Anaandika Wakili @Advocate_Kisabo
Leo, Julai 27, 2026, nimemtembelea Mhe. Tundu Lissu Tundu Antiphas Lissu Gereza la Ukonga. Mbali na kunipa maelekezo kuhusu maandalizi ya nyaraka za submissions katika kesi yetu, kufuatia kukamilika kwa maswali ya dodoso Julai 23, 2026, Mhe. Lissu amesisitiza kwamba watu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashitaka ya ugaidi wanapaswa kupata uwakilishi wa kisheria na kutembelewa mara kwa mara magerezani ili kuwafariji, kufuatilia ustawi wao na kujua maendeleo ya kesi zao.
Amenieleza pia kwamba hakuna hata mmoja anayepaswa kusahaulika, wote wanapaswa kutetewa na mawakili.
Nilienda na Wakili Deogratias Mahinyila Deogratius Mahinyila lakini hakuruhusiwa kuingia baada ya maafisa wa Magereza kudai kuwa jina lake halipo kwenye orodha ya mawakili wanaoruhusiwa kumwona Mhe. Lissu.
Mhe. Tundu Lissu anawasalimieni sana Watanzania. Pokeeni salamu zake.
@SuluhuSamia Mhe Rais naendelea kushauri kwa dhati Tundu Lissu aachiwe huru kwani kesi haikamiliki. Hekima na busara iliyokufanya kutangaza sera ya 4Rs mara ulipoingia madarakani ikuongoze tena katika jambo hili. Simulizi hizi za kutisha za vyombo vya habari vya kimataifa, zinaibua hisia kali hasa kwa vijana, hata wazee tumekumbushwa kadhia ya operation Sogeza iliyounda vijiji vya ujamaa 1974 -1976. Taarifa hizi zinaathiri kikubwa taswira ya taifa letu na maslahi yake. Athari ni kubwa. Tutafute muafaka kupitia uwajibikaji na maridhiano. Tuwe na hofu ya Mungu na kutambua miujiza yake mfano wa risasi 16 kushindwa kukomesha uhai ingawa maumivu ni makubwa. Tutubu na kusali kuliombea taifa letu kila mtu kwa imani yake.
Safari ya kuelekea Kilosa katika Operesheni Katiba Mpya na Free Tundu Lissu ilitupitisha Dumila. Huko, wananchi walituomba tumtembelee mzee huyu shupavu. Wanasema bendera kwenye baiskeli yake haijawahi kushuka, ishara ya msimamo na imani yake. Ilikuwa ni heshima kubwa kukutana naye. Kila siku huzunguka na spika hii niliyoibeba, akiendelea kueneza sauti ya kile anachoamini.
HUU NDO UJUMBE WANGU AMBAO NIMEMTUMIA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA, JENERALI JACOB MKUNDA.
👇👇👇👇
Kwako CDF Mkunda,
Ni matumaini yangu kwamba umzima wa afya.
Wewe unaitwa Mkuu wa Majeshi Tanzania kwasababu majeshi yote nchini yapo chini yako kwa mujibu wa Katiba yetu ya Tanzania.
Jeshi lenu linaitwa Jeshi la Wananchi sio Jeshi la Rais wala Serikali kwasababu moja kati ya majukumu yenu ni kulinda Uhuru wetu, kulinda Usalama, na mipaka ya nchi yetu.
Kabla ya Oktoba 29, kuna Wanajeshi kutoka nchi ya Uganda waliingia Tanzania, taarifa zilisambaa kila kona lakini wewe na vikosi vyako vyote mlikuwa kimya licha ya kwamba ulikuwa unajua kuwa kuna uwepo wa Jeshi kutoka Uganda na unajua Katiba ya Nchi hairuhusu jambo kama hilo.
Oktoba 29, tulipoteza Watanganyika wenzetu zaidi ya elfu kumi ambao waliuwawa kwa risasi na waliofanikisha mauaji hayo ni Jeshi la Polisi, TISS, KMKM na Wanajeshi mamluki kutoka Uganda.
JWTZ mmeshindwa kulinda mipaka ya nchi yetu ndo maana Wanajeshi kutoka nchini Uganda waliingia Tanzania kwa msaada wa Jeshi la Polisi Tanzania, na wakapewa majina feki na bunduki ili wauwe Watanganyika wenzetu, mamluki kutoka Uganda, TISS, KMKM, Polisi na baadhi ya Wanajeshi wako walishirikiana kikamilifu kuwamiminia risasi ndugu zetu bila hata chembe ya huruma.
JWTZ mmeshindwa kulinda usalama wetu na usalama wa nchi yetu ndo maana kabla ya Oktoba 29 ndugu zetu zaidi ya 600 walitekwa na kupotezwa na hata baada ya Oktoba 29 hali imezidi kuwa mbaya maana bado watu wanaendelea kutekwa na kupotezwa na wengine tunawindwa kila kona, tunaishi kama digidigi halafu bado nyie mnaguts za kujiita Jeshi la Wananchi, Jeshi gani la Wananchi ambalo haliwezi kulinda usalama wa hao Wananchi wake?
JWTZ mlishindwa kulinda uhuru na usalama wetu, maana kulinda Uhuru na usalama wetu ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha Maandamano ya Wananchi ya Oktoba 29, yanafanyika kwa amani na yanaisha kwa amani, lakini nyie mlitulia tu mkaacha vikosi vya Samia vimwage damu za maelefu ya Watanganyika ambao waliuwawa kwa risasi.
Kibaya kuliko yote baadhi ya Wanajeshi wa JWTZ ambao walionekana wakilinda Maandamano ya Wananchi Oktoba 29 maeneo mbalimbali nchini.
Baada ya Oktoba 29, wewe CDF uliagiza wakamatwe na wafunguliwe kesi kwenye Mahakama ya Kijeshi (Court Martial) mkawabambika kesi kwamba walichochea Maandamano, yani kwa lugha nyepesi ni kwamba wewe CDF, ulichukizwa sana sana kwa kitendo cha baadhi ya Wanajeshi wako wa JWTZ kulinda Wananchi ili wasiuwawe kwenye maandamano ya Oktoba 29, means ulifurahishwa sana na mauaji ya Watanganyika wenzetu siku ya Oktoba 29.😭
Mahakama ya kijeshi ( Court Martial) iliwatia hatiani Wanajeshi ambao walijitolea kulinda Wananchi siku ya Oktoba 29 ili wasiuwawe, Yani wanajeshi ambao walijitolea kutulinda Oktoba 29, Wamefungwa wapo magereza wanasota wakati huo Viongozi wa ulinzi na usalama walioshiriki kuuwa kwa risasi Watanganyika zaidi ya elfu kumi wapo mtaani wanatamba bila wasiwasi licha ya kwamba hata wewe mwenyewe unawajua kwa majina na sura zao.
Hii dhambi itakutafuna wewe na kizazi chako mpaka siku unaingia kaburini.
NB. Hii video ambayo nimekutumia hapa huyu ni Mwanajeshi wako wa JW, kamvua nguo raia na kumtesa hadharani, huu ndo ukatili ambao baadhi ya Wanajeshi wako walikuwa wakiwafanyia watu siku ya Oktoba 29, hili tukio lilitokea Tunduma siku ya Oktoba 29z
Ndimi Hilda Newton,
Mwanachama wa Chadema na Mwanaharakati wa Haki za Binadamu.
Nchi yetu inafurahisha sana. Fikiria eti Serikali imewashtaki watu hawa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kigoma kwa kusema " mauaji ya 29 Oktoba 2025 hayawezi kufichwa na tume ya Uchunguzi" hapa kosa lao ni nini? Hivi tume ilisema wale 518 walijiua?
Nitawatetea watu hawa.
Watanzania watakomesha huu ujinga very soon..
Wote mnaofanya haya mtakosa pakukimbilia, haiwezekani mtekaji akajichunguza mwenyewe..
Kitendo walichofanya polisi kimeondoa mashaka yote, kwa mtu yeyote aliyekua haamini namna hii dola dhalimu imeoza na inavyofanya vitendo vya kijambazi dhidi ya raia wema.
Nasuburi Chande aseme mpenzi mwenye pingu, au mshirikina anaeteka raia kwa pingu.
Naibu Katibu Mkuu Bara wa @ChademaTZ2 Amani Golugwa ameeleza alivyoshangazwa na kauli ya ZCO, Afande Faustin Mafwele mara baada ya kuongea nae na simu juu ya ukamatwaji wa msaidizi wa Tundu Lissu.
Natoa pole nyingi sana kwa Msaidizi wa Mheshimiwa Tundu Lissu, Ndugu Jumbe, kufuatia tukio baya na la kinyama lililomtokea. Huu si utamaduni wa Watanzania, wala si maadili yanayopaswa kupewa nafasi katika jamii yetu.
Tofauti za kisiasa zisigeuke sababu ya chuki, vitisho, au mashambulizi dhidi ya watu. Taifa lenye afya ya kisiasa hujengwa juu ya ushindani wa hoja, heshima ya utu wa binadamu, na kulinda haki ya kila mtu kuwa salama bila kujali itikadi yake.
Wananchi, wakati umefika wa sisi sote kupaza sauti na kukemea matukio ya aina hii bila kujali tofauti zetu za kisiasa. Ukimya mbele ya uovu unaweza kuupa nguvu uovu wenyewe.
Namtakia Ndugu Jumbe uponaji wa haraka na nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia naomba vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka, wa haki, na wa uwazi ili wote waliohusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara @HecheJohn akielezea hali ya Afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Tundu Lissu alieko gereza la Ukonga kwa kesi ya kuchonga.