Siku 577, sawa na mwaka mmoja na miezi saba ya kuhudhuria kesi ya uhaini ya Mwenyekiti Lissu, hatimae kuambiwa kosa ni la uchochezi😁 Anyways #LISSUSIOMHAINI and it has been proven beyond reasonable doubt
6.11.2026: Hukumu ya TUNDU LISSU NA KUMBUKUMBU YA KESI YA MWALIMU NYERERE YA MWAKA 1958. HISTORIA INATUFUNDISHA NINI?
Leo, tarehe 6 Novemba 2026, Tundu Lissu ameshinda kesi ya uhaini lakini mahakama ikasema amepatikana na hatia ya uchochezi (incitement) na kuhukumiwa kifungo cha miaka 4. Tunamshukuru Mungu kwa kesi ya uhaini kutupiliwa mbali na kumpongeza Lissu kwa umahiri na ujasiri wake hadi kujitetea. Lakini hukumu ya uchochezi inasikitisha, inafikirisha na inatukumbusha historia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ambaye naye mwaka 1958 alikutwa na hatia ya jinai ya kashfa (criminal libel) wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Makosa haya mawili ni tofauti kisheria, lakini kesi hizi zinafanana katika jambo muhimu: zote zilihusu kiongozi mkuu wa upinzani aliyeshtakiwa na Serikali kutokana na kauli zake za kisiasa.
Turejee historia.
Tarehe 27 Mei 1958, Mwalimu Nyerere alichapisha makala katika gazeti la Sauti ya TANU, Toleo Na. 29, akiwakosoa Wakuu wawili wa Wilaya wa Serikali ya kikoloni kwa madai ya kutumia madaraka yao vibaya na kuihujumu TANU.
Akafunguliwa kesi ya jinai Na. 2207/1958 chini ya kifungu cha 187 cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code). Serikali ya Uingereza ilitoa maelezo kuhusu mashtaka hayo katika Bunge lake (House of Commons) tarehe 26 Juni 1958.
Nyaraka za UN zinathibitisha kwamba Mwalimu alikutwa na hatia katika mashtaka mawili na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi 3,000 za Afrika Mashariki, sawa na pauni 150 za wakati huo, au kifungo cha miezi sita. Alilipa faini tarehe 12 Agosti 1958 na hakukata rufaa.
Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa. Wanaharakati wa kupigania uhuru huko London walihoji iwapo Mwalimu angepata haki katika mahakama za kikoloni na kudai kuwepo kwa waangalizi huru. Serikali ilikataa, ikisisitiza kuwa uamuzi wa kufungua mashtaka ulikuwa chini ya mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Miaka 68 baadaye, tunajikuta tena tukitafakari maswali kuhusu uhuru wa kisiasa, matumizi ya sheria za jinai na nafasi ya mahakama katika mfumo wa kidemokrasia.
Pamoja na hukumu ya mwaka 1958, Mwalimu Nyerere aliendelea na harakati zake hadi Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961.
Funzo muhimu ni kwamba hukumu ya jinai dhidi ya kiongozi wa kisiasa si lazima iwe mwisho wa safari yake ya kisiasa. Historia inaonesha umuhimu wa kuendeleza majadiliano (dialogue) badala ya mapambano na vurugu (confrontation).
Kwa wanaothamini demokrasia, mfumo wa vyama vingi, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utawala wa sheria, hukumu ya uchochezi dhidi ya kiongozi mkuu wa upinzani inaibua maswali mazito yanayohitaji mjadala mpana wa kitaifa.
Je, mipaka kati ya ukosoaji halali wa Serikali na uchochezi wa jinai ikoje?
Je, mwanasiasa awe mpinzani au wa chama tawala atakosoa je Serikali au kudai maboresho au mageuzi bila kuhofia kutafsiriwa kuwa mchochezi?
Je, wananchi watawezaje kudai haki zao kwa nguvu ya hoja bila kuonekana wanachochea uvunjifu wa amani?
Walimu na wanataaluma tutawezaje kufundisha, kuchambua sera, kutoa mapendekezo na kukosoa mifumo ya utawala bila kuhofu kuitwa wachochezi?
Viongozi wetu wa dini watawezaje kutekeleza wajibu wao wa kinabii wa kukemea maovu na kusimamia haki bila kuonekana wanachochea waumini wao?
Uhuru wa kujieleza una mipaka yake na hauhalalishi haki ya kukashfu, kuchochea vurugu au uhalifu. Lakini ni muhimu sana kuweka mipaka iliyo wazi kati ya uchochezi wa jinai na ukosoaji halali wa kisiasa.
Iwapo sheria za jinai zitatumika kudhibiti ukosoaji halali wa kisiasa au kitaalamu, tunaweza kujikuta tunadhoofisha demokrasia, haki za binadamu, kuongeza hofu na kuzidisha mkwamo wa kisiasa na kiuchumi badala ya kuutatua.
Hukumu ya leo inatupa sababu nyingine ya kujadili kwa kina uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, haki za raia na za vyama vya upinzani na mipaka ya matumizi ya sheria za jinai katika siasa.
Ninarejea msisitizo wangu wa muda mrefu kuhusu falsafa ya Rais Samia ya 4Rs. Tujenge utamaduni wa kusikilizana na kukosoana kwa hoja
TUJISAHIHISHE
“Waheshimiwa Majaji, kwa bahati mbaya sana, mmefanya kile ambacho Mahakama Kuu ya Kenya ilifanya mwaka 1954 katika kesi ya Mzee Jomo Kenyatta. Walimuadhibu kwa sababu ya kuwa mpinzani wa wakoloni. Historia haijawahi kuwaacha salama wale Majaji walioamua kutumika kisiasa. Kwa sababu nyinyi wenyewe mnajua kwamba sina hatia, mnamuadhibu mtu asiye na hatia. Hivyo, nataka niseme jambo moja: Watu wasio na hatia hawaombi msamaha. Wanaoomba msamaha ni wale waliokosa. Huombi msamaha unapokuwa huna hatia. Waheshimiwa Majaji, kwa hiyo, naomba iwekwe wazi katika kumbukumbu rasmi za Mahakama kwamba SIJAOMBA MSAMAHA. Mimi nipo hapa, na Mahakama imekubali kunitia hatiani licha ya kutokuwa na hatia, kutokana na shinikizo na maelekezo ya kisiasa. Mahakama inatumika kisiasa. Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, nataka niwe wazi kabisa kwamba maneno nitakayoyasema yasichukuliwe, kwa namna yoyote ile, kuwa ni ombi la msamaha. Siombi msamaha. Siombi msamaha kwa sababu sina hatia kabisa (I am completely innocent).”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
Dakika 7 zilizoshiba Lissu aki analyse
1. Aina za siasa na mabadiliko anayotaka kufanya ndani ya chama na kwa nchi kwa ujumla ( vision yake).
2. Anajibu swali la msingi sana kwanini Wananchi walikuwa wagumu ni wagumu kutoka kuandamana wakati waliwahi kufanya hivyo (Hapa anagusia Upumbavu wa viongozi wa chama kula "dinner na Samia na Abdul") Msikilize.
Video credits; @bbcswahili na @awamisammy
Kwa wito wa Kanisa na mimi leo nimeshiriki MISA TAKATIFU ya kuwaombea MAREHEMU wote waliouawa Oct. 29.
Nimesali na kukomunika kwenye kanisa la ST. PETER’S hapa Dar. 🙏🏾🙏🏾
#RipOurMartyrs
#OCTOBER29#MO29 Mauaji ya oktoba 29 Tanganyika , Daima tutawakukumbuka wewe Simon Alex na wengine wote walioporwa uhai Mwenyezi Mungu awape pumziko lenye Rehema yake. Raha ya MILELE uwape ee Bwana namwanga wa milele UWAANGAZIE WAPUMZIKE kwa AMANI Amina .
Naibu Katibu Mkuu akiwasha mishumaa kuwakumbuka marehemu waliouawa Oktoba 29, 2025. Tukio hilo limefanyika kwenye kanisa kuu Katoliki la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Oktoba 29, 2026
Tarehe kama ya leo mwaka jana,ni siku ambayo ilikuwa ngumu,mbaya na ya kuumiza kwa kila mwanadamu mwenye utu,moyo na zaidi iliacha historia na kidonda chenye kovu gumu linalouma wakati wote.Ndugu ,jamaa na rafiki zetu (my cousin Jo😭) walipatwa na madhila ya kuuwawa,kujeruhiwa na wengine kupotea bila kujulikana waliko.Mpaka sasa bado hatujapata majibu ya nani alidhulumu nafsi zisizokuwa na hatia kwani wapo waliokumbwa na mauti wakiwa majumbani,watoto wadogo,watu waliokuwa kwenye majukumu yao na wale walioamua kutoka kudai uwajibikaji,uchaguzi huru ,uwazi na usawa .Mungu wa mbinguni tunakuja leo tukiomba uwape pumziko la milele wote waliopoteza maisha ,waponye majeruhi na waliopondeka mioyo na mwisho wafariji wote wanaoendelea kuishi na maumivu makali ya kutowaona wapendwa wao.Mwisho tunaliombea Taifa hili la Tanzania likapate kurudi kwenye hali ya amani ,upendo na utulivu kama ulivyokuwa historia yetu.R.I.P Makamanda 😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️❤️🇹🇿
Oktoba 29, 2026, ni siku ya majonzi kwa Tanzania, ikitimiza mwaka mmoja tangu ghasia zilizohusishwa na Uchaguzi Mkuu wa 2025 zilipogharimu maisha ya mamia ya watu na kujeruhi maelfu. Nyuma ya takwimu hizo kuna familia zilizopoteza wapendwa wao, watoto waliobaki yatima na wazazi ambao hadi leo wanabeba maumivu yasiyoelezeka. Kwa wengi, siku hii si tarehe tu, bali ni kumbukumbu ya maisha yaliyokatika na maswali ambayo bado hayajapata majibu.
Ripoti ya Tume ya Uchunguzi iliyoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman, iliyokabidhiwa Aprili 23, 2026, iliweka wazi ukubwa wa maafa hayo. Tume iliripoti vifo vya watu 518 na kueleza mazingira mbalimbali yaliyochangia ghasia hizo. Takwimu hizo zimebaki kuwa alama nzito katika historia ya taifa, zikikumbusha kuwa nyuma ya kila kifo kulikuwa na ndoto, familia na maisha yaliyokuwa na thamani.
Ripoti hiyo ilieleza pia changamoto zilizozunguka uchaguzi na sababu mbalimbali zilizochangia vurugu, huku ikiweka wazi haja ya uchunguzi zaidi ili kubaini wajibu wa wahusika. Vilio vya wananchi vinahusu si vifo pekee, bali pia waliopotea, waliojeruhiwa na familia zinazotaka kujua ukweli. Kwa wengi, haki haitakuwa imepatikana mpaka maswali yao yajibiwe na hatua stahiki zichukuliwe.
Wakati wa kupokea ripoti hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan aliahidi Serikali kutekeleza mapendekezo yake, kufanya uchunguzi wa kina na kuunda Tume ya Maridhiano itakayosaidia kuponya mipasuko ya kitaifa. Alisema mapendekezo hayo ni kama dawa ya kuponya taifa, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na kuzuia matukio kama hayo kujirudia. Ahadi hiyo imekuwa kipimo muhimu ambacho wananchi wanakitazama kwa matarajio ya kuona matokeo yanayogusa maisha yao.
Serikali imeeleza pia hatua za kufuatilia madai ya uhalifu, watu waliopotea na kusaidia waliojeruhiwa. Hata hivyo, mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu, yakiwemo Amnesty International na Human Rights Watch, yameendelea kutaka uwazi, uchunguzi huru na uwajibikaji wa waliohusika. Familia bado zinahitaji majibu, huku jumuiya za kimataifa zikisisitiza kuwa amani ya kudumu haiwezi kujengwa bila ukweli na haki.
Leo, makanisa, jumuiya na taasisi mbalimbali zinapokumbuka siku hii kwa sala, toba na maombolezo, taifa linapaswa kusimama na kutafakari maumivu yaliyobaki. Oktoba 29 haitakiwi kuwa kumbukumbu ya vifo pekee, bali onyo dhidi ya chuki na migogoro inayoweza kugharimu maisha.
Mwaka mmoja baadaye, kilio kikubwa cha taifa ni ukweli, haki na uhakika kwamba maafa kama haya hayatarudiwa tena.
Today, the U.S. Embassy community joined me to honor the memory of all those who lost their lives in the violence surrounding Tanzania’s October 2025 general elections. We remember them, and the families who still grieve and seek answers. As I said to the U.S. Senate during my confirmation hearing, this will not be swept under the rug.