Kutafakari na kuhoji ni dalili Za uhai. Maiti haiwezi kutafakari wala kuhoji! Twaweza kuamua kuishi kama maiti au viumbe hai wenye uwezo wa kuutiisha ulimwengu na kujiletea maendeleo! Maendeleo uletwa na watu hai, si maiti!
Sioni tatizo la nguo ya Mbunge,aliyetolewa nje ya Bunge. 1987,nilimtembelea rafiki yangu Mmasai, Loliondo, tulilala na wasichana kitanda kimoja bila kufanya chochote! Rafiki yangu aliniambia matatizo yako vichwani mwetu..kichwani mwa spika!
@AMkioma Ndiyo nilikuwa padri na nilimtemmelea padri wa kimassai rafiki yangu. Ni ngumu kuelewa maana vichwa vyetu vina matatizo,lakini ukienda umasaini, utaelewa!
@EChelialis Nenda kwa wamassai,hadi Leo, kuwatenga wasichana na wavulana ni matatizo vichwani mwetu, wao hawana shida mvulana na msichana kulala kitanda kimoja bila kitendo. Nilishuhudia 1987, nilikuwa na miaka 31!
Nilifikiri kwa vile kituo kipya cha mabas Mbezi, ni cha kisasa, basi na mambo yote ya huduma yatakuwa ni ya kisasa, wapi! Wapiga debe, vurugu,mpangilio, UCHAFU kama kawa! Watanzania tuna matatizo gani? Hata ujenzi bado kukamilika!
@MsigwaPeter Msigwa, nimeiona video hiyo, imechukuliwa kanisani! Tatizo kanisa tunazoziona si zile za Yesu wa Nazareti! Ni zile za Consatino, falsafa za Kigiriki na tamaduni za wazungu. Ile ya pigwa kulia,geuza kushoto, to a uhai wako, umepewa Bure toa Bure, hakuna!
The Holy Trinity not complicated as The The Holy Father Pope Francis, tweeted. Father, Son and The Holy Spirit,three persons in one! Body, different parts in one! Community, different persons in one! Life is unity! It is simple,yet difficult to see!
Mkoa mpya Rubondo, hitaji la wananchi wa Chato? Muhimu kwa sasa?Chato ulikuwa Kagera,ikamegwa kwenda Geita, sasa inakwenda Rubondo! Wanachi wanataka hivyo au mapenzi ya mtu mmoja? Katiba mpya, katiba ya wananchi ni lazima ili kuondoa utata kama huu!
Somo kutoka DAWASCO, ni kwamba kama maji hayatoki, ufunge mabomba yote, ukiyaacha wazi, hewa ya kwenye bomba ikipita kwenye miter inasoma! Na hii inakwenda kasi sana na kupandisha unit, hivyo funga bomba kama maji hayatoki!
Ninawashukuru DAWASCO, kwa tweet yangu ya kulalamikia unit za maji, wamekuja kwangu, wanarekebisha baadhi ya vitu, ili tuone kama unit zitapungua! Kumbe mitandao ya kijamii ina nguvu?
@zittokabwe@Yed360 Zitto,soma vizuri kitabu hicho. Kiliandikwa kwa mapenzi makubwa chini ya vitisho vikubwa. Lakini mapenzi, uzalendo wa taifa letu vilifunika vitisho hivyo. Hongera sana Attilio!
@deusishe Ninafikiri mengi hatuyafahamu! Vita ya uchumi ni mbaya sana. Sisi Tupo tu bendera fuata upepo. Soma vizuri historia ya Afrika. Vika DRC. Mifano ni mingi.
COVID 19, huko nyuma sikuogopa, pia sikukubaliana na JPM, sasa ninaogopa sana! COVID 19 ni fumbo kubwa! Msimamo wa sasa umekuwa wa haraka bila utafiti wa kutosha! Chanjo inatisha kuliko COVID 19. Tuwe makini!
DAWASCO, si wakweli! Nimelalamika mara nyingi kwao. Meter zao zinasoma hewa! Lita elfu moja ni maji mengi! Kutumia Lita elfu 30, kwa mwezi, matumizi ya kawaida ya familia haiwezekani! Tunaibiwa! Hili lichunguzwe!