Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameeleza lengo kuu la kuunda Tume ya Taifa ya Mipango pamoja na umuhimu wake katika maendeleo ya nchi.
Habari kwa Picha πΈ
Tume ya Taifa ya Mipango imefanya kikao maalum leo, tarehe 18 Juni 2025, jijini Dodoma chini ya Makamu Mwenyekiti Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.).
Kikao kimejadili rasimu ya Dira 2050 na Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu (LTPP).
ποΈ Habari katika Picha πΉπΏ
Juni 4, 2025 β Dkt. Fred Msemwa (Tume ya Mipango) amekutana na Ndugu Said Salim Bakhresa kujadili maendeleo ya sekta binafsi na ujasiriamali nchini.
#SektaBinafsi#UjasiriamaliTanzania#MaendeleoEndelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Blandina Buganzi Kilama kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshughulikia biashara na ubunifu kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 24 Mei, 2025.
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Mipango wameungana na wengine kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani kwa kushiriki maandamano kitaifa mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Singida, Mei 1, 2025.
Dkt. Fred Msemwa, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, ashiriki mazungumzo kuhusu ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Benki ya Dunia, pembeni ya Mikutano ya Kipupwe ya IMF & WB, Washington D.C. Mazungumzo yajikita kwenye IDA 21 na miradi ya maendeleo.
βMhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanzidha Tume ya Taifa ya Mipango ili kuimarisha Uchumi na Mipango ya Maendeleoβ
@kitilam
Waziri wa Fedha Dkt. @mwigulunchemba na ujumbe kutoka Tanzania wamekutana na Benki ya Dunia leo Aprili 22, 2025 Washington DC kujadili ufadhili wa miradi ya maendeleo.
Ameambatana na @StanslausNyongo, Dkt. Fred Msemwa (Tume ya Mipango), Bw. Tutuba (BoT), Dkt. Mwamba (Hazina).
Serikali yaweka matarajio makubwa kwa Tume ya Taifa ya Mipango kusimamia maendeleo ya kiuchumi kulingana na mahitaji ya wananchi na jiografia ya nchi. Spika Dkt. Tulia amesema hayo baada ya kukutana na Dkt. Fred Msemwa leo Aprili 16, 2025 Bungeni, Dodoma. @TuliaAckson@fredmsemwa
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa amekutana na Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Yusuph Mwenda kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kodi na mipango ya maendeleo. Mazungumzo haya yamefanyika leo 14 Aprili 2025, Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa, amewafuturisha watumishi wa Tume na kuwatakia heri ya Mfungo wa Ramadhanina sikukuu njema ya Idd. Hafla hiyo, ilimefanyika 27 Desemba 2025 jijini Dodoma, ililenga kudumisha mshikamano na mahusiano mazuri ya watumishi
Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Mipango limefanya kikao cha pili leo, Machi 20, 2025, Jijini Dodoma, Kikao hicho kimeongozwa na Dkt. Fred Msemwa Katibu Mtendaji wa Tume, Kikao Kilipokea na kujadili utekelezaji wa Bajeti ya 2024/25 na mapendekezo ya Bajeti ya 2025/26.
Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ikifuatilia kwa makini uwasilishwaji Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025/26 ulio fanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof Kitila Mkumbo (Mb.) leo tarehe 11 Machi, 2025 Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, leo amekutana na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari katika Ukumbi wa Mikutano wa JNICC, kwa ajili ya kujadili na kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Mkutano huo, uliofanyika tarehe 16 Desemba 2050.