Mradi wa Maji wa Miji 28 kutoka Mto Ruvuma umefikia asilimia 97 ya utekelezaji.
Mradi huo tayari umeanza kutoa huduma kwa wakazi 81,000 wa vijiji vya Masuguru na Mangaka.
Morogoro
TANROADS imekamilisha tathmini ya km 2,071 za barabara na madaraja 1,032 ili kubaini maeneo yanayohitaji uangalizi maalum wakati wa mvua za El Niño.
Tathmini hiyo imebaini maeneo 49 yanayohitaji ufuatiliaji maalum na kuweka mikakati ya kupunguza athari za mvua.
Tanzania imetangaza azma yake ya kugombea kiti kisicho cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kwa mwaka 2029–2030, ikiahidi kuendeleza mchango wake katika juhudi za kulinda amani na usalama wa kimataifa.