Asante Mama Yetu na Amiri Jeshi Mkuu @SuluhuSamia#SASHA...Watanzania Tunajivunia jinsi unavyoiunganisha Tanzania yetu Kimataifa. Mungu azidi kukutia nguvu Mama. #Africa4Her@LifefYalilearns
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Balozi wa Sweden Nchini Bw. Anders Sjoberg, Mwakilishi Mkazi wa UN Women hapa Nchini Dkt. Hodan Addo na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake (TAWJA) Jaji Joaquine De Mello.
Wako watu wana karama ya kuleta watu pamoja. Ukikutana nae ni sawa na umekutana na halaiki. Hakikisha unakuwa na mtu huyu miongoni mwa wanaokuzunguka katika maisha yako. Atakupunguzia gharama na muda katika kutatua mambo mengi kwenye maisha yako.
Unaweza kuwajua watu maelfu, lakini pengine ni mmoja tu kati yao ndio aliyebebeshwa 'kifurushi' chako cha mafanikio. Tatizo ni kumjua ni yupi na unamfikiaje alipo. Usimdharau yoyote unayekutana nae au anayekuzunguka, aweza kuwa ndiye, au daraja la kumfikia mwenye kifurushi chako.
@mdudechadematz @SuluhuSamia Wenzio wewe @mdudechadematz wako milembe....usione kuachwa uropoke ni ushindi au sifa kisiasa...asiyefunzwa na mamae ufunzwa na ulimwengu.
Miradi iliyotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa ECDF nchini ni pamoja na ujenzi wa VETA za mikoa, mradi wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Daraja la Kikwete (Malagarasi) na barabara zake, Daraja Jipya la Selander, Hospitali ya Mloganzila na mradi wa kilimo cha umwagiliaji Zanzibar.
Wepesi ule ule tunaouonyesha wa kumsifu Mwenyezi Mungu pale maombi yetu yanapojibiwa na tunapopata, tuuonyeshe pia pale majibu yanapochelewa, tunapokosa au anapopata mwenzetu mwingine. Yawezekana alikutangulia kuomba au yako inapitia kwake. Kupata kwake kwaweza kuwa kupata kwako!
Naipongeza timu yetu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya COSAFA Wanawake 2021. Ubingwa huu unatuletea heshima, unaitangaza nchi yetu na kutia chachu kwa vijana wetu kushiriki michezo. Naipongeza TFF na wote walioshiriki kuiandaa timu yetu.
Nimefurahishwa na ushindi wa Taifa Stars wa 1-0 dhidi ya Benin. Nawapongeza wachezaji, benchi la ufundi na TFF, kwa jitihada za kushinda pambano la leo. Nawatakia kheri katika michezo iliyobaki ili Tanzania iweze kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini Qatar mwakani.
#KaziIendelee
Nakupongeza Bw. Abdulrazak Gurnah kwa kutunukiwa Tuzo ya Nobel katika fasihi ya mwaka 2021. Tuzo hii ni heshima kwako, Taifa letu la Tanzania na Afrika.