"Tuna jeografi ambayo nchi nyingi za Kiafrika hazina. Sisi tunaunganisha masoko mawili; soko la SADC na EAC. Tungenyimwa kila kitu, bandari tu ingeweza kuiendesha hii nchi. Je! Tunaitumia hiyo jeografia?"
Kiongozi Mstaafu wa @ACTwazalendo@zittokabwe#TaifaLaWote#MaslahiYaWote
DKT. NASRA AIBUA MAZITO ZANZIBAR: AFICHUA YATIMA KULALA NJAA. AHOJI ZILIKO BILIONI ZA MRADI WA ‘PAMOJA’
Mwakilishi wa Viti Maalumu wa @ACTwazalendo, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi, Mhe. Dkt. @drnasranassor amelipua bomu zito linaloanika uzembe na viashiria vya ufisadi katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Katika hotuba yake Dkt. Nasra amefichua kashfa katika kituo cha kulelea yatima Mazizini, ambapo watoto wanalala njaa wakati stoo imejaa shehena ya chakula kutokana na usimamizi mbovu. Pia, amesema jengo la kituo halijafanyiwa ukarabati tangu mwezi Machi lilipoungua moto.
Kuhusu mradi wa jinsia wa PAMOJA, Dkt. Nasra amebainisha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2025/2026 Serikali iliweka Sh bilioni 6.512 kwenye mradi wa PAMOJA, walakini ni Sh milioni 685 tu (10%) ndio zilizotumika hadi mwaka wa fedha unamalizika. Hapa Dkt. Nasra akahoji, ziko wapi asilimia 90 ya fedha zilizotengwa?
Kwenye mradi wa Nyumba za Limbani (Sh bilioni 2.2), Dkt. Nasra ameeleza kuwa kamati yao ilibaini njama za watendaji waliotaka kumfukuza mkandarasi aliyebakiza hatua za mwisho (finishing) na ambaye tayari ameshalipwa 93% ya fedha, kwa lengo la kuingiza mkandarasi mpya.
Kufuatia msimamo huo wa Dkt. Nasra, Wizara imetakiwa kutoa majibu ya kina mbele ya Baraza kabla ya bajeti mpya kuidhinishwa.
#ZanzibarMpya #ZanzibarMoja #MamlakaKamili
"Jitihada ifanyike ya kulisafisha Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi halipaswi kuwa jeshi la kutumia nguvu kupita kiasi kwa raia."
Mwakilishi wa @ACTwazalendo Jimbo la Gando na Mbunge Kutoka Baraza la Wawakilishi
@SaidAliMbarouk#TaifaLaWote#MaslahiYaWote
Leo 30 Mei 2026, nimepata nafasi ya kuwa mmoja ya waliohudhuria kikao cha baraza na kusikiliza Hotuba ya Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyowasilishwa mbele ya baraza la wawakilishi Zanzibar.
DAR: Mwenyekiti wa Chama cha @ACTwazalendo, @othmasoud amesema hayo Mei 16, 2026 wakati akizungumza katika Mjadala wa Kitaifa kuhusu Mwelekeo na Hatima ya Tanzania uliowakutanisha Makada na Viongozi wa Chama hicho, Wasomi, Wanadiplomasia na Waandishi wa Habari.
"Mwaka wa jana Uganda wameuza nje kahawa za thamani ya USD Bilioni 2.6, lakini sisi ambao tuna mara tatu ya ardhi inayolima kahawa kuliko Uganda, tumepata kama USD Milioni 150."
Kiongozi Mstaafu wa @ACTwazalendo@zittokabwe#TaifaLaWote#MaslahiYaWote
"Hii bandari ya Dar, nchi mbili tu, DRC na Zambia; zikiamua kutopitisha mizigo yao hapa, hii bandari inakuwa haina kitu. Kwa sababu ⅔ ya mizigo ya bandari yetu inakwenda na kutoka katika nchi hizo"
Kiongozi Mstaafu wa @ACTwazalendo@zittokabwe#TaifaLaWote#MaslahiYaWote
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema kitendo cha Wananchi kushangilia pindi Viongozi wa Nchi Wanaporafiki ni matokeo ya Chuki na hasira kubwa iliyojengwa kwa Wananchi na Vingozi ikiwemo yaliyotokea katika uchaguzi Mkuu wa Octoba 2025.
Akizungumza kwenye Mdahalo wa Kitaifa kuhusu mwelekeo na Khatima ya Tanzania, leo May 16, 2026, Jijini Dar es salaaam, Othman amesema “Mshikamano wa kijamii umeyumba sana tunasema pamoja na utamaduni huu wa Mtanzania wa kuwa na mshikamano, kuwa na uvumulivu lakini kwa yaliyotokea katika uchaguzi basi umeyumbisha sana mshikamano huu wa Kitaifa tumeona Chuki kubwa ambayo imejengwa hasira kubwa ambayo iko kwa Wananchi”
“Tunachosikitika na kinachosikitisha ni kwamba viongozi badala ya kuona hili ni tatizo walichukulie hatua wao wanalaani watu wanaoshangilia Kiongozi anapofariki haya ni matokeo tu ya kile ambacho mmekitengeneza sasa wakulaaniwa ni nani? Ndie aliyevuna matokeo au aliyesababisha tukafika hapa ndio maana mimi nasema haya yote ni matokeo ambayo mimi nayaita uasi katika Nchi hii na uasi mkubwa ni pale ambapo mna Viongozi ambao hawataki kwa makusudi, wanavuruga misingi ya Katiba, misingi ya Sheria katika Nchi na kutufikisha hapa tulipo”
#MillardAyoUPDATES
VIDEO:
Profesa mkongwe wa Sheria nchini Profesa Issa Shivji ametolea ufafanuzi uhusiano wa msingi kati ya amani na haki, akijenga hoja kuwa uwajibikaji ndio unaofanya kazi kama daraja muhimu kati ya mambo haya mawili mema.
Akizungumza leo, Mei 16, 2026, kwenye Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Demokrasia jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na chama cha @ACTwazalendo , Shivji ameweka msimamo kwamba jamii haiwezi kufikia amani ya kudumu bila haki, wala haiwezi kupata haki bila kuwepo kwa utamaduni thabiti wa watu kuwajibika kwa matendo yao.
“Bila uwajibikaji huwezi ukawa na haki na bila haki huwezi kuwa na amani, na katika tukio lililotokea suala muhimu linajitokeza ni uwajibikaji. Kwa maoni yangu hatuwezi tukapiga hatua yoyote ile bila uwajibikaji”, ameeleza Shivji.
Makamu Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu, amesema chama hicho kimeandaa mkusanyiko mkubwa wa kitaifa kwa ajili ya kujadili matokeo ya tume iliyoundwa na Rais kuchunguza matukio ya Oktoba 29, 2026.
Jussa amesema hayo leo Jumamosi, Mei 16, 2026, alipokuwa akihutubia Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Demokrasia linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema uamuzi wa chama hicho kuitisha mkusanyiko huo umetokana na hatua ya Serikali kutoweka hadharani ripoti kamili ya tume hiyo, huku muhtasari pekee ukiwasilishwa na mwenyekiti wake, Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman.
#mwananchiupdates
#tunawezeshataifa
VIDEO:
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman (OMO), amesema kuwa kuna mgogoro mkubwa katika mfumo wa kikatiba wa Tanzania, akidai kuwa misingi ya kidemokrasia ya taifa imebomolewa kwa makusudi kufuatia mzunguko wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliogubikwa na ghasia.
Akihutubia Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Demokrasia nchini leo Jumamosi, Mei 16, 2026, jijini Dar es Salaam, OMO amelaani ukosefu wa uwajibikaji na amekosoa uchunguzi rasmi wa Tume ya Jaji Chade akidai kuwa imezidisha majonzi ya familia za wahanga badala ya kutoa haki.
Aidha, ameonya kuwa kuzimwa kwa uhuru wa kujieleza bungeni na kuibiwa kwa haki ya wananchi ya kupiga kura kumewageuza raia kuwa 'watawaliwa' (subjects), jambo ambalo kwa hakika limeharibu uhusiano muhimu wa uzalendo, akiongeza kuwa pale nguvu ya kuchagua viongozi inapoporwa na kikundi kidogo cha watu, uwepo wenyewe na uhalali wa kimaadili wa dola unakuwa hatarini.
VIDEO:
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman, amesema kuwa Tanzania kwa sasa ipo katika kipindi cha mpito na mkanganyiko mkubwa unaohitaji uongozi thabiti ili kuepusha mkwamo wa kisiasa, kiuchumi, na kijamii.
Akihutubia Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Demokrasia nchini leo Jumamosi, Mei 16, 2026, jijini Dar es Salaam, Othman amebainisha kuwa tathmini ya chama chake inaonyesha nchi inahitaji mwelekeo mpya kufuatia matukio yaliyojiri kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Othman ameeleza kuwa sababu kuu ya ACT Wazalendo kuitisha kongamano hilo la wadau ni kutokana na ukweli kwamba nchi ipo katikati ya changamoto kubwa. Amesema bila kupatikana kwa uongozi thabiti wa kutoa dira na mwelekeo sahihi, nchi inaweza kutumbukia kwenye mkwamo mkubwa zaidi usio na shaka.
"Siasa za kidemokrasia zimetoweka na mamlaka ya wananchi kuchagua viongozi imetekwa nyara na watu wachache. Vyama vya Siasa, ikiwemo CCM, haviendeshi tena siasa ya nchi badala yake, siasa imeachwa mikononi mwa kikundi cha watu wachache."
Mwenyekiti wa @ACTwazalendo@othmasoud
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
#MjadalaWaKitaifa
Profesa mkongwe wa Sheria nchini Profesa Issa Shivji ametoa simulizi ya kihistoria ya ghasia za dola na vitendo vinavyofanywa na polisi nchini Tanzania, akitaja majanga maalum kama vile mauaji ya katika shamba la sukari Kilombero na mauaji ya wafanyabiashara wa Arusha ili kuangazia ukosefu wa uwajibikaji unaojirudia.
Akizungumza leo, Mei 16, 2026, kwenye Kongamano la Kitaifa la Wadau wa Demokrasia lilioandaliwa na chama cha ACT Wazalendo jijini Dar es Salaam, Shivji amejenga hoja kuwa haki yenye maana haiwezi kupatikana kupitia ripoti za serikali zinazotoka juu kwenda chini au mikutano ya milango miwili, kwani mbinu hizi mara nyingi zinafeli kuleta mabadiliko ya kweli. Badala yake, Shivji ametoa wito wa kuwa na mjadala wa umma jumuishi, akisisitiza kuwa amani inategemea daraja la uwajibikaji lililojengwa na wananchi wenyewe.