Heri ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani.
Tunawakumbusha kujali Afya zenu za Akili muwapo kazini.
Kama mnavyojali afya za mwili
AFYA YA AKILI NI AFYA
#AfyaYaAkiliMahalapaKazi#AfyaYaAkiliniAfya
KAMPENI YA AFYA YA AKILI NI AFYA YAZINDULIWA RASMI
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Bi. Ziada Sellah amezindua rasmi Kampeni ya kitaifa ya Afya ya Akili ni Afya, yenye lengo la kuongeza uelewa juu ya afya ya akili nchini ili kuhakikisha kila mwananchi ana ustawi wa akili.
KAMPENI YA KITAIFA YA AFYA YA AKILI NI AFYA KUTIMUA VUMBI MKOANI IRINGA
Kampeni ya kitaifa ya Afya ya Akili ni Afya imeaanza rasmi Chuo Kikuu cha Iringa ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa MNMH @Plawala2023 na wataalamu mbalimbali kutoka @Mirembe_hosptz wameweka kambi Iringa
MIREMBE YAZINDUA KAMPENI KITAIFA“ AFYA YA AKILI NI AFYA”
Na WAF, Dodoma
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Bi. Ziada Sellah amezindua rasmi Kampeni ya kitaifa ya Afya ya Akili ni Afya, yenye lengo la kuongeza uelewa juu ya afya ya akili nchini ili kuhakikisha kila mwananchi ana ustawi wa akili.
Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 7, 2025 jijini Dodoma Katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe ambapo kampeni ya kitaifa ya "AFYA YA AKILI NI AFYA", ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Uhamasishaji jamii juu ya uelewa wa Afya ya Akili (Mental Health Awareness Month) unaoadhimishwa mwezi Mei kila mwaka.
Bi. Ziada amesema Kampeni hii inalenga kuhamasisha jamii nzima kuhusu umuhimu wa afya ya akili kama sehemu muhimu ya afya ya binadamu kwa ujumla.
“Kauli mbiu hii ina ujumbe mzito: “Afya ya akili ni afya”, hivyo hatuwezi kuwa na jamii yenye nguvu bila kuhakikisha kila mmoja ana ustawi wa akili, ”ameaema Bi. Ziada.
Amesema kuwa Afya ya akili ni kichocheo muhimu cha maendeleo ya jamii na uchumi ambapo amesema bila afya ya akili iliyo imara, hakuna ufanisi kazini, hakuna furaha katika familia na hakuna mshikamano katika jamii.
Ameeleza kupitia kampeni hiyo, wanataka kuondoa unyanyapaa, kuhamasisha mazungumzo ya wazi kuhusu changamoto za afya ya akili na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora bila hofu wala unyanyapaa.
Tunaelewa kuwa changamoto za afya ya akili zinatokana na sababu mbalimbali za kibaiolojia, kisaikolojia, kijamii na kiuchumi, kwa mfano, umasikini, ukosefu wa ajira, magonjwa sugu, na majanga kama COVID-19 yameongeza kwa kiasi kikubwa mzigo wa changamoto za afya ya akili katika jamii yetu.
Ameongeza kuwa takwimu zinaonesha kuwa magonjwa kama sonona (depression), wasiwasi (anxiety) na utegemezi wa dawa za kulevya yanazidi kuongezeka, huku Shirika la Afya Duniani likikadiria kuwa mtu mmoja (1) kati ya wanne (4) duniani anakumbwa na tatizo la afya ya akili katika maisha yake.
Kupitia kampeni ya "AFYA YA AKILI NI AFYA", tunalenga kufikia malengo makuu manne ambayo ni Kuelimisha jamii kuhusu afya ya akili, dalili zake, na namna ya kupata msaada, Kupunguza unyanyapaa, Kuwezesha huduma bora za afya ya akili na Kushirikisha wadau wote
mesema Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuchukua hatua mahususi kuhakikisha huduma za afya ya akili zinaboreshwa.
"Tumeimarisha utoaji wa huduma katika hospitali za rufaa za mikoa na wilaya, na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya ili kuwawezesha kutambua na kushughulikia masuala ya afya ya akili kwa ufanisi, "amefafanua na kuongeza kuwa
tunapambana pia na changamoto za kifedha na unyanyapaa unaozuia watu wengi kufika vituoni kupata msaada.
Vile vile amesema pamoja na afua nyingine, kampeni hii ni jukwaa la kuunganisha nguvu. Tunatoa wito kwa waajiri, walimu, wazazi, walezi, viongozi wa dini, na vijana kote nchini kushiriki kikamilifu.
Amesema kuwa kila mmoja ana nafasi ya kuwa sehemu ya suluhisho iwe ni kwa kutoa msaada kwa rafiki mwenye changamoto, kusikiliza bila kuhukumu au kwa kushiriki katika shughuli za uelimishaji jamii.
“Aidha tukumbuke Afya ya akili ni afya na hivyo hatuwezi kuwa na maendeleo ya kweli bila kuwekeza kwenye ustawi wa akili wa watu wetu. Hii ni kampeni ya kila mmoja wetu. Tuanze mwezi huu wa Mei kwa mabadiliko – mabadiliko ya fikra, vitendo, na sera,” amesisitiza Bi. Ziada.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Dkt. Paul Lawala amesema kampeni hiyo itafanyika kwa muda wa mwezi mmoja na ni jambo ambalo litakuwa endelevu kwa muda wa miaka mitatu.
Mkurugenzi Mtendaji wa MNMH, Dkt. Paul Lawala, amevitaka vyuo vikuu kuwa mabalozi wa afya ya akili, akizungumza UoI & RuCU wakati wa kampeni ya Afya ya Akili ni Afya Mkoani Iringa.
🎖️ UoI yatunukiwa tuzo ya mchango wa kitaaluma!
#AfyaYaAkiliNiAfya#MentalHealthAwarenessMonth
Tunajiunga na ulimwengu kuadhimisha Siku ya Uelewa Kuhusu Usonji Duniani. Usonji si ugonjwa, bali ni hali inayohusiana na tofauti katika ukuaji wa ubongo, inayoathiri namna mtu anavyoingiliana na dunia inayomzunguka
Elewa. Kubali. Saidia.
#AfyaYaAkiliNiAfya#AutismAwarenessDay
Tunarudi Very Strong kama Taifa! 🇹🇿
Kwa furaha kubwa tunatangaza tena kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Mshauri wa Masuala ya Afya kwa Rais wa Tanzania, Profesa Muhammed Janabi, AMEPITISHWA RASMI kuwania tena nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kwa Ukanda wa Afrika (WHO Afro)!
Taarifa hii imetangazwa rasmi katika ukurasa wa Shirika la Afya Duniani (WHO):
🔗 Orodha Rasmi ya Wagombea
https://t.co/MMYcuh4huG
Tanzania As One! 🇹🇿🔥
Taasisi ya GH Foundation inasherehekea mafanikio ya wanawake na wasichana duniani kote. Tumejizatiti kupambana na ukatili wa kijinsia na magonjwa yasiyoambukiza ili kukuza jamii yenye usawa na usalama. Heri ya Siku ya Wanawake Duniani.!
Katika kambi hii wataalamu Bingwa kutoka @Mirembe_hosptz imefanikiwa kuwafikia watu zaidi ya 300 ambapo wamepatiwa elimu ya afya ya akili pamoja na matibabu ya kibingwa kwa waliogundulika na changamoto au ugonjwa wa akili.
#AfyaYaAkiliNiAfya#HakunaAfyabilaAfyayaAkili