#HABARI Waziri wa Habari, utamaduni , sanaa na michezo Mheshimiwa Makonda amefika Bara la Ulaya na kukutana na wachezaji wa klabu maarufu duniani ya FC Barcelona, nyota waliowahi kufanya maajabu makubwa katika soka la dunia.
Akihitimisha ziara yake ya kihistoria, Mheshimiwa Makonda alipata nafasi ya kubadilishana mawazo na wachezaji hao, huku akiwaalika mmoja mmoja kuja kutembelea Tanzania na kujionea uzuri, utamaduni na vivutio vya kipekee vya nchi yetu.
Huu ni mwanzo wa ukurasa mpya katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na FC Barcelona. Dunia sasa inaelekeza macho yake Tanzania na makubwa zaidi yanakuja!
#EastAfricaRadio #TogetherTunawakilisha