Siri ya kufanikiwa ni nin ?
Ingawa kila mmoja anatamani kufanikiwa kwenye maisha haya na waliofanikiwa hawezi kukuambia namna alivyofanikiwa..wataishia kukupa stori za insparation na kukumotivate..
Emb tupeane darasa kidogo wadau
Moja ya habari kubwa kuhusu yanayojiri Urusi kwenye mkutano unaoendelea kati ya Putin na Viongozi wa Afrika ni hii ya Rais Putin kumzawadia Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Helikopta ya Rais (M1-38) wakati wa mkutano unaoendelea Urusi kati ya Putin na Viongozi wa Afrika.
Wizara ya Habari ya Zimbabwe imesema "Mh Rais Putin amempa Mh Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa Helikopta ya Rais, ambayo hivi karibuni itawasilishwa Zimbabwe”
Ofisi ya Rais wa Zimbabwe imesema Helikopta hiyo ina uwezo wa kubeba Watu wanane upande wa VIP na Watu hadi 30 upande wa siti za kawaida.
Putin na Mnangagwa hapo awali walikutana kwa ajili ya mazungumzo mbali na Kongamano la uchumi linalofanyika Jijini St. Petersberg nchini Urusi.
Putin ameiweka Zimbabwe pia kwenye orodha ya Nchi sita masikini zaidi Afrika ambazo zitapokea nafaka za bure kutoka Urusi baada ya Serikali ya Urusi kujiondoa katika makubaliano ya kuruhusu mauzo ya nafaka ya Ukraine kufikia masoko ya Kimataifa kupitia Bahari Nyeusi.
#MillardAyoUPDATES