZANIA wanaitizama serikali kwa jicho la kipekee sana kuelekea kupata majibu kutokana na kikao kilichofanyika tarehe 12 Machi mwaka huu, Umoja wa walimu wasio na ajira una matumaini makubwa sana kwa viongozi
Ikumbukwe kuwa dhamira kuu la kuanzishwa kwa NETO ni kudai haki ya ajira kwa walimu wasio na ajira kwa mwaka 2015 hadi 2024 pasipo kuvunja sheria za nchi, na NETO inafuata na itaendelea kufuata taratibu zote za kisheria kuhakikisha kwamba dhamira hiyo inafanikiwa kwa kias kikubwa