Katibu wa Fedha na Uchumi wa @ACTwazalendo, Ndugu @RachelKimambo amewaeleza wananchi wa Simbo Jimbo la Kigoma Kaskazini kuwa kwenye chaguzi zijazo waikatae CCM kwa sababu imeshindwa kuleta huduma bora za kijamii; badala yake waichague ACT-Wazalendo.
#Miezi10#WanachamaMilioni10
FOLENI YA KADI ZA ACT WAZALENDO
Wananchi wa Kata ya Nkunguru Jimbo la Magu wakiwa kwenye foleni kusubiri kusajiliwa kuwa wanachama wa ACT Wazalendo baada ya Mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu Katani hapo jana tarehe 22 Julai.
Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara wa @ACTwazalendo, Ndugu @Mwanaishamndeme amesikitishwa na kauli chafu za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila zilitolewa Julai 13 akizungumza na Wamachinga katika stendi ya Simu 2000
Aidha Ndugu Mwanaisha Mndeme ameitaka Serikali kuhakikisha inatoa mpango mkakati utakaotatua changamoto za wamachinga nchini.
"Tunaitaka Serikali ije na mpango mkakati wa wazi kuhusu suala la Wamachinga." Mwanaisha Mndeme
Vilevile Waziri Kivuli amesema kama suala la wamachinga halitatatuliwa kwa wakati sahihi litaleta madhara makubwa nchini kwani asilimia kubwa ya vijana wamejiajiri kwenye shughuli hizo.
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
https://t.co/i9K0Wo72yT
"Miili ya watu inazuiliwa hospitali. Inakaa kwenye majokofu kama samaki. Watu hawapewi miili ya wapendwa wao hadi walipe madeni ya matibabu. CCM haiwapendi Watanzania wakiwa hai na hata wanapofariki."
Makamu Mwenyekiti wa @ACTwazalendo Bara
@MchinjitaIR#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
Kwa muda wa siku saba Waziri Kivuli wa Maji wa @ACTwazalendo, Ndugu @CornelySinta amefanya ziara katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es salaam na kujionea namna tatizo la maji lilivyokuwa kubwa. Hali hii iko maeneo mengi ya nchi yetu, vijijini na mijini.
Ili kumaliza tatizo hilo, Waziri Kivuli anapendekeza Serikali itenge Shilingi trilioni 2 kila mwaka katika kipindi cha miaka 5. Aidha ameitaka Serikali kutoa ruzuku kwa mamlaka za maji ili kuziwezesha mamlaka hizo zitoe huduma nzuri na toshelevu kwa wananchi.
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
FEDHA ZA BAJETI ZINAKWENDA WAPI?
Mgawanyo wa matumizi wa fedha za serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 unaonyesha kuwa Shilingi trilioni 34.6 imetengwa kwa ajili ya matumizi ya Mishahara, posho, magari na misafara ya viongozi, chai na Deni la Serikali ambayo ni sawa na asilimia 70%.
Wakati miradi ya barabara, mikopo ya wanafunzi, ujenzi wa vituo vya afya, shule, madawa, maji, pembejeo za kilimo, imetengewa Shilingi Trilioni 14.75 sawa na 30.%. hii maana yake ni kuwa katika kila shilingi elfu moja ni shilingi 700 inaenda kwenye chai na posho na shilingi 300 tu ndio inaenda kuhudumia wananchi.
Waziri Mkuu Kivuli wa @ACTwazalendo@MchinjitaIR
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
"Nchi yetu ina uhitaji wa wahudumu wa afya zaidi ya 150,00 na bajeti iliyopita juzi inakwenda kuajiri wahudumu 13,000 tu. Watanzania wanakufa majumbani mwao kwa kukosa huduma ya afya."
Waziri Mkuu Kivuli wa @ACTwazalendo@MchinjitaIR#TaifaLaWote#MaslahiYaWote
VIDEO:
“ACT Wazalendo tulimwambia Rais Samia hatutaki uchaguzi wa Serikali za Mitaa uongozwe kutokea Ikulu kwa sababu Ikulu inaongozwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, hatukubali. Kwa niaba ya Rais, TAMISEMI inaongozwa na Waziri wa TAMISEMI bwana Mchengerwa ambaye mara kadhaa amenukuliwa akisema kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi itafanya vizuri kwenye chaguzi zinazokuja” Ado.
Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu akizungumza katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na uongozi wa chama hicho Kata ya Tandika katika Jimbo la Temeke Jumapili Juni 30, 2024.
Makamu Mwenyekiti wa @ACTwazalendo Bara, Ndugu @MchinjitaIR amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Jimbo la Kondoa. Pamoja na mambo mengine, Makamu Mwenyekiti amewataka viongozi wa Kondoa na Mkoa mzima wa Dodoma kujipanga vema kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
#NECijiuzulu
"Tunachukua fedha tunakwenda kununua ndege, halafu ujenzi wa madarasa tunakwenda kukopa. Tukichukua mikopo, basi mikopo hiyo ielekezwe kwenye sekta ambazo zenye mnyororo mkubwa wa ajira; mfano kilimo."
Waziri Kivuli wa Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira, Mhandisi @Ndolezi_Petro@ACTwazalendo
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote
"ACT Wazalendo tutakwenda kwenye kikao cha wadau kilichoitishwa tarehe 15 Juni, 2024 Dodoma kuieleza TAMISEMI isimamishe mara moja mchakato
inaoendelea nao wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu ni batili na unavunja sheria za nchi." -Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT Wazalendo
"ACT Wazalendo tumewasiliana na Asasi za Kiraia juu ya umuhimu wa kufungua kesi Mahakamani kuzuia hatua za maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa zinazoendelea kuchukuliwa na TAMISEMI. Tumefarijika kuwa Asasi hizo zipo kwenye hatua za mwisho kufungua kesi hiyo. ACT Wazalendo itatoa ushirikiano kwa taasisi hizo kwenye kesi hiyo"-Ado Shaibu, Katibu Mkuu ACT Wazalendo
"Tunaitaka Serikali izibe mianya ya utoroshwaji wa madini na kuchukua hatua kali kwa wahusika wa vitendo hivyo. Pia isimamie utekelezaji wa sheria ya madini na kanuni zake zinazoipa Serikali 16% ya umiliki kwenye makampuni ya madini."
Naibu Waziri Kivuli wa Madini
@RayaIbrahim3
"Tunaitaka Serikali kumaliza kadhia ya uvamizi wa tembo, wanyama waharibifu na isitishe operesheni za kuwaondoa kwa nguvu wananchi wanaozungukwa na maeneo ya hifadhi nchini."
Naibu Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii
@AnthonyishikaTZ@ACTwazalendo#TaifaLaWote#MaslahiYaWote