Operations Manager at Klimax Solutions - Arusha, Tanzania | Dealing with Digital Printing. We are specialized in Digital Book Printing
Contact us +255687699862
Tuna battle mfumo mbovu ili tupate haki. Tushindane kwa haki. Tuwe na kesho bora. Wewe unaungana na watesi, kwa ubinafsi, thinking utatoboa, uibe uuage ufukara. Mosi, hautoboi. Pili, you are an enemy of the public. Tatu, ukitoboa, hautadumu. Ubaya haudumu!
Kila mtu ana uhuru binafsi, ubinafsi.
Ila kushiriki ubatili ukijua unawapa veggies legitimacy ni suala linalotuhusu.
Ubunge ni utumishi kwetu.
Si suala binafsi.
Kwenu opportunists: welcome to public scrutiny.
Kwanza muangukie pua akili ziwakae sawa.
Then tusalimiane๐ค
@SwahiliBible Happy birthday Mwl.
Maombi yangu kwa Mungu juu yako ni kuwa;-
Aendelee kukubariki na kukutunza
Aendelee kukuongezea maarifa zaidi
Roho Mtakatifu azidi kujaa moyoni mwako
Umri wako ukawe wa baraka kwa wote unaokutana nao
Amen
Hesabu 6:22-26
๐ฉAnaandika Wakili Msomi Jonathan Wilfred Mndeme
Je Chadema itashiriki uchaguzi kwa kutoridhia kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi za mwaka 2025?
Naomba kuanza na Msingi wa kisheria ( Legal principle) ya *โWaiver of right principleโ* Waiving a right means that such a right cannot be claimed by that individual. Kwa tafsiri yangu isiyo rasmi ni kwamba, ukipewa haki na mamlaka au mtu na ukashindwa au ukasusa kutumia haki hiyo; huwezi kurudi kuidai haki hiyo wakati mwingine.
Bahati mbaya sana hiki hakisemwi na wenye maoni tofauti na haya, mimi naona ni mtego mkubwa sana ambao wanaojenga hoja kwamba Chama kiko sahihi kutokusaini Kanuni za Maadili jana tarehe 12.04.2025 wanaenda kukumbana nayo Mahakamani.
Kwa sababu nafahamu baadhi ya CSO/NGO zinapush kwenda Mahakamani kuishtaki Serikali ili Mahakama Kuu itamke kwamba Chama ambacho hakijasaini Kanuni za Maadili kina haki ya kushiriki uchaguzi.
Maswali ambayo Mahakama inaweza ikajiuliza au itawauliza wadaawa ni Je Waombaji walipewa taarifa ya kushiriki kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi!? Jibu litakuwa โNdiyoโ; kwa sababu ni kweli Tume ilipeleka mialiko kwa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu kushiriki zoezi husika.
Kama jibu ni โNdiyoโ, Waombaji waliitikia mwaliko huo!? Jibu litakuwa โHapanaโ.
Kwa Msingi wa โWaiver of rightโ tayari Waombaji watapoteza game ya kisheria kirahisi sana Mahakamani.
Kifungu cha 162 (2) Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024 kinatumia maneno lazimishi (mandatory terms โshallโ) kwamba Tume, Serikali na Vyama vya Siasa vinalazimika kusaini Kanuni za Maadili.
Kifungu cha 162(3) kimeenda mbali kusema kwamba Kanuni hizo za Maadili zitaweka adhabu, moja ya masharti au adhabu za Kanuni za Maadili zilizosainiwa jana kwa mujibu wa Kanuni ya 1.5 (a) ni kutoshiriki uchaguzi.
Hii ni mantiki ya kawaida katika tafsiri ya kisheria ya *โ๐๐๐น๐น๐ผ๐ด๐ถ๐๐บโ* kwa sababu ya premises ambazo nimezieleza hapo juu.
Kwa maoni yangu ya jumla, Chama kimeacha haki yake na hakina uwezo wa kuidai kwa msingi wa โ"๐ช๐ฎ๐ถ๐๐ฒ๐ฟ ๐ผ๐ณ ๐ฅ๐ถ๐ด๐ต๐โ Aidha, kwa msingi wa tafsiri ya kisheria ya kifungu cha 162 kama nilivyoeleza hapo awali na utaratibu wa kuchapisha Kanuni za kisheria kwa Mpiga Chapa wa Serikali kwa ajili ya kuchapwa kwenye Gazeti la Serikali, sioni Chadema ikiwa na nafasi ya kipekee kupewa nafasi ya kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Mwaka 2025. Kwa sababu haki yao waliipoteza jana tarehe 12.04.2025.
Kwa wasilisho langu; Chadema imepoteza haki yake yenyewe na haiwezi kuidai hapo baadae.
I humbly berg to differ na maoni ya Rais wa TLS Boniface Mwabukusi na Wakili Kilatu.
Jonathan Mndeme- Advocate
13.04.2025