Kabla sijalala. I wanna see if yβall can show some love to SC Tundu Lissu. Today been a great day. Letβs give the defiant TAL his flowers. Top lad!βοΈππΌ
Amekuwa jela kwa siku 118. Lakini amejiandaa kufundisha sheria. Na kuonesha akili ndogo za serikali. Na kwamba yeye si mhalifu. Leo Hakimu na Mawakili wa dola wanalala na viatu. Huyu ndiye mwalimu wetu, kaka yetu, ndugu yetu, mwenyekiti wetu, SC Tundu AM Lissu.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 14
Anaendelea Mhe. Lissu
Lissu ameulizwa je utakuwa na mashahidi wangapi?
Mashahidi wangu watakuwa kama ifuatavyo
1. Samia Suluhu Hassan atakuwa ni shahidi wangu wa kwanza
Hakimu anasema anasema kuna taarifa inasambazwa muda huu, anasema kuna watu wanasambaza taarifa za hii kesi.π
Lissu anednelea na kutaja mashahidi wake.
1. Samia suluhu Hasaan apelekwe summons.
2. Philip Isdory Mpango ni msaidizi wa serikali aje atoe ushaidi nilivyowatisha.
3. Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu nimesmtishia serikali aje atoe ushahidi
Hakimu anasema kwa vile sheria hailazimishi kukulazimisha utaje mashahidi wako utaomba Kibali cha mahakama kuu mimi siwezi kuwaandika hao mashahidi wako.
Hao mashahidi unaowataja utawaomba mahakama kuu mimi siwezi kuwaandika hapa.
Hakimu amekataa mashahidi wa Lissu anasema akawaombe mahakama kuu yeye ni mjanja pia hawezi kuingia huo mkenge.
Hakimu anasema hii safari haikuwa ndogo ilikuwa ndefu kwelikweli. Haisikilizi shauri wala kutoa maamuzi.
Hivyo basi mahakama haikuwa inasikiliza shauri kabisa.
Kwa mujibu wa kifungu cha 263 ninakupeleka mahakama kuu kwa tarehe ambayo itakuwa imepangwa kwa tarehe ambayo itasemwa na msajili wa mahakama kuu.
Kwa leo tumehitimisha hapa so tukutane Mahakama Kuu.
Naomba Repost yako.
Mahakamani pamechafuka sana Leo.. π
TAL ameambiwa ataje mashahidi wake kama anao. TAL amemtaja SSH, Mpango na Majaliwa katika orodha ya mashahidi wake. Hakimu Franco Kiswaga akasema hao mashahidi ataomba kibali Mahakama Kuu waingie kwa kuwa hawezi kuwaingiza katika commital.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 11,
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa naomba nizungumzie kesi yenyewe sasa.
Kwa kuanzia baada ya kusikiliza information ilivyosomwa yote baada ya kusoma haya maelezo yote.
Cha kwanza ninachoweza kusema ni kwamba
Hapa hakuna uhaini.
Pili hapa hakuna kosa lolote la jinai.
Hakuna uhaini na hakuna kosa lolote la jinai.
Mashitaka yanasema nimefanya kosa la uhaini.
Kifungu cha 39(2) (d) cha penal code kinatengeneza kosa la aina gani?
Ni kweli mimi ni raia wa Tanzania lakini nia ya kufanya uhaini ni kuzuia uchaguzi, kuvuruga uchaguzi, imesemwa imerudiwa imerudiwa.
Je kuzuia uchaguzi ni kosa la uhaini? Au wanasema wakiyatoa wapi?
Kifungu cha 39 kinasemaa uhaini ni kutishia Bunge, Serikali na Bunge.
Kuzuia Uchaguzi sio uhaini.
Kwa sheria za Tanzania kuhamasisha kuzuia Uchaguzi sio uhaini labda wawe na sheria zao binafsi huko sirini.
Sheria ya Uchaguzi imetengeneza makosa ya Uchaguzi imeandikwa kiswahili.
Hakuna kosa linaloitwa kuzuia uchaguzi.
Hakuna kosa la kuvuruga uchaguzi.
Sio jinai kwa mujibu wa sheria.
Nashangaaa inakuwaje uhaini kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi?
Hebu nyie mawakili wa serikali mseme inakuwaje uhaini?
Mheshimiwa utakumbuka tangu mapema kabisa kwamba hii kesi sio kesi ya kwanza ya uhaini Tanzania ni kesi ya nne.
Kwahiyo tunayo Precedent ya Mahakama ya afrika mashariki na mahakama ya rufani ya Tanzania zote zinaeleza kuhusu mambo ya uhaini.
Tunamuomgozo wa kesi ya uhaini inavotakiwa kuwa na Muongozo wa Mahakama ya rufani on how to frame a charge of treason.
Mwongozo unasema pawe na statement of the offence, particulars and overt act hiyo nia iwe na tendo la wazi.
It must be pleaded, Utekelezaji lazima uwepo na uelekezwe.
Wamekoroga mashitaka hayaeleweki, haijulikani overt act ni ipi? Walichokifanya hapa ni mkorogo maana hakuna charge hapa.
Jambo lingine muhimu kuhusu hii information ni kwamba maelezo Mheshimiwa Lissu alisema alisema alisema.
Swali ni kwamba Je maneno peke yake yanatengeneza uhaini? Maneno matupu yanatengeneza uhaini?
Kwa mujibu wa mahakama ya rufani Khatibu Gandi ilisema maneno matupu hayatengenezi uhaini isipokuwa yanatengeneza kosa la uhaini.
Kuzuia uchaguzi sio kosa la uhaini na sio kosa la jinai.
Hakimu anasema mimi pia leo nitapata relief wewe kuondoka kwenda mahakama kuu kwahiyo naomba naomba ujielekeze pia kwako na wewe utunze muda.
Mhehsimiwa naomba niendeleee nisipotezewe muda tafadhali sana.
Je Tundu Lissu peke yake anatosha kutenda kosa la uhaini?
Hili kosa nimeshtakiwa peke yangu na hakuna mtu mwingine kabisa.
Kwanza sheria inataka nifanye publication kwa watu wengine kuhusu huo uhaini na mipango yake. Sasa mimi hakuna mahali nimefanya publication. Wanasema JAMBO TV ndio walichapisha hayo maneno.
Hakuna aliyesema kuwa Tundu Lissu amemtishia Rais, Bunge au mahakama? Hakuna hata mmoja amesema hivyo. Wote wamesema tutazuia uchaguzi tutafanya vurugu.
Pia maelezo ya mashahidi hakuna aliyesema zaidi ya maneno niliyosema nilitenda kitendo kingine chochote. Hakuna aliyesema hata mmoja.
Part 12, itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 10
Anaendelea Tundu Lissu
Nilishiriki pia katika Bunge maalumu la Katiba la mwaka 2014 na 2015 nikawa mbunge pia.
Nilitumikia nafasi hiyo sikumalizia Tarehe 07/09/2017 nilishambuliwa kwa risasi nyingi na kupelekwa nje kwa matibabu nikafutiwa ubunge wangu na Ndugai marehemu mwenyezi Mungu aiweke roho yake inapostahili.
Pia 2017 nilikuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika na sikumalizia nafasi hiyo kwasababu nilizosema.
Professionally nilipata heshima kuwa Rais wao kwahiyo tunapozungumza kuhusu treason tunauzngunza kuhsu mtu wa aina hiyo.
Mimi nimekuwa mwanaharakati katika maisha yangu yote.
Mwaka 2016 nilipata tuzo ya chuo kikuu huko Marekani (BrichPort University) Maelezo ya tuzo hiyo inasema TUNDU LISSU ni mtetezi wa haki za binadamu na mazingira Tanzania na Afrika. Nilipewa hiyo tuzo.
Ni muhimu kusema mambo haya ilitumjue Tundu Lissu ni nani na yanamaanisha nini?
Yanamaanisha kwamba huyu mtu anbae amechaguliwa na wananchi,
Amepata heshima ya kuwatumikia wanataaluma wenzake,
Heshima ya kutambulika na taasisi za kimataifa.
Haya yote yanasema ukweli mmoja kuwa, MIMI NI MPIGANIA HAKI, DEMOKRASIA NI MTETEZI WA HAKI ndo maana nimetambuliwa hivi.
Mimi sio MHAINI,
Mimi sio mhalifu na sio yote hayo uliyoyasikia hapa.
My contribution recognised nationally na internationally.
Hii kesi ya uhaini ni kesi kweli au ni siasa tu?
Mambo hayo niliyosema yanakusaidia kujibu swali hilo hapo juu.
Lingine uelewe kwangu mimi ni mwendelezo wa mashitaka ambayo nimefunguliwa kwa zaidi ya miaka 23 nimefunguliwa mashitaka kwahiyo huu ni mwendelezo tu.
Kesi yangu ya kwanza katika Mahakama hii katika chumba hiki siku ya Christmas mwaka 2002 mbele ya hakimu Lugulu kwenye chumba hiki hiki kosa lilikuwa uchochezi.
Tulimkosoa Rais Mkapa kutokana na wachimbaji wa wadogowadogo 1996 nikapewa kesi ya Uchochezi nilikaa nayo kwa miaka 6 baada ya miaka 6 kesi hiyo ilifutwa bila maelezo.
Baada ya hapo miaka 10 ya kikwete nilishtakiwa mara tatu, mara moja Tarime, nilikoenda kupinga mauaji nikashitakiwa huko kesi ya criminal trespasses,
2012 nikafunguliwa kesi mbili Arusha mjini, kesi ya kwanza kupinga mauaji ya waandamanaji 2011 tukaenda kupinga nikafunguliwa kesi.
Kesi ya pili Arusha nilienda kupinga mkutano wa Chadema kupinga wanachadema kuuliwa arusha ikafutwa pia na kesi hiyo.
Tulivyoingia Tanzania ya Magufuli kwenye mwaka mmoja wa Magufuli 2016 hadi 2017 kwenye mahakama hii na kwenye chumba hiki nilishatakiwa kwa kesi sita nilikuwa nikipinga mambo ya Magufuli.
Nilipochaguliwa RAIS wa TLS nilitokea hapa Kisutu na kwenda kushinda uchaguzi wa TLS nilikamatwa na mapolisi mara nane.
Kesi zote hizo pia zilifutwa hizo kesi zilifutwa na hakuna aliyekuja kutoa ushahidi hata mmoja.
Ikaja ile habari ya risasi walitaka kuninyamazisha forever.
Tangu mwaka jana hadi leo nimeshakamatwa na Polisi mara 3 nilikamatwa Mbeya, August mwaka jana, mara ya pili 13/09 nikakamatwa pia kulikuwa na mauaji ya Mzee Kibao walikuja nyumbani kunikamata.
Anasimama Katuga anasema haya maelezo ya Lissu hayana umuhimu wowote, asiyaseme na ni kinyume na Sheria.
LISSU Anasema yeye sheria yuko nayo na anasoma Sheria.
Lissu anasema anachokisema wakili wa serikali ni non sense huwa sipendi kusema maneno haya lakini anapaswa kurudi shule huyu asome kifungu cha 53 cha sheria ya ushahidi kwaba good character is relevant to the case.
Hakimu anasema maelezo yote ajielekeze kwenye charge sheet
Lissu anasema mheshimiwa kazi yako wewe ni kuandika na mimi kazi yangu nitasema kama hutaki kuandika usiandike ila mimi nitasema. π€£π€£π€£π€£
Wapendwa Leo mambo yangekuwa live vingekuwa ni vituko sana vinaendelea hapa ndan Hakimu kapanic, Mawakili wa Serikali wamepanic, Mhe. Lissu anawashona bila ganzi πππππ
Part 11, itaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 9
Anaendele Mhe. Lissu
Kifungu cha 263(3)(5) kinanipa haki ya kusema na nitakayosema yote uyaandike na uyasome kwangu ni muhimu kwasababu kwa kesi kama hii kubwa kuliko zote Tanzania.
Ambayo adhabu yake ni adhabu ya kifo kwa kesi ya aina hii,
Anasimama Katuga hapa anasema Mhehsimiwa kifungu namna anavyokitafsiri ni tofauti na maana yake. Hapaswi kusema kila kitu, yeye aseme ni kweli au sio kweli?
Tundu Lissu anasema huyu Wakili wa serikali tumemvumilia sana kasema yakwake. Sasa muda huu anisubiri na mimi niseme yakwangu. Anivumilie na awe mtulivu kabisa.
Hakimu anasema ntuhumiwa unapaswa kwenda direct. Lissu anasema hapana siwezi kwenda huko
Kwanza naomba niendelee na nipewe muda.
Jambo la kwanza nataka kusema kuhusu mimi. Masuala ya character ni muhimu sana kwasababu ni maswala relevant to the charge.
Jina langu ni TUNDU ANTIPHAS MUGH'AI LISSU. nimezaliwa Mahambe Ikungi Singida 20/01/1968. Nina miaka 57 ni mtoto wa Saba kati ya watoto 10.
Nilipata elimu ya msingi Mahambe.
Amesimama Katuga anasema mheshimiwa asiende kwa style hiyo asiseme mambo ya amesoma wapi?
Mheshimiwa anasema Lissu asome hati ya mashitaka
Amesoma yote.
Lissu anasema Mhehsimiwa Hakimu unapswa kulinda haki yangu ya kusema. Inakuwaje hawa wameongea yote kuanzia asubuhi hadi sasa hivi wamekaa siku zaidi ya 100 wanaandaaa haya makaratasi. Na wewe ulinde hiyo haki yangu sitakubali kabisa kwenye jambo hilo.
Nimesoma Ilboru, Galanos, nilienda kwa mujibu wa sheria JKT 1989/1990. Baaada ya JKT nilitakiwa kwenda kusoma chuo kikuu 1990 kutokana na mgomo wa wanafunzi kwahiyo nilifanya kazi shule ya sekondari Bondeni arusha.
1991 nilisoma kitivo cha sheria shahada ya kwanza pale UDSM.
Nilimaliza UDSM na kumaliza November 1994 na kuzawadiwa shahada ya sheria ya heshima. Honours degree. Mimi ndie niliyekuwa mwanafunzi bora wa sheria wa mwaka wa 3 pale UDSM.
Nilipograduate nilipata scholarship kwenda kusoma nje kutoka Serikali ya Wingereza, Mwaka 1995 hadi 1996 nilipata distinction na ndoto zangu nilikuwa nataka kurudi UDSM kufundisha sheria ilikuwa ni ndoto yangu siku zote.
Nilipata kazi LEAT ya Dar es salaam mwaka 1998 kama mtafiti wa masuala ya mazingira na haki za binadamu hadi mwaka 1999.
Nilipata kazi world resources institute (Taasisi ya Rasilimali za Dunia)
Nilifanya kazi WRI kwa miaka 3 na 2002 nilirudi Tanzania.
June 2003 nilipata uwakili wa mahakama kuu za Tanzania na chini yake. Nimekuwa Wakili wa nchi hii namba yangu ni 945.
Ni muhimu kuelewa maisha yangu ya ajira kwasababu yana uhusiano na kesi hii maana nimesikia wanasema kuhusu siasa zangu.
Katika maisha yangu yote nimekuwa mwanaharakati wa kisiasa. Na mwanahatakat wa haki za binadamu. Kwenye siasa mimi nilipiga kura kwa mara ya kwanza 1985 nikiwa kidato cha 5.
Kabla sijaenda chuo kikuu nilienda jeshini na majeshi yalikuwa ya CCM. Na mimi nikiwa jeshini nilikataa utaratibu wa majeshi kuwa ni mali ya CCM.
HAKIMU anauliza hiyo ni relevant Lissu anamjibu kuwa hiyo ni Character na ni muhimu sana urekodi.
Nayasema haya ili ujue mimi ni mtu gani yuko mbele yako. Nilianza harakati zangu jeshini sio tu huku mtaani.
Mwaka 1995 nikiwa mwanafunzi wingereza nilirudi nyumbani kuja kugombea ubunge singida kusini miaka ile. Nilikuwa mgombea ubunge kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi na baadae nilirudi shule.
Naomba kusema kuhusu Chadema, nilijunga Chadema 2004 July na nilipojiunga niliteuliwa kuwa mkurugenzi wa sheria na haki za binadamu. Na kwasababu nilikuwa wakili uchaguzi wa 2005 nilikuwa wakili wa wagombea wote wa Chadema walioshitakiwa kwenye uchaguzi.
Kwahiyo kwenye haya masuala ya Uchaguzi nina historia ndefu sana.
2010 nilichaguliwa kuwa mbunge kwa tiketi ya Chadema. Na nilikuwa mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.
Part 10, itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako.