Jaji Mkuu wa Tanzanaia, George Masaju amesimulia namna alivyomsaidia bibi mmoja ofisini kwake na haikuchukua muda akateuliwa na Rais Kikwete kuwa mshauri wake wa masuala ya sheria. Ameyasema hayo tarehe 17 Juni, 2026 alipokuwa akizungumza na Naibu Wasajili wapya 31 walioapishwa
Marais wote wastaafu wa USA walio hai wameungana na Barack Obama katika tukio lake la kuzindua kituo chake huko Chicago chenye lengo la kusaidia jamii. Kina makumbusho, Library, Studio ya Muziki, viwanja vya basketball, Kumbi za mikutano, gym nk. Bush wa chama pinzani naye yupo
"Lissu hana kosa, anachosema ni kwamba rasilimali za Nchi hii zitumike kwaajili yetu sote na ndiyo maana tunakuja tunasema mzizi wa fitna wa mambo yote haya yatakatwa na Katiba mpya. Na tunazunguka sasa hivi kuwaomba watanzania wote mtuunge mkono kwenye suala la kudai katiba mpya na kuwaambia wamuachie Lissu, wasipitusikiliza kwasababu Nchi hii ni ya kwetu sote tutaenda hatua ya pili."
"Huu ndio ujumbe wetu kwenu na tunazunguka kusema, hatuna chuki na mtu, hatuna hasira na mtu lakini tunashida na Nchi yetu inavyoendeshwa." Amesema Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania bara Bw. John Heche, akizungumza na wananchi wa Nachingwea kwenye Viwanja vya Mahuridi, Majengo C leo Alhamisi Juni 18, 2026.