Mbunge wa Jimbo la Kahama Mkoa wa Shinyanga Jumanne Kishimba akichangia mjadala wa Bajeti kuu ya Serikali 2024/25 unaoendelea Bungeni Jijini Dodoma ameishauri Serikali kuachana na sheria za kikoloni zinazowabana Madaktari na badala yake wawapatie vibali Madaktari waliopo mtaani wakisubri ajira ili waendelee kutibu kama ilivyo Waganga wa jadi.
“Leo tuna Madaktari zaidi ya 7000/8000 hawana ajira waliostaaduy zaidi ya 8000 kwanini Watu hata wasipatiwe leseni kama za Waganga wa kienyeji kwa 30,000 wafanye shughuli zao wengine wamebakiza miaka nane kustaafu na kazi hawajapata, je mtamdai akiwa amestaafu?, waruhusuni watibu watu hali ya Mahospitali tunaifahamu hali hiyo kuna Zahanati zetu zinatibu Watu mpaka saa tano asubuhi na kuanzia saa tano asubuhi mpaka jioni ziko tupu, Daktari aweke bango pale kuwa natibu kwa bei hi ukija hata na mbuzi, kama huna hela utakuja kufanya hata kibarua kwangu”
#MillardAyoUPDATES