Tunamshukuru Mungu tumeweza tumekutana na mabalozi wote 490 wa Jimbo la Kasulu Mjini, tumegawa bendera 550 za @ccm_tanzania na kuzungumza nao kwenye semina maalum. Nawashukuru sana wananchi wa Kasulu Mjini kwa upendo wao.
Umoja ni nguvu. Kazi inaendelea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa. Mheshimiwa Lowassa ameitumikia nchi yetu katika nafasi mbalimbali kwa zaidi ya miaka 35, akianzia ushiriki wake katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge, Waziri katika wizara mbalimbali na Waziri Mkuu.
Tumempoteza kiongozi mahiri, aliyejituma na kujitoa kwa nchi yetu. Natoa pole kwa mjane, Mama Regina Lowassa, watoto (Mheshimiwa Mbunge wa Monduli, Fredrick Lowassa na wadogo zako), ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mzito.
Katika mawasiliano yangu na familia, nimewaeleza kuwa kama taifa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu, na kamwe wasiache kumtegemea Mwenyezi Mungu na kutafakari neno lake, hasa Kitabu cha Ayubu 1:21.
Mwenyezi Mungu amweke mahali pema. Amina.
Nimewahakikishia Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, kuwa serikali inayachukulia kwa uzito mkubwa, maoni na mapendekezo yao kuhusu maboresho ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi, na kuwa yapo mbioni kuja.
Kazi inaendelea.
Nimefungua Kikao Kazi cha Mafunzo ya Uelimishaji kwa Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Kanda ya Kusini na Watendaji wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Songea, Mkoani Ruvuma.
Asubuhi ya leo nimemkaribisha nchini na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Poland, Mheshimiwa Andrzej Duda. Uhusiano kati ya Tanzania na Poland ni wa kihistoria na umedumu kwa zaidi ya miaka 60. Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Poland kufanya ziara ya kitaifa Tanzania, na nimemshukuru kwa kuchagua Tanzania kama nchi mojawapo kufika katika ziara yake barani Afrika.
Poland ni nchi ya 21 kwa ukubwa wa kiuchumi duniani na mshirika wetu muhimu katika Jumuiya ya Umoja wa Ulaya. Tunashirikiana katika maeneo mbalimbali ya kwa manufaa ya wananchi wetu hasa kwenye utalii ambapo Poland ni kati ya nchi 10 zinazoleta watalii wengi zaidi nchini. Kutokana na ukuaji huu wa biashara ya utalii baina yetu, nimemueleza nia yetu ya kuwa na safari za moja kwa moja za ndege kutoka Poland kuja Tanzania. Mbali na utalii, pia tuna ushirikiano mkubwa katika sekta ya afya, wakishiriki nasi miradi kwenye hospitali za Aga Khan, Temeke, Mwananyamala, Kituo cha Afya Chanika na Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana.
Tumekubaliana kuendelea kushirikiana zaidi katika maeneo ya elimu, kilimo, biashara, uwekezaji, utalii na TEHAMA eneo ambalo wenzetu wamepiga hatua kubwa. Kiuchumi, tumeweka nia ya pamoja na kuazimia kuhamasisha uwekezaji zaidi kwenye sekta za kimkakati kama viwanda, uzalishaji, nishati, madini, gesi asilia na uchumi wa bluu. Nimeshukuru pia kwa utayari wa nchi yake kupitia wakala wa mikopo ya usafirishaji kutoa bima kwa benki za biashara katika utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa nchini kwa vipande vya Makutopora - Tabora na Tabora - Isaka.
Kwa ujumla, sote tumeona kwamba kwa umri na historia ya ushirikiano uliopo kati yetu, maswala ya biashara na kuinua uchumi bado ni madogo hivyo basi lazima kuongeza ushirikiano wetu kiuchumi kwa njia za uwazi, haki na kuaminiana.
Mheshimiwa Rais amenipa pia mwaliko wa kutembelea Jamhuri ya Poland, na mimi nimemuahidi kuwa panapo majaliwa, mimi na ujumbe wangu kwa niaba ya nchi yetu tutafanya ziara ya kitaifa nchini humo.
Nikizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Uzalishaji Umeme wa Megawati 49.5 kwa nguvu ya Maji Katika Mto Malagarasi Mkoani Kigoma, hafla iliyofanyika jijini Dodoma.
Kazi inaendelea.
Nimeungana na Makamu wa Rais wa JMT Mhe.@dr_mpango pamoja na viongozi wa Vyama vya Waajiri katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 7 wa Wadau wa Kijamii wa Afrika katika masuala ya Kazi na Ajira.
Kazi inaendelea
Tumejadili Mpango Kazi wa Umoja wa Afrika kuhusu masuala ya Watu wenye Ualbino, Rasimu ya Mpango Kazi wa Watu wenye Ualbino na hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu ujumuishwaji wa Watu wenye Ualbino na ufikiwaji wa huduma ya afya, haki zao na elimu jumuishi.
Kazi inaendelea
Nimekutana na kufanya mazungumzo na Mtaalam wa kujitegemea wa masuala ya haki za Watu wenye Ualbino kutoka Umoja wa Mataifa (UN Independent Expert on the Enjoyment of rights by Persons with Albinism), Bi. Muluka-Anne Miti-Drummond jijini Dodoma.
Kutokea Kasulu Mjini, Wana CCM wenzangu wote Tanzania nawatakia umoja, amani na ushindi wakati wote tunapo sherekea miaka 47 ya kuanzishwa kwa Chama chetu.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.π
Heri ya Miaka 47 toka kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Imekuwa miaka 47 ya mapinduzi makubwa kwa kila Mtanzania kwenye kila kona ya nchi yetu. Tulipo leo, sipo tulipokuwa miaka 47 iliyopita. Tumepiga hatua kubwa za kimapinduzi na za kujivunia zenye matunda mazuri katika uchumi wetu, miundombinu yetu, huduma zetu za afya, maji, kilimo, elimu, nishati, utawala bora, uhuru wa watu, haki na maendeleo kwa ujumla. Katika miaka hii 47 tumeendelea pia kubaki wamoja, wenye amani na mshikamano, tunu ambazo hazijawa rahisi kupatikana, kutunzwa na kudumu katika maeneo mengi ya bara letu.
Maendeleo ni mchakato, ni hatua inayotaka juhudi na weledi wa kila mmoja wetu. Tafakuri na sherehe za miaka 47 ya kuzaliwa kwa chama hiki muhimu kwa historia, umoja, uimara na maendeleo ya nchi yetu ziendelee kutusukuma mbele kuifanya vyema kazi iliyo mbele yetu; kazi ya kuhakikisha tunaipatia majawabu kila changamoto inayomkumba Mtanzania popote pale alipo kwa kiwango cha juu kabisa.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Kazi Iendelee.
wakiwezeshwa vijana hawa kufanya kilimo biashara wataweza kujiajiri, kuajiri wenzao na kuongeza mchango wa sekta ya kilimo katika pato la Taifa.
Kazi inaendelea.
@HusseinBashe
Nimeshiriki kwenye hafla ya mapokezi ya vijana 268 wanufaika wa Mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT), iliyochini ya @WizaraKilimo katika Shamba la pamoja la Chinangali II Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, ambapo serikali imeanzisha programu hii ili kupunguza tatizo la ajira.
Karibu rasmi kazini Baba Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Mwenyezi Mungu aliyekuita, na wewe kuitika kwa kazi hii ya kutumikia watu wake akakusimamie na kukuongoza. (Tafakari: Mithali 3:5-6)
Nakuahidi ushirikiano wangu na Serikali katika utekelezaji wa jukumu hili, ikiwa ni pamoja na kazi ya kuendelea kuimarisha uchumi wetu, demokrasia yetu, utoaji haki, umoja na mshikamano wetu, na kuendelea kutunza amani ya nchi yetu ili wananchi waendelee na shughuli zao mbalimbali za ujenzi wa Taifa lao na ustawi wao, ikiwemo kutekeleza haki yao ya kuabudu.