Mwanamke kuanzia anapo vunja ungo mpka kufikia miaka 24/25 anatakiwa awe ashatimiza ndoto zake richa ya Apo ataanza kuishi kwenye ndoto za wengne Tofauti na mwenaume ✍️
@baraka_asege Bangi mbaya mshujaa hana uchumi wa kupanda ndege kg to pemba afu baada ya siku 3 ande mbeya then siku 3 aende kagera kucheza na kagera sugar
SHULE YA MAOMBI
[PETITIONING PRAYERS]
23
SIFA ZA MAOMBI YA MAHITAJI
IMANI
Sehemu ya tatu
Mchakato wa kutuma na kuwa na uhakika kwamba maombi yamefika mbinguni ni muhimu sana. Nilikuambia uhakika unatoka kwenye ufunuo/uvuvio wa Neno la Mungu.
1 Yohana 5:14-15
14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.
Nilikuambia mapenzi ya Mungu huja unapopata nuru/mwanga kwenye wa maandiko. Ule mwanga ndio unakupa kuona uhai na uhalisia wa Maandiko. Kwa hiyo kuingia kwa nuru ya maandiko ndani ya roho yako huzaa kitu ambacho ni halisi na kukugusika. Moja ya zao la kuingia kwa nuru ya maandiko kwa Roho Mtakatifu ndani yako hukupa ufahamu wa kiroho wa kitu unachosoma.
Psalms 119:130 The entrance of thy words giveth light; it giveth understanding unto the simple.
Utaisoma kwa kiswahili ila haina maana iliyokusudiwa kama kingereza, tunaweza kusema inamanisha kuingia kwa Neno lako hutoa nuru na kuwapa ufahamu [wa kiroho watu].
Unapoomba unakuwa na ufahamu wa kiroho ndani yako ambao unakusaidia kuomba. Huwezi kuombea kitu ambacho hufahamu kibiblia, ndiyo maana unatakiwa kusoma Neno la Mungu kwa bidii zote.
Neno la Mungu linapoanza kukugusa kwa sababu limekua hai ndani yako kuzaa kitu kingine ambacho ni muhimu sana. Neno la Mungu huumbika ndani yako. Kuumbika ni lugha ambayo inakupa kujua uzito wa kitu kilichoingia ndani yako. Uzito huo hutoa msukumo wa kimatendo wa kimaombi na mwenendo. Ukiwa unaomba kutoka kwenye huu mkao una uhakika unaomba kwa kutumia kitu kilichoingia ndani yako. Huwezi kukosa uhakika wakati ufahamu na mimba ya Neno la Mungu vinekua halisi ndani yako, automatically utajua Mungu anakusikia.
Neno la Mungu linapoumbika ndani yako hukaa kwa kitambo. Ni kitu cha kiroho [spiritual substance] ambacho kinavimba moyoni na kukusukuma kukitendea kazi kiroho. So wakati unaomba unakua na uhakika 100% unafanyia kazi kitu fulani. Bila uvuvio/ufunuo wa Neno la Mungu ni vigumu kupata uhakika kwamba Mungu anasikia. Ni vigumu sana kujipatia hakika kitu gani unafanyia kazi au kazi ya maombi imefika wapi. Ukifika hapa utajua, unaweza ku-trace kazi ya maombi imefika wapi. Inapoisha unapata mrejesho hapo hapo kwamba kwamba umemaliza maombi kwa sababu ile mimba ya Neno la Mungu rohoni hupungua na kupotea So swala la kupokea majibu/Mungu kukujibu siyo kitu cha kufikirika au kutojua itakuaje au kuwa desperate kama Mungu atajibu au hatajibu. Mambo ya Kiroho can be traced/recorded.
Msukumo wa Neno la Mungu huzaa nguvu ya Neno la Mungu. Ile nguvu hugusa nafsi yako, mifupa na nyama. Neno la Mungu linapenya na lina nguvu. Nguvu ya Neno la Mungu ndiyo linakupa kufuatilia. Unajua nimetumia nguvu kiasi gani katika ulimwengu wa roho. Mambo yanapokaribia utaona nguvu za Neno la Mungu ndani yako zipungua, mzigo kushuka maana yake unakaribia kupokea majibu. Unaweza kujua umepika maombi yako kwa kiasi gani. Unakua kuna watu wanachukulia maombi kama kitu kisichoeleweka[uncertain]/cha kubahatisha[unpredictable]. Maombi ni kazi rasmi[official work]. Though kuna mahali utaanzia ila kadri unavyokua kwenye maombi utajua kazi ya maombi ni kazi rasmi. Ni kazi anayaoeleweka. Unajua pa kuanzia na pa kuishia. Utajua jinsi ya kuomba na kusababisha majibu.
Ufunuo/uvuvio wa Neno la Mungu unatabia hizo kwa kiufupi. Lengo ni kukuhakikishia kazi yako ya maombi. Usije kufanya maombi kwa kubahatisha. Akina Paulo walisema hawapigi hewani, kwa kubahatisha bali wanalenga tageti zenyewe kwenye maombi. Uhakika huu ndo Imani. Imani hukua mpaka pale inapozaa majibu. Kwa hiyo mapenzi ya Mungu hujulikana kupitia Ufunuo/nuru/mwanga wa Neno la Mungu. Na Imani huanza mapenzi ya Mungu yanapojulikana. Hii ndiyo nguvu ya maombi.
@EliabuDanford@rugilandavyi Mwana wa Mungu samahani m napenda kufunga ila ttzo nikifunga nguvu za kuomba zinaniishia nakuwa dhaifu tofauti nikiwa nimekula naomba sana bila kuchoka