Kikao cha Kamati ya Usalama na Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Mara na Wilaya ya Musoma zimekubaliana kuwa shughuli zote za kuirejesha Manispaa ya Musoma katika hali yake ya awali zikamilike ndani ya siku 10 kuanzia leo tarehe 27 Machi, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 26 Machi, 2025 amekabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi shilingi milioni 100 kusaidia wananchi waliopata maafa tarehe 23 Machi, 2025 katika Kata 10 za Manispaa ya Musoma
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara leo tarehe 26 Machi, 2025 ametoa saa 48 kwa taasisi za umma zilizoathiriwa na mvua kubwa
na upepo mkali Manispaa ya Musoma kukarabati majengo na kurejesha huduma
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Majaliwa Kassim Leo tarehe 25 Machi, 2025 ametoa pole kwa wananchi wa Manispaa ya Musoma walioathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kupitia simu ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi
Kamati ya Usalama Mkoa wa Mara tarehe 25 Machi, 2025 imetembelea Manispaa ya Musoma kujionea athari za mvua kubwa iliyoambatana na upepo iliyoathiri majengo, miti, miundombinu ya huduma katika Kata 10 na kuathiri kaya 319, taasisi, maeneo ya biashara na huduma za kijamii
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma Dkt. Martanus Ocholo Omoro akizungumza na Walimu wa Shule za Msingi masomo ya Hesabu na Kiingereza Mkoa wa Mara katika mafunzo yanayofadhiliwa na Mradi wa Shule Bora yanayoendelea katika Hoteli ya Gold Crest, Jijini Mwanza tarehe 25/3/2025
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Makwasa Bulenga amefungua mafunzo ya siku mbili ya Walimu wa Kiingereza na Hesabu, Shule za Msingi Mkoa wa Mara yaliyoandaliwa na Mradi wa Shule Bora, Hoteli ya Gold Crest, Mwanza amewataka walimu kutimiza wajibu wao.
Walimu wa Shule za Msingi masomo ya Hesabu na Kiingereza Mkoa wa Mara walioshiriki mafunzo ya siku mbili yanayolenga kuboresha ufaulu wa masomo hayo wakiimba katika ufunguzi wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mradi wa Shule Bora katika Hoteli ya Gold Crest, Jijini Mwanza leo 25/3/2025
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Edwin Paul Mhede leo amezindua uvunaji wa samaki waliofugwa kwenye vizimba na kueleza kuwa Wakala wa Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA) inaanza uzalishaji wa vifaranga vya samaki eneo la Gangimori, Rorya kuanzia Julai, 2025.
Kamisaa wa Sensa na Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda na Maafisa Habari wa mikoa ya Kanda ya Ziwa katika ufunguzi wa mafunzo ya takwimu yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) tarehe 17-18 Machi, 2025 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 20 Desemba, 2024 kwa niaba ya wananchi na viongozi wa Mkoa wa Mara amepokea zawadi za sikukuu ya Noeli na mwaka mpya kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambapo Mhe. Mtambi ameishukuru TRA kwa zawadi hizo
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo tarehe 20 Desemba, 2024 imempatia tuzo ya shukrani Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari ambayo imekabidhiwa na Kamishna wa Kodi za Ndani Bwana Alfred Mregi
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 20 Desemba, 2024 amewapokea na kuzungumza na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiongozwa na Kamishna wa Kodi za Ndani Bwana Alfred Mregi ambapo Mhe . Mtambi ameipongeza TRA kwa ukusanyaji mzuri wa kodi
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo amezungumza na Waandishi wa Habari na kuwahakikishia usalama wananchi wa Mkoa wa Mara wakati huu wa sikukuu za Noeli na mwaka mpya na kulitaka Jeshi la Polisi kuongeza doria na udhibiti wa madereva wa vyombo vya moto.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo 12/12/2024 ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri (RCC) amezipongeza Halmashauri kwa makusanyo mazuri ya mapato ya ndani ambapo hadi tarehe 30/11/2024 zimekusanya shilingi bilioni 16.516 sawa na asilimia 107 ya lengo
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 12/12/2024 amezindua Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kuitaka Bodi na Menejimenti ya Hospitali kusimamia maboresho ya utoaji huduma na mapato ya uendeshaji wa hospitali hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Dkt. Khalfany Haule leo tarehe 11 Desemba, 2024 amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara kuongoza kikao cha Baraza la Biashara Mkoa wa Mara amekemea baadhi ya wafanyabiashara kupitisha bidhaa kwa njia zacmagendo kutoka nchi jirani na kuwataka kulipa kodi stahiki
Mkuu wa Wilaya ya Rorya leo tarehe 11 Desemba, 2024 amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara kuongoza kikao cha Biashara cha Mkoa wa Mara na amekemea baadhi ya wafanyabiashara kupitisha bidhaa za magendo kutoka nchi jirani na kuwataka kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Nchi yetu