BABA PAROKO AMETEKWA
HUKU NGURUKA UTEKAJI UNAENDELEA,NDANI YA SIKU 7 ZILIZOPITA WAMETEKWA WATU WATATU BAADHI YAO NI WAKEREKETWA WA MASUALA YA SIASA KWENYE VIJIWE VYA KAHAWA AMBAO NI
1.VEDASTO MFANYABIASHARA NGURUKA
2.SELULE HUYU NI KADA WA CCM
NA PAROKO WA PAROKIA YA NGURUKA PR.JOSEPHAT MISIGARO ambaye inasemekana ameponzwa na mahubiri yake jumapili iliyopita ..
Hapa ni NGURUKA wilaya ya Uvinza kigoma
Hali ni ya UTEKAJI ni hivo hivO KATIKA vijiji viñgine kama MPETA NA MLYABIBI
Inaonekana sasa UTEKAJI ni jambo la kitaifa...mtusaidie kupaza sauti
Kwanza kabisa sisi kama VIJANA WA GEN-Z sio vichaa na hatuna njaa hivyo kama unavyoielezea kwenye hotuba yako.
MADAI YETU.
1. TUNATAKA HAKI YA KUISHI.
Serikali yako imekuwa kinara kwenye kuteka wakosoaji wako. Hiyo ndio njia pekee unayoona inafaa kushugulika na wakosoaji wako. Hii sio sawa, na tangu umeanza kuwateka hujifunzi WAKOSOAJI wako hawaishi ndio wanaongezeka kila siku.
2. TUNATAKA HAKI YA KUCHAGUA VIONGOZI TUNAOWATAKA.
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na sio nchi ya KIFALME au KIDKTETA. Kwa chaguzi 2 MFULULIZO tumenyimwa HAKI ya kuchagua na kuchaguliwa kwa uhuru na HAKI. Yalitolewa mapendekezo ya kuwa na chaguzi HURU NA HAKI ukapuuzia (NO REFORMS NO ELECTION).
3. TUNATAKA UWAJIBIKAJI.
Serikali yako imekuwa inaongoza kwa UFISADI na kiongozi wa HUO UFISADI NI MWANAO ABDUL. Ushihidi lukuki umetolewa kuhusu UFISADI unaoendelea nchini ila umetupuuzia. Kibaya zaidi unafanyika UFISADI wa kutisha huku wananchi tunakosa huduma nzuri za MUHIMU.
4. TUNATAKA KATIBA MPYA.
Katiba Wewe uliita ni “Kiji kitabu” ndiomaana huiheshimu. Kama tungekuwa na KATIBA nzuri wewe hukustahili kuwa Raisi kwa uliyoyafanya OKTOBA 29. Tunaihiyaji KATIBA mpya TUKUWAJIBISHE.
5. TUNATAKA UHURU WA KUTOA MAONI.
Serikali yako imekuwa kinara wa kukandamiza VYOMBO VYA HABARI, WAANDISHI WA HABARI na MITANDO YA KIJAMII. Umegeuza vyombo vya habari kama KASUKU wa kutupigia kelele ya sifa zako tuu.
Mitandao ya kijamii ambayo inaongoza kukukosoa UNAIFUNGIA kama X. Na unafika Mbali KUTEKA wote wanaokukosoa hutaki kabisa kusikia wakosoaji masikioni mwako.
Hayo ndio mambo matano ambayo UNAYAJUA NA UNASUMBUA WASTAAFU kwa kuiita “Tume huru” wakachunguze. Afu acha kutona sisi maskini sana kiasi cha kuamua kuchoma nchi yetu kisa kulipwa. TUHESHIMIANE TAFADHARI.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Habil na kabil jana kasema tu download Proton VPN..soon atatoa internet ya bure bila MB ata wakizima mtandao sisi tutapeta.
So tufanye hivyo msije sema sikuwaambia✌️✌️
Repost bila kuchoka ✌️
Waandamanaji South Africa wakiwa wamebeba picha za mauaji yaliyotokea Tanzania, kupinga mauaji Aliyoyafanya Samia nchini.
Madam yao
1.Uchaguzi ufutwe
2.Samia ashtakiwe kwenye mahakama ya ICC kwa mauaji Aliyoyafanya
3.Katiba Mpya
Hongera Mwenyekiti wa CHASO DIT, @DarChaso ina jivunia kuwa na wewe.
Wanafunzi wanakosa wa kuwasemea kwa sababu @TahlisoOfficial imetekwa na kikundi cha watu
Tuwasemea wanafunzi, hatutaacha mpaka tahliso itakapokuwa huru #NoReformsNoElection
Huyu kijana mdogo ametekwa na kupotezwa Soka alijua na akasema na bado serikali ya Rais @SuluhuSamia ikapuuza na leo Soka hayupo.
Sio kweli kwamba tutanyamaza kwasababu ya kutekwa na kupotezwa, kelele itazidi kuwa kubwa.
Iko siku wote mnaofanya haya mtasema mbele ya Watanzania kwanini mlifanya uovu huu kwa binadamu wenzetu.
Tuna taka mawakala wa vyama vya siasa waruhusiwe kuwa na mawasiliano na wagombea wao pamoja na chama chake kwa utaratibu utakaopangwa ,kama ambavyo wengine wanaohusika katika chumba hicho kuwa na mawasiliano (simu).
No Reforms No Election.
Wanachama wa CCM ni zaidi ya milioni 10. Huu si wakati wa kunyamaza. Mna haki, mna sauti — itumieni bila woga.
#KataaWahuni 👊🏽👊🏾👊🏿
#NoReformsNoElection
NI ZAMU YA VYOMBO VYA HABARI..?
Waandishi wa habari nguli na maarufu wa radio na TV maarufu hapa Jijini Dar es Salaam wamefungiwa na Bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) kutangaza au kufanya kazi ya uandishi wa Habari kwa kile kinachoitwa "kushindwa kujisajili katika bodi ya ithibati"
Mpaka naandika habari hii Wahusika na mwaajiri wao wamefanya siri kwa mujibu wa maelekezo waliyopewa na serikali kuwa "wasifanye kazi ya uandishi wa habari na wasiseme lolote kuhusu kuzuiwa kwao"
Kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229 kina weka masharti kuwa
"waandishi watakaoshindwa kujisajili hawataruhusiwa kufanya kazi za kihabari"
Waandishi hawa wamewekewa kikwazo hiki baada ya kuwa mwiba katika vipindi vyao na mahojiano yao kwa wakati huu nchi inapoelekea katika uchaguzi Mkuu
Uchunguzi unaonyesha Masoud Kipanya ameingia katika kifungo hiko baada ya kuchora mchoro wa katuni uliowakasirisha watawala uliolenga kutaka media zisitumike kama Toilet Paper
Mwenyekiti wa Jukwa la Wahariri Tanzania Balile aliongea na kuonyesha hadharani kukasirishwa na mchoro huo huku akiahidi Masoud Kipanya achunguzwe na mamlaka za nchi.
Masoud Kipanya na Ciza Wameshindwa kujisajili kwa sababu ya kukosa sifa ya kusomea taaluma ya uandishi wa Habari kinyume na sheria kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 24 cha sheria ya huduma za habari sura ya 229.
Rungu la namna hii pia linaonekana kumkumba mwanahabari na Mkurugenzi wa Jambo TV, John Marwa ambaye amekuwa mwiba katika mahojiano mbalimbali na kuendesha vipindi vilivyo wakwaza watawala.
Duniani kote watu wenye uzoefu na kazi ya uandishi wa habari kwa zaidi ya miaka 10 kama Masoud Kipanya, SIZA, na John Marwa walipaswa automatically kuwa na sifa za kusajiliwa na bodi ya ithibati ya Waandishi wa Habari kwa kigezo cha uzoefu na muda waliofayia kazi tasnia ya habari.
Hawa ni baadhi ya Waandishi wa Habari wakubwa Duniani ambao hawakusomea taaluma ya uandishi wa Habari Anderson Cooper (CNN na ABC News) Stephen A. Smith (ESPN) na Trevor McDonald (ITN na ITV)
N.B
Kwa upande wa mmoja mtangazaji maaurufu wa radio na Tv kutoka ofisi hiyo hiyo, kwake maarufu kama imekuwa tofauti kidogo. Pamoja na kukidhia sifa zote za Sheria ya Huduma ya Habari na Kujisajili katika Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari
Wenye Mamlaka wamepiga simu kwa mwajiri wake na kumtaka aondolewe katika majukumu yake kwa kile walichokiita "mkosoaji sana"
Boniface Jacob
The voice of the Silenced Majority.