Kwa akili za @ccm_tanzania wata mwachia @makonda_paul@MwijakuBurton au Steve nyenyere kujibu mambo muhimu kama haya bila aibu wanaweza wachia machawa kina baba levo ndio wasaidia kusema kwaniaba ya chama nawapa sikuchache utasikia @__abdulazack @SuphianJuma ndio wanasifia kabisa
UTEKAJI WA MUSA MZIBA UNA MKONO WA WATU KATIKA MAMLAKA
Musa Mziba alitekwa tarehe 07 Disemba 2023, ila utekaji wake umegubikwa na utata baada ya kugundulika kuwa waliomchukua walijitambulisha kama polisi huku kukiwa na ushahidi kuwa miezi miwili kabla aliipa taarifa Mamlaka husika kusumbuliwa na polisi kwa shinikizo ya mfanyabiashara mwenzake Dorice Mutalemwa
Dorice mutalemwa ni nani kwenye biasahara ya dhahabu?
Dorice Mutalemwa kupitia kampuni yake inayodaiwa kuitwa Macefield inayojishughulisha na biashara ya madini kama Musa (hivyo ni mhasimu wake kibiashara) alikuwa anadai kuwa anawakilisha (power of attorney) kampuni ya Rwanda iliyokuwa na mkataba na Mzibaz! Akadai Mzibaz haikukamilisha kazi wakati mkataba bado ulikuwa haujaisha! Cha ajabu Dorice Mutalemwa alishindwa kuonyesha nyaraka yoyote wala hakufungua kesi mahakamani bali alitumia jeshi la polisi ZCO Dar es Salaam na polisi Ngara kumnyayasa Musa Mziba! Januari 13, 2023 Musa alikamatwa na ZCO Mafwele na alikaa jela wiki nzima! Hata hivyo ilibidi wamwachie baada ya kuona kuwa Musa alitaka nyaraka na uthibitisho!
Musa aliendelea kusumbuliwa na polisi mwaka mzima akifanyiwa matukio mengi
Taairfa ya malalamiko ya Musa Mziba kuhusu unyayasaji huu ilipokelewa na polisi 13 Oktoba 2023.
Ushahidi wote ulipelekwa na Musa Mziba kupitia mwanasheria wake ikieleza kwa kiina kusumbuliwa na huyu mama ambaye inasemekana kuwa ni mke wa Mutalemwa aliyopo Ofisi ya Rais (hii tutaipakua baadaye) na matukio ya polisi
Utekaji wa Musa umekuja siku mbili baada ya kukamilisha mkataba wake na kampuni ya Rwanda ambayo haijawahi kufungua kesi yoyote.
Sasa SACP Muliro anaposema anasikia Musa alidhulumu watu aseme kwanza wazi kuwa Musa alimshtaki kwa barua na ushahidi Dorice Mutalemwa kwa harassement! Je Dorice amehojiwa? Kwani kuna ushahidi ya kutuma vitisho vya kutosha
Pili, ugomvi wa kibiashara huamuliwa mahakamani na huwa ni CIVIL
KESI yaani kesi ya madai siyo jinai. Kwa nini jeshi la polisi iliingilia na kumbeba Dorice Mutalemwa huku ikimnyanyasa Musa tokea January 2023?
Nani yuko nyuma ya MACEFIELD?
Polisi wanatakiwa kujibu haya wakati tunaendelea na mchakato wa kupeleka suala hili kimataifa!
Msitake hili suala lije kuharibu mahusiano na nchi jirani maana tuna mengine kuhusu hii dili ya Rwanda
Mrudisheni Musa Mziba!
#WhereIsMusaMziba
#ChangeTanzania
Haya mambo yalifanywa na Polisi hulo Senegal 🇸🇳
Najaribu kutafakari hawa polisi leo watamwambia nini Rais Faye hasa baada ya kuwa Rais
Wanasiasa waliowatumia hawa polisi hawana nguvu tena
Polisi kumbukeni, Nchi ni ya wananchi, mambo yakibadilika unabaki pekee yako #ChangeTanzania
Hivi kweli Rais @SuluhuSamia unashindwa kuwawajibisha hawa wezi? Mkuu wa mkoa hadi anataka kulia. Kamata waweke ndani fukuza kazi taifisha mali zao zote Bilion 8 kweli zimeibiwa? @ikulumawasliano tuoneeni huruma sisi wananchi masikini
Mashirika yanayojiendesha kwa hasara...
ATCL-56Bilion
TTCL-800 million
TRC-100.7 Billion
TanOil-60+Billion
Posta-1.3Bilion
Haya Ni Baadhi yaliyosemwa leo na CAG, kwenye hasara mama anaupiga mwingi.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Charles Kichere amesema hasara iliyotengenezwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ni shilingi bilioni 56.64.
Juzi walikua uwanja wa Ndege wanapokea hasara nyingine.
Jana mchana nilifika nyumbani kwa Marehemu Gidion Sanaa Kijana wa bodaboda aliyeuwawa wik iliyopita na wahusika kukamatwa na POLIS Tabata na kuachiwa, Sasa Jana nilisindikizwa na VIJANA wa bodaboda aliokua anafanya nao kazi Marehemu. Cha ajabu wale vijana Leo wamekamatwa wanne
Hajawahi kuwa Diwani, Mbunge wala Waziri. Alikuwa mwanasheria ambaye siasa ilianza kuingia kwenye damu Mwaka 2014 tu na akaishia kufungwa 2023. Ameachiwa huru siku 7 tu kabla ya Uchaguzi na bado Bassirou Diomaye Faye amekuwa Rais wa Senegal. Mungu akipanga, hakuna wa kuzuia.
"Ukaguzi umebaini kuwa Halmashauri hazikukusanya kiasi cha Shilingi bilioni 61.15 kutoka katika vyanzo muhimu na vikubwa wakati shilingi bilioni 6.19 zilizokusanywa hazikuwasilishwa benki . Hali hii inaathiri uwezo wa mamlaka za serikali za mitaa kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa jamii" CAG Kichere .
Hayo yamezungumzwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati akikabidhi ripoti ya utendaji kazi wa serikali na mashirika mbalimbali ya umma ya mwaka 2022/2023
Akili za watanzania wengi zipo likizo. Zaidi ya nusu ya wakazi wa nchi hii walipaswa kuwepo hospitali ya Milembe wanapata matibabu ya afya ya akili. Akili zote zimeelekezwa kwenye Simba na Yanga. Serikali inazitumia timu hizi ipasavyo kutoroka kelele za watu wenye akili timamu.
Wamebana wameachiaaaaaaaa 🤣🤣🤣
Madhulmat na mahodari wameigwaya nguvu ya umma na wameondoa mapendekezo ya kubadili sheria!
Sasa na mkataba FUTENI na hilo liazimio lenu!
#OkoaBandariZetu#TutaelewanaTu
Wakati watanzania maskini wanauana kwa shilingi elfu tano, kuna mbunge analipwa laki nne na sabini (470,000) kama posho kila siku + milioni 16.5 kila mwezi, na kila miaka mitano ana milioni 200+ pensheni kwa kazi ya kuipigia serikali makofi tu bungeni.
Watawala ni laana kwenye hii nchi.
@SuluhuSamia@bunge_tz@tanpol
ARUSHA- KUTOKA KWA MDUDE NYAGALI
-------
Huyu mtu pichani anatufuatilia tangu tupo mahakamani Arusha. Ikafika mahali anatufuata mpaka chooni mimi na mwabukusi. Tukaweka tahadhali ya kumfuatilia bila yeye kujua. Tulipoondoka mahakamani akawa anaongea na simu kuwajulisha wenzake .
Mungu wetu ni mwema sana. Tumeamka salama tena. Tuliyoshindwa jana, leo tutayaweza tusipozimia moyo. Ni Mungu gani aliye mkuu kama Mungu wetu? Mungu wetu anayetenda maajabu na fadhili zake ni za milele. Ondoeni wasiwasi, kukata tamaa, hofu, kutokuamini, wasiwasi kuhusu wapendwa wenu, kwa ndoto zilizopotea au kuvunjika. Kupitia imani, muujiza utakuja, ingawa sio lazima kwenye ratiba yetu au kwa azimio tulilotamani. Tukasome [Mathayo 11:28]
Mwenyekiti CHADEMA Taifa @freemanmbowetz leo katika mkutano wa hadhara Mwanhuzi, Meatu amempokea aliyekuwa Mkuu wa wilaya za Meatu na Maswa na mbunge wa viti maalum (CCM), Rosemary Kirigini na wanachama wengine wa CCM
Tahadhari; Mkuu wa Wilaya ya Meatu, asifukuzwe kazi tafadhali
Namna hii, vyombo vya habari vinahitaji elimu ya katiba kwa miaka mitatu.
Serikali ilipeleka bungeni mabadiliko Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili, 2017 lengo kuruhusu uwekezaji bandarini
Serikali imeyaondoa na kufuta mapendekezo yake yote. Jukumu la bunge likabaki kuwa ni kuketi kama kamati na kuridhia kufutwa mapendekezo hayo.
Habari ya “Bunge lakataa mapendekezo ya serikali kurekebisha sheria” zinatoka wapi? Habari “bunge lagomea marekebisho sheria” mmepewa na nani?
Bunge la Tulia Ackson, ni ‘executive rubber stamp’ halina uwezo wa kukataa au kugomea mapendekezo yoyote ya serikali. Wabunge wake ni wapiga chapa wa hati za serikali.
Msiwape wabunge wa CCM sifa wasizostahili. Hawana akili hizo. Hawastahili sifa njema. Wao hufuata wanachoelezwa katika party caucus ya CCM. Hakuna kupinga.
Sifa wapewe wananchi waliopinga na kugomea kabisa mabadiliko hayo nje ya bunge hadi serikali kubadili msimamo wake. Siyo wabunge wa mchongo wasiojitambua.
Serikali isingeyaondoa mapendekezo yake ya kubadili vifungu vya Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Act, 2017 (No. 5 of 2017), wabunge wangepitisha.
Hatuna ‘elected’ president, bali tuna ‘declared’ president. Hakuchaguliwa na umma. Hatuna bunge bali tunao wawakilishi wa CCM ndani ya jengo la bunge wanaojiita ‘wabunge’
Wananchi kwa upande wetu, hatuna serikali, hatuna mahakama, na kipekee kabisa hatuna bunge. Ni nchi ambayo bunge halijui wajibu wake. Bunge hili halina ithibati ya wananchi.
Bunge hili halijui kama liwakilishe wananchi bungeni au liwakilishe serikali bungeni. Bunge halijui liisimamie serikali bungeni au liwanange wananchi.
Hili ni bunge ambalo hata leo likiambiwa Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa wanapewa Qatar, wabunge wake watashangilia na kuungana na serikali.
Wataimba hadi nyimbo, wataruka juu ya meza, watagonga meza na watasema jambo la Rais ni jambo la CCM hakuna kulipinga lazima lipitishwe. Bunge au mazombi?
MMM, Mtikila.