Hello Dearsโฅ๏ธ Mungu ametubariki na week nyingine tumshukuru๐ Iwe week ya kuona miujiza ya Mungu katika njia zako za utafutaji Mungu asikie kuomba kwako na kukufanikisha zaidi ya yote akuepushe na kila ubaya uliojipanga kukudhuru๐๐
Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
Isa 43:2 SUV
Hello Dearsโฅ๏ธ Giza halimaanishi chochote kwa mtu mwenye mwanga katika moyo wake na ufahamu wake unaona kile anachokitaka Nia ya dhati humpa njia ya kufikia malengo yake bila kukwamishwa na mazingira wala ugumu unaokutana nao My Friend Dhamiria Unaweza๐ช๐
Njaa, kukataliwa, na kucheleweshwa sio ishara ya kushindwa, ni mazoezi ya moyo kabla ya ushindi. Endelea kusonga hata kama hakuna anayekupigia makofi, maisha humbariki anayesimama peke yake bila kelele. Ndoto haifi kwa sababu ya kuchelewa, inafia pale unapochoka kujaribu
ANGUKO LINALOTOKANA NA KIBURI CHA UZURI NA UTUKUFU
Eze 28:17 SUV
[17] Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.
Mfalme wa Tiro alijawa na kiburi kingi kutokana utajiri wake, uzuri wake, na nafasi yake ya kifalme. Hivi vilimfanya ajione yeye ndio kila kitu.
Lugha iliyotumika katika mstari inataka kufanana na simulizi ya anguko la Shetani, pale alipojiona anaweza kukaa kwenye nafasi ya Mungu.
Isa 14:12-15 SUV
[12] Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa! [13] Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. [14] Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. [15] Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo.
Vile vitu vinavyotolewa na Mungu na kuwafanya watu waonekane ni wa maana hapa duniani, hugeuka kuwa chanzo cha majivuno kwao waliopewa hiyo fursa na mwisho wake hupata anguko baya.
Tunapaswa kuelewa kuwa kiburi na Mungu havikai pamoja, Mungu akikuinua eneo fulani, alafu ukajisahau na kujawa na kiburi, utakuwa umejitangazia kwa Mungu hutaki kuendelea kuwa na hayo mafanikio yako.
Yak 4:6 SUV
[6] Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
Mfalme wa Tiro ni mfano kwetu wa kuona vile mtu anayejivuna kwa vipawa vyake, na kusahau ile neema ya Mungu iliyomfanya awe hivyo alivyo, awe na uhakika atapokea anguko baya katika maisha yake.
Vile ulivyo leo, uzuri wako, uwezo wako wa kifedha au kiuchumi, nafasi yako ya uongozi, hekima ulizonazo, unapaswa kutambua ni Mungu amekufanya uwe hivyo ulivyo na sio kujifanya wewe ni mungu.
Kiburi chako kisije kikakuharibia kwa Mungu, utakuwa umepoteza uzuri wote uliokuwa nao, utapokea kifo cha kiroho, uhusiano wako na Mungu utakufa, na utapoteza nafasi yako na heshima yako.
Kristo ni mfano kwetu wa unyenyekevu, alijinyenyekesha hadi akatupatia ukombozi msalabani (Fil. 2:5-11). Hekima yake na uzuri wake unapaswa kuwa njia yetu ya kufuata.
Ukiwa mwamini usije ukajivunia vipawa vyako vya kimwili au kiroho, badala yake ishi kwa unyenyekevu, ukijua ni neema tu imekuangukia ukawa hivyo ulivyo. Hapo utaendelea kula matunda ya unyenyekevu wako.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
Yeremia 15:19
[19]Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ukirudi, ndipo mimi nitakapokurejeza, upate kusimama mbele zangu; nawe ukitoa kilicho cha thamani katika kilicho kibovu, utakuwa kama kinywa changu; nao watakurudia wewe, bali hutawarudia wao.