Hii ndio inavyotakiwa, wastaafu watoe matamko kama haya ya kuweza kuli-shape taifa na watawala. Hamkuiacha Tanzania ilivyo leo, Tupo kwenye hali ya hatari Amka!
Ni kweli kabisa. Hawa ni watu ambao ni wazi hawakulelewa vizuri na wazazi wao na walijingiza kwenye chama chao kinyemela. Ni watu ambao inaelekea hawakujifunza chochote kutoka kwa Mwalimu Nyerere bali wanapinga kila kitu alichokisimamia Mwalimu Nyerere na wanasema Ikulu si sehemu takatifu kwani kwao ni pango la Wanyang'anyi na kujitajirisha.
Wanaamini kuwa kila aliye serikalini ale kwa urefu wa kamba yake. Hivyo kamba ya Mkuu na Mktugenzi wa Wilaya insidhia katika wilaya yake. Mkuu wa Mkoa ni mkoa wake; Waziri ni Wizara yake na Raisi ni nchi nzima!
Kwa hawa watu uchaguzi si shughuli takatifu ambapo Wananchi wanachagua viongozi kwao ni udanganyifu mkuu. Mjanja na mbabe anayeweza kutumia dola na ubabe ndiye anakuwa kiongozi. Hivyo hata mchakato wa uchaguzi katika chama chao ni udanganyifu mtupu kwani mgombea wa chama hicho, kisicho na maadili, anapatikana kwa kushitukiza kupitia mkutano usio wa uteuzi na mgombea huyo ndiye anakuwa mwenyekiti wa mkutano huo!
Mgombea huyo ambaye alidaiwa kuchangiwa fedha za kuchukua fomu na wananchi wa makundi mbalimbali kwa kipindi cha miaka miwili nyuma hata fomu hiyo hakuchukua kinyume na Katiba ya chama hicho kisichofunzwa na mamaye. Mgombea huyo hakuwa hata na staha ya kurudisha fedha hizo kwa wananchi hao vimbelembele.
Mgombea huyo hakuridhika kupitia serikali yake akaamua kumuweka ndani kiongozi mkuu wa upinzani anayepigania mabadiliko ya kweli ya demokrasia na kumfungulia Kesi ya uhaini. Na kukifungia chama cha mpinzani wake kupitia kesi ya mamluki wa chama hicho iliyoendeshwa na mahakama kwa kasi ya ajabu.
Ni mgombea aliyehakikisha vyombo vyote vya habari vinaiba nyimbo za mapambio ya kumsifu kuwa Dunia nzima hakuna kiongozi kama yeye na kufikia hatua ya kumuita "Mama wa Taifa"! Hakuna kuandika habari yoyote hasi dhidi ya Mgombea huyu aliyetukuka sana.
Ni mgombea aliyeweka mabango ya kampeni zake kwa miaka mitatu mfululizo kupitia njia ya kuadhimisha mwaka wa kwanza,wa pili, wa tatu na wanne wa utawala wake na kupewa Kila aina ya sifa. Mwaka 2025 nchi ikashamirishwa na picha zake akipewa sifa kede kede. Mara: "Muadilifu, Mama Hana Deni, Mtu wa Watu, Msikivu, Mnyenyekevu, na Mpatanishi". Yaani ni sifa za Mtu anayejua kila kitu hata Kim Jong Un, yule Raisi wa Korea Kaskazini, lazima amuonee wivu.
Mgombea huyu akawafikia wananchi kwa motisha za ajabu kwani kinyume Cha Sheria za nchi zinazokataza rushwa na takrima akagawa pikipiki na baiskeli. Akatoa michango mikubwa mikubwa ya ujenzi wa makanisa japo hakututajia za misikiti kwani huko alitoa kimya kimya.
Vyombo vya dola navyo akavitumia kikamilifu kufanya kampeni zake. Kila mkutano wa kampeni wake na viongozi wa kitaifa wa chama chake wafanyakazi wa serikali na wanafunzi ilikuwa ni lazima wahudhurie. Aliyekosekana huyo ni mpinzani wa Kiongozi Wetu Mkuu na Chama chetu kikubwa barani Afrika na alishughulikiwa.
No mgombea ambaye kampeni yake ilihanikizwa na usombaji wa wasikilizaji. Malori na mabasi yakatumika kuwasomba watu kuhudhuria mikutano yake ya kampeni na wahudhuriaji hawa wakasombwa kutoka vijiji, kata, wilaya na mikoa jirani. Ikajaa pomoni. Akasema kuwa Watanzania wanampenda haijawahi kutokea.
Akasema kuwa wanaopanga kuandamana siku ya tarehe 29 Oktoba wakumbuke yeye ni "Amiri Jeshi Mkuu na kuwa maandamano pekee anayoyatambua ni ya kwenda kupiga kura basi. Akaendelea kusema siku hiyo ya uchaguzi hakutakuwa na ,"nywinywi Wala nywinywinywi".
Siku hiyo ikafika kiongozi huyo kipenzi Cha watu na wafuasi wake wasio jaa katika mkono ndio waliopiga kura. Mamilioni ya Watanzania wakalinda kura zao kwa kubakia majumbani mwao. Malaki ya vijana (Gen-Z) wakaandamana. Jeshi la polisi na vyombo vingine vya Dola vikaua maelfu ya Watanzania na nchi ikawekwa lockdown ikiwa ni pamoja na mitandao kuzimwa kwa siku Tano. Ajabuye Tume ya Uchaguzi iitwayo Huru, wakati si huru hata kidogo, ikatutangazia matokeo kuwa mgombea huyo Kashinda uchaguzi kwa 98%.
Ndiyo maana wahenga wakasema "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu."
@MabalaMakengeza Kwann akutengeneza Katiba Bora kabla yakung'oka ni kweli hakujua Kuna wahuni wanaweza kuchukua nchi mbona alikuwa na akili na akili sana Leo watoto wetu wanakufa ili watu watawale Mungu mwenye haki tokeza
MTOE MTOTO NJIAN GARI LITAMKANYAGA KWANI MWENYE ELIMU NA CHEO KASHIKA GARI HASIKII WALA HAONI, KAFUNGA KITAMBAA USONI, KAWEKA PAMBA MASIKIONI, ANAENDESHA BILA KUANGALIA.