Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Mbeya kwenda maeneo mbalimbali nchini wamejikuta katika wakati mgumu baada ya mabasi ya masafa marefu kusitisha safari kutokana na mgomo wa madereva ulioanza leo Jumanne, Septemba 29, 2026.
Mgomo huo ulianza saa 11:00 alfajiri, muda ambao mabasi ya mikoani yalipaswa kuanza safari, lakini hadi saa 5:00 asubuhi, zaidi ya saa sita baadaye, bado hayakuwa yameondoka.
Hali hiyo imeathiri wasafiri waliokuwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi, huku baadhi wakieleza hofu ya kuchelewa kufika wanakoelekea na kuiomba Serikali kuingilia kati ili kutatua mgogoro huo.
#KemgongoUPDATES