For Boys Only – Wale Fighters Wenzangu Tu, if you are faint-hearted ujumbe huu haukuhusu, beat it! 😆🤛🏾
1. Dream big. Believe. Think . Plan. Chukua hatua. Become. Usijizuie kufikiria makubwa. Kama unaweza kuota, unaweza kutimiza. Dunia ni ya wale wanaothubutu. #TeamBelieve
2. Marafiki wa kweli ni kama nyota – utawagundua unapozungukwa na giza. Si kila anayekusifia ni wa kweli, na si kila anayekukosoa ni adui. Jifunze kutofautisha.
3. Tengeneza thamani kwa wengine, utajikuta umepata thamani kwenye maisha yako. Ukianzisha biashara ama jambo lolote, faidisha wengi. Kubali kushirikisha wengine , hata kama unachobaki nacho ni kidogo — kama ni sehemu ya jambo kubwa, utakula kikubwa.
4. Kuna watu watahangaika kupunguza bei kwa mkulima maskini, lakini wakifika kwenye malls, bar na ama kwenye migahawa ya kifahari wanaacha na chenji kabisa. Fighter, lipa zaidi ya bei atakayokupa mkulima au mfanyabiashara mdogo. Saidia wanyonge kimya kimya, siyo lazima dunia ijue. Hii ndiyo sadaka/charity yenye utu ndani yake.
5. Ikitokea una mamlaka ama maguvu ya kumzabua mtu, jizuie kumnyima haki yake ya kulia.
6. Usionyeshe uoga mbele ya watu. Unapoongea na wakubwa kazini, usizidishe uchawa – unapojipendekeza kupitiliza, unajishusha hadhi. Unapoongea na wadogo zako kazini, usionyeshe ujuaji – badala yake, onyesha tabia njema na mtazamo chanya.
7. Ukiyapanga matofali moja juu ya jingine, unajenga ukuta. Kila hatua ndogo unayochukua leo ni msingi wa kesho yako. Usidharau mwanzo mdogo.
8. Usijifananishe na mtu mwingine. Kuwa wewe na neema zako. Kila mtu ana safari yake, changamoto zake, na baraka zake. Hujui mtu mwingine kapitia nini kufika alipo, wala anapokwenda.
9. Jifunze kuvua samaki, usiombe kupewa samaki. Ukipewa msaada leo, kesho utahitaji tena. Ukipewa maarifa, utaendelea kuyatumia milele. Kama umebarikiwa zaidi ya wengine, usiwadharau – wafundishe nao wajitegemee.
10. Piga push-ups nyingi kila siku. Piga squats na sit-ups. Uwe na strong and heavy handshake. Usimpe mtu mkono ukiwa umekaa. Simama. Kula nyama nyingi, mboga, na matunda. Lala vya kutosha ili akili yako iwe fresh, uwe mbunifu, makini na timamu. Cheka zaidi. Tabasamu. Penda sana, vumilia maumivu ya moyo. It’s okay. Soma vitabu, punguza screen time. Jifunze kitu kipya kila siku. Cheza michezo, tembea misituni, ipende nature. Fahamu historia yako. Jua utamaduni na asili ya kwenu. Wakumbuke waliotangulia mbele ya haki. Chukua muda wa kukaa kimya bila simu, bila story na mtu. Sali sana. Omba dua.
11. Kata marafiki wabaya. Kata tabia mbaya. Kata uzembe, ulevi, uvivu, uraibu, na upuuzi. Kata mwanamke anayekuzingua – maisha ni mafupi, usiyapoteze kwa drama.
#HK #Fighter #NjeYaBox
Leo nataka kuzungumza na boys; wadogo zangu wapiganaji kabisa:
1.) Maisha siyo rahisi sana. Mafanikio siyo rahisi kabisa. Yatakujaribu. Yatakukatisha tamaa. Usikubali. Komaa, pambana! Kukata tamaa ni dhambi. Kurudi nyuma ni mkakati kabisa vitani. Wewe siyo mwepesi kiasi hiiicho!
2.) Wewe ulikuwa mgumu sana ndiyo maana Mungu aliamua uwe wa kiume mwanangu. Komaa kiume dogo.
3.) Kumbuka kuwa una dhamana kwa familia yako, dhamana hii ni kubwa zaidi kama hautoki kwenye familia tajiri, maana familia tajiri inatakiwa kutokana na wewe.
4.) Mtu aliyefanikiwa leo, ujue alianguka mara nyingi sana jana na juzi.
5.) Kufanya biashara ni kitu kigumu sana lakini pia kuwa kuajiriwa mpaka umri wa miaka 60 kila siku kuamka kuwahi kazini ni kazi ngumu pia. Chagua chako kimoja.
6.) Kama mkeo hakutii hasira, basi huyo siyo mkeo. Pole sana kaka.
7.) Kuwa na vyanzo vya pesa ni kitu kizuri zaidi kuliko kuwa na chanzo kimoja. Mkeo akiwa na kazi ama biashara ni nafuu kwako ila usimuulize anatumiaje pesa zake, timu za wajibu wako wa kumhudumia, usipigie hesabu pesa yake.
8.) Pesa haitafutwi kwa kulalamika, inatafutwa kwa ubunifu na juhudi. Ukiwa unalalamika sana badala ya kutafuta suluhisho, utaishia kuangalia wenzako wakifanikiwa. Simama, tafuta njia, usikubali kushindwa.
9.) Heshimu muda wako na muda wa wengine. Usipoteze muda kwa starehe zisizo na tija, badala yake utumie muda wako kujifunza, kufanya kazi, na kujenga mustakabali wako.
10.) Marafiki zako ni taswira ya maisha yako ya baadaye. Ukiwa na marafiki wavivu, wasio na maono, na wanaopenda majungu, basi ujue upo kwenye njia mbaya. Tafuta marafiki wanaokutia moyo, wanaokufundisha, na wanaokuinua.
11.) Jifunze kusema ‘hapana’. Usikubali kila jambo, kila ombi, na kila fursa kama haina maslahi kwako. Usihadaike na ‘muda wote uko available’. Jua thamani yako.
12.) Afya ni utajiri. Unaweza kuwa na pesa nyingi lakini bila afya njema, utajiri wako hauna maana. Fanya mazoezi, kula vizuri, na epuka anasa zinazoathiri afya yako.
13.) Siku zote jifunze kitu kipya. Usiwahi kufikiri unajua kila kitu. Dunia inabadilika, biashara zinabadilika, fursa zinabadilika. Mwanaume anayejifunza kila siku ndiye anayeendelea kushinda.
14.) Usiishi kwa kushindana na watu, ishi kwa kushindana na jana yako. Kama leo unafanya vizuri zaidi ya jana, basi unashinda. Weka malengo yako binafsi, usipoteze muda kujilinganisha na wengine.
15.) Jifunze kuvumilia na kustahimili maumivu ya mafanikio. Hakuna aliyefanikiwa bila kupitia mateso, misukosuko, na changamoto. Ukikataa tabu za kujenga, utapitia tabu za maisha kwa kukosa. Chagua tabu zako!
#HK #Fighter #NjeYaBox
"We now live in a World where doctors destroy health, lawyers destory justice,
universities destroy knowledge, the press destroys information. religion destroys morals, and banks destray the economy."
Chris Hedges