my daughter, amayra, turned one year old today. please join me and my family in wishing her a very happy birthday. baby amayra, as her brothers assad and anwar call her, means the world to me, and i thank my wife, and her lovely mother, @zahratunda, for her โค๏ธ:
shukran sana. binafsi nadhani si sawa kuihukumu jamii nzima kwa vitendo vya watu wake wachache. lakini, endapo kama waislamu, na wazanzibari, watakubali utambulisho wao utumike kama dekio la kusafishia ukatili wa dola, wasikasirike watu wakiwashambulia. actions have consequences!
Leo, kama Siku ya Baba Duniani, nimekumbuka kisa kimoja kuhusu baba yangu nikiwa chuoni UDSM. ๐๐ฟ
Nilipokuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa kujiunga na UDSM, nakumbuka ndiyo ilikuwa mara ya kwanza baba alinipa TZS 100,000 kama pocket money. Njiani nikakata tiketi ya Rungwe Express kutoka Tunduma hadi Dar es Salaam.
Baada ya kuanza chuo maisha yalikuwa magumu sana. Mwanzoni nilipata mkopo wa 80%, lakini baadaye ukakatwa nikabaki na 0%. Nikawa napata boom tu, ambalo lilikuwa linasaidia kulipa ada kwa kushirikiana na mzee. Pocket money nilikuwa napewa TZS 15,000 au 30,000 kwa mwezi hela ambayo haikutosha kabisa, japo nilikuwa hostel. Mara nyingi nilikuwa nakula kwa kuchanga na wenzangu au kunywa chai na keki pale Hall 5 UDSM au kwenda riverside kwa wale wa mama wa barabarani usiku au kula kifusi๐ .
Baba yangu, licha ya umaskini wake, suala la elimu alikuwa halichezewi. Angeweza kufanya chochote ili nisiikwame shule.
Siku moja nikampiga kibomu. Nikamwambia kwamba sisi wanafunzi wa sayansi tunatakiwa kwenda maabara na kila mmoja achange TZS 500,000. Ukweli ni kwamba nilihitaji pesa za kununua nguo na simu kwasababu mimi chuo nimeenda sina smartphone wala laptop. Nilijua tu nikimwambia hivyo, mzee angefanya lolote kuhakikisha sipati shida chuoni.
Baada ya siku chache akanitumia TZS 500,000. Mimi nikazitumia zote kununua nguo na kutumbua club. Enzi zile maisha ya club LAPF pale Makumbusho ilikuwa moto. ๐
Muda ukaenda, likizo ikafika nikarudi nyumbani. Siku kama ya pili tu, mama akaniambia:
โBaba yako hana amani kabisa. Ana deni kubwa kwa sababu ya pesa alizokutumia chuoni. Ameenda kuuza mahindi shambani kwa hasara, wakati hata hayajakomaa wala kuvunwa, ili tu aweze kulipa deni hilo.โ
๐๐๐ช
Aisee, sijawahi kujuta kama siku ile. Roho iliniuma sana. Fikiria mtu anauza mahindi ambayo bado hayajavunwa kwa hasara, kisa tu alitaka mtoto wake asiikwame chuoni.
Nililia sana. Nikamuomba baba msamaha kwa moyo wangu wote.
Tangu siku hiyo ikawa mwanzo na mwisho wangu kuomba pesa nyumbani kwa matumizi binafsi. Nikajiambia, โMimi na Dar es Salaam mpaka kieleweke. Nilale njaa sawa, lakini sitamuongezea mzigo baba.โ Isipokuwa labda suala la nauli tu.
Leo ninajivunia sana baba yangu. ๐ช๐ฟ
Amenifundisha maana halisi ya kuwa baba. Amenifundisha maana ya kuwa mwanaume. Amenionyesha kwamba upendo wa mzazi haupimwi kwa utajiri, bali kwa kujitoa.
Happy Fatherโs Day kwa baba yangu na kwa mababa wote wanaopambana kimya kimya kuhakikisha watoto wao wanapata maisha bora kuliko wao walivyokuwa nayo. โค๏ธ๐๐ฟ
Mzee, nakupenda sana na nitabaki nakushukuru milele. Ahsante kwa kuendelea kuwa shabiki yangu๐๐ฟ๐ช๐ฟ
That's the difference between men of old and the modern man
When most of you were birthed, your father's weren't even present, they were busy working. Because that's the most important thing a father can do for his wife and child - to work
What's the point of a man being present at the birth of a child? Standing outside the maternity ward just pacing around like a mad man. Or let's say you even get inside, what can you possibly do besides hold her hand, saying "push" as if the nurses can't do that
This is the World Cup, it's your country at war with other nations. You're no different from a soldier on the frontlines saying I need to be excused so I can go see my wife giving birth
This is the current state of modern men, just emotional decisions, to appear good to a female biased society OVER their duty.