Kabla Mungu hajakupa kile unachostahili, mara nyingi huondoa faraja yako kwanza. Anaijaribu subira yako, anakutenga na anaisafisha mioyo na mikono yako. Hiyo sio adhabu; anakujenga. Kabla ya baraka kukufikia, wewe ambaye unaweza kuzibeba baraka hizo ni lazima ujengwe.
MWANANGU nisikilize kwasasa Wanawake watakuacha saaana tu, Mabinti hawatodumu kwenye maisha yako ila lisikupe shida, kanuni ya maisha ni kuwa Paka hakai na Msela, mara atakwambia haupo romantic yani hujui kubembeleza, utawezaje Mwanangu wakati kichwa kinawaka moto na maisha yanataka kupetiwa ili vitu viende.
Kuna wakati atakwambia hakuna Mwanaume busy kwa Mwanamke anayempenda lakini anasahau maisha ya Msela akishika simu sometimes kuna mchongo anaosikilizia anauchungulia kama umetiki, kuna wakati anawasha data sio kuchat bali kuona kama Email imejibiwa ama kuna tangazo la ajira.
MWANANGU kwasasa utaitwa kila jina, tushawahi shuhudia Diamond akiitwa Domo na sasa Mabinti wanasema ana lips denda, tushawahi shuhudia Wanetu wanaambiwa โWewe sio type yanguโ ila wapo busy kulamba vitambi vya Wakongwe na kujibebisha eti Dady, atasema sidate na Watoto ila analala na Mwanaume umri wa Babu yake.
WANANGU kama tunazitaka mali tutazipata kwenye hustle, kama tunaumizwa na hawa Mabinti na Wanawake aminini Wanangu tutawakuta wengine mbele, tuwe BIZE SAAANA kwakuwa wao ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu, tunao Ndugu na Wazazi wetu wanaotaka ushindi wetu.
WANANGU tujibu texts zao pale ambapo muda umepatikana, tupokee simu pale ambapo hakuna mishe nyingine, tuwe busy tupambanie maisha, wao ajira zao zipo ndani ya nguo zao wengi wao, sisi ajira zetu zipo ndani ya jasho letu, mpaka mwisho Wanangu, wakisema sio romantic fresh, wakisema hatujali fresh sisi hatuna muda mwingi wa kujiteteta tunasaka USHINDI.
MKULIMA WA BONDE LA MTO KILOMBERO.
Kijana mwenzangu;
1. Sikiliza kama Mshauri
2. Soma kama Mwanafunzi
3. Zungumza kama kiongozi
4. Fikiria kama Mwanafalsafa
5. Tembea kama Mwanamazoezi
6. Saidia wahitaji kama mtakatifu
Wakikuambia wanakupenda
Wanakuamini wanasimama na wewe na wanakushangilia waulize watakuwepo upande wako kwa muda gani kwa maana unaweza Kua muhim sana kwa watu lakini sio kilasiku utakua muhimu ikitokea mtu wamemuona mzuri kuliko ww watakuacha wataenda kwa uyo mwingine jitambue ishi acha kujipa umuhimu kwenye MAISHA ya watu nimeandika HII BAADA ya kuona kwa wanasiasa Wa chadema na maisha halisi ya kilaisku tumekua muhimu kwa watu ila sio kilasiku
Watu wanaposema uongo kuhusu wewe maana yake nini?
Maana yake hicho ndicho walichotamani ungefanya, ungesema au kingekutokea. Watu waongo ni wabaya kuliko maadui wa wazi, maadui wana confidence ya kukuambia hisia zao hawakupendi ila waongo ni hatarii. Muongo ni adui anayekulia timing.