@Hakingowi@maelezonews@TZMsemajiMkuu@MadiniTanzania Njia ya pekee na nzuri ya kupunguza mzigo Kwa wananchi kwenye bei ya mafuta ni kufuta/kupunguza ututiri wa tozo kwenye mafuta Kwa nusu yake. Hapo mafuta yatakuwa bei poa sana.
The grievances of the Palestinian people cannot justify the horrific attacks by Hamas.
Those horrendous attacks cannot justify the collective punishment of the Palestinian people.
"Huwezi kuwa unasonga mbele kama hawapo unaowaacha nyuma wala hawapo unaowapita mbele yako. Ukigeuka nyuma na usione wanaokukimbiza ujue wewe ndio wa mwisho. Ukitazama mbele usione wa kuwakimbiza ujue mwisho wako umekaribia. Nafasi zote hizi mbili ni hatari kwa ustawi wako."
"Mzunguko wa kupata mafanikio ni kama mto, matawi na mikondo yake. Ukiona umepata ugumu kwenye kufanikiwa basi ujue aidha mto umebadili uelekeo au ulitegesha kwenye mto wa msimu." ~Togolani Mavura.
"Hata wabinafsi husaidia. Tofauti ya wabinafsi na wasio wabinafsi ni nia nyuma ya msaada wanaotoa. Kusaidia itabaki jambo la hiyari na utu. Tusigeuza lazima na kushinikiza na kumkasirikia mtu kwa kutokukusaidia. Walio tayari na walioguswa watakusaidia. Wasio tayari waelewe pia."
Northern Gaza is going to be turned into Dust if a quick solution for resolving the conflict will not be taken.....this needs to be stopped by the @UN . I condemn what Hamas has done to the people of Israel but innocent Palestinian should not be bombed by Israel in Occupied Areas
"Ingawa ni kweli kuwa hujamjua mtu tabia na hulka zake kikamilifu kabla hajafanikiwa, ukweli mwingine tusioambiwa ni kuwa, nawe hujawajua watu kabla hujafanikiwa. Pata uwajue, pata mjuane!" ~Togolani Mavura.
"Kuishi ni kuegemeana. Kila mtu anatafuta egemeo na wa kumuegemea. Hata yule unayemuegemea na kupata amani ya akili na roho yako, naye kuna mahala kaegemea. Kabla hujaegemea, jiridhishe ikiwa unayemuegemea, anajua umemuegemea, naye kaegemea panapoegemeka. Egemea kwa tahadhari!"
"Usikazane sana kuwashawishi na kuwabadilisha wale wa jana ambao wameshaweka hisia na hitimisho juu yako, kiasi cha kupoteza fursa ya watu wapya kukufahamu katika sura mpya. Songa mbele. Maisha ni kama sura za vitabu, ili usome sura mpya, hauna budi kuifunga ile sura iliyopita."
“Tujifunze kuvumilia watu na machaguo yao ya maisha hata kama hayaleti maana akilini na machoni mwetu. Mengi ya machaguo yetu katika maisha ya leo ni fidia ya yale tuliyoyapania kuyafanya, au kuyamiliki huko nyuma ambayo hatukuweza kuyafanikisha kwa kuwa hatukuwa na uwezo nayo.”
"Binadamu tuna uhuru na mawazo yetu, tuna uhuru na maoni yetu, lakini hatuna uhuru na ndimi zetu. Fikiria unavyoweza, waza unavyopenda lakini sema kwa mahesabu." ~Togolani Mavura.