VIDEO:
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, ameshusha dongo lingine zito kuhusu mporomoko wa demokrasia nchini, akisema kuwa kwa sasa nguvu na thamani ya kura ya mwananchi wa kawaida imeuawa mchana kweupe, kwani maafisa wa usalama wa wilaya wana uwezo wa kupindua maamuzi ya sanduku la kura.
Akizungumza katika mwendelezo wa mahojiano yake kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM leo Alhamisi, Mei 28, 2026, Zitto amefichua kuwa nchi ipo kwenye mkwamo mkubwa wa kikatiba ambapo sheria zinasema jambo moja lakini mamlaka zinasimamia matakwa yao binafsi, akitolea mfano kizungumkuti kilichopo juu ya kile kinachotajwa kuwa ugawaji usio wa kikatiba wa viti vya wawakilishi wa wanawake (Viti Maalum) bungeni.
Actually, CCM is a THREAT to national security. Wametekwa na vyombo vya ulinzi na usalama, hawawezi tena kufanya siasa inabidi watumie vyombo vya dola. Kura zinapigwa na tume ya Uchaguzi. Imani ya wananchi imeondoka na matokeo yake ni mauaji makubwa kupata kutokea nchini.
Chande: watu 1740s ( waliothibitishwa kufa, waliopotea, wasiojulikana hatma zao) HAWAPO
Yaani sawa na MV Bukoba 3 zizame na abiria wote!
CCM ni TISHIO la usalama wa Taifa letu
Janeth Rithe M/kiti wa @NgomeyaWanawake:
"Nyie Kigoma kila familia inaandaliwa sanda ili izikwe. Mimi ningedhani ukiwa kiongozi wa watu ungeenda kutafuta mashine za kufanya dialysis watu watibiwe waweze kuishi. Lakini unawaletea sanda wafe wazikwe!"
#MachoziYaMamaDeniLaTaifa 💔
TAARIFA KWA UMMA
Chama cha @ACTwazalendo tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuzuia matukio ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa CHADEMA.
#TaifaLaWote#MaslahiYaWote
Maazimio ya Kamati Kuu kuhusu mustakabali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK)
Kamati Kuu inawapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kukipa imani kubwa Chama cha @ACTwazalendo, Mgombea wake wa Urais wa Zanzibar, Ndg. Othman Masoud Othman na wagombea wake wengine kwenye nafasi za Ubunge, Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi na Udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Kutokana na imani hiyo, Kamati Kuu inaweka wazi kwamba hoja ya ACT Wazalendo haihusiani kabisa na kuingia ama kutoingia kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Maridhiano ya Wazanzibari na Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyoingizwa kwenye Katiba ya Zanzibar mwaka 2010 hata mara moja haikukusudiwa iwe ni kichaka cha kufichia wizi wa kura za wananchi na kisha aliyeiba kura hizo na sauti ya umma amualike aliyemuibia kuingia kwenye Serikali ili ahalalishe wizi huo.
Kamati Kuu inawahakikishia Wazanzibari kwamba lengo la ACT Wazalendo katika kushiriki kwenye hatua zinazoendelea za kuupatia ufumbuzi mgogoro mkubwa uliosababishwa na uporaji wa haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa ni kusimamia mageuzi yatakayohakikisha kwamba haki yao hiyo inarejeshwa na inaheshimiwa. Kamati Kuu imetoa ridhaa yake kwa Timu ya Chama inayoshiriki hatua hizo kusimamia msingi huo.
Makamu Mwenyekiti Bara
@MchinjitaIR
#MaazimioYaKamatiKuu
Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu kunyongwa hadi kufa maafisa watatu wa Uhamiaji, Fredrick Kyomo, Joachim Trathizius na Mabruki Hatibu, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Enos Elias, mkazi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, aliyekuwa akishukiwa kuwa si raia wa Tanzania.
Chama cha @ACTwazalendo, kupitia
KCM @zittokabwe kilipaza sauti na kutaka haki itendeke. Zaidi Mstaafu na viongozi wa chama mkoa wa Kigoma walifika nyumbani kwa mama wa marehemu na kumfariji.
Hatimaye jana Desemba 15, 2025 haki imetendeka.
#TaifaLaWote
#MaslahiYaWote
KC @SemuDorothy alipozungumza na @AlJazeera, aliaangazia haki ya kuandamana na umuhimu wa Serikali kusikiliza madai ya waandamanaji; hasa ya vijana ambao kwa kweli wana changamoto nyingi zinazohitaji majibu ya kueleweka na kutekelezeka.
#TaifaLaWote#MaslahiYaWote@ACTwazalendo
@bbcswahili@NdagijeVeronic2 ACT ilishiriki 2025 ili kuthibitisha uchafu wa CCM kwa ulimwengu – na imefanikiwa! Sasa inakataa tume feki ya serikali na inahitaji tume huru kimataifa. Boycott ni chaguo lenu, lakini kushiriki ili kupambana si usaliti. Tusiachane, tuungane kupigania haki!
ACT imetangaza wazi: KUKATAA NA KUPINGA MATOKEO (taarifa ya Nov 9, 2025). Ilisema uchaguzi ulichafuka kwa mauaji, vitisho na hila. Hata sasa inakataa tume ya serikali ya uchunguzi (Nov 18, 2025) coz ni dhihaka na inahitaji tume huru ya kimataifa (UN, AU, Commonwealth)@zittokabwe