Wananchi wa Kisaki wakilalamika ndugu zaoekuuwawa na Askari wa wanyama Pori, wamesema msituni kuna mafuvu mengi ya binadamu WENZAO. #MsiogopeTunashinda
Kabla Taifa Halijaanguka
Na Rev Peter Simon Msigwa
Kabla taifa halijaanguka, mara nyingi taasisi zake ndizo huanza kuchoka.
Sheria hubaki imeandikwa, lakini huacha kutawala. Katiba hubaki kwenye vitabu, lakini huacha kuwa mwongozo wa maamuzi ya kila siku. Bunge huendelea kukutana, lakini uwezo wake wa kuisimamia Serikali hupungua. Mahakama huendelea kufanya kazi, lakini wananchi huanza kuhoji kama haki inatolewa bila upendeleo. Polisi huendelea kuvaa sare, lakini utii wao huanza kuelekezwa zaidi kwa amri za watu kuliko kwa mamlaka ya sheria. Viongozi wa dini huendelea kuhubiri, lakini sauti ya kinabii ya kutetea haki, ukweli na utu wa mwanadamu huanza kufifia.
Hatari kubwa si kwamba taasisi hizo hazipo. Hatari ni pale zinapokuwepo kwa jina, lakini zikapoteza kusudi la kuanzishwa kwake.
Mwanafalsafa wa Kifaransa Montesquieu aliwahi kueleza kwamba uhuru wa wananchi hulindwa pale mamlaka yanapowekewa mipaka na taasisi zinazoweza kusimamia na kuwajibisha kila mmoja. Wazo hilo ndilo lililozaa misingi ya mgawanyo wa madaraka katika demokrasia nyingi duniani. Taasisi zinaposhindwa kutekeleza wajibu huo, nguvu huanza kujikusanya mahali pamoja, na hapo ndipo hatari huanza.
Historia ya dunia inafundisha kuwa hakuna taifa lililoanguka ghafla. Mataifa mengi yalianguka baada ya wananchi kuanza kuzoea mambo yasiyo ya kawaida kana kwamba ndiyo hali ya kawaida. Dhuluma ilipoanza kuonekana kama utaratibu. Rushwa ilipoitwa ujanja. Ukimya ulipoitwa hekima. Kuhoji kukaitwa uadui. Na uwajibikaji ukaonekana kama tishio badala ya msingi wa uongozi bora.
Barani Afrika pia kuna masomo muhimu. Nchini Ghana, kipindi cha misukosuko ya kisiasa kilifuatiwa na juhudi za kuimarisha taasisi za uchaguzi, mahakama na utawala wa sheria. Leo, licha ya changamoto, nchi hiyo imekuwa mfano wa mabadiliko ya uongozi kupitia uchaguzi wa amani mara kadhaa. Zambia imeonyesha kwamba uchaguzi unaweza kusababisha kubadilishana madaraka kwa amani pale taasisi zinapoheshimu matokeo na wananchi wanapotumia kura badala ya nguvu. Malawi, baada ya Mahakama kubatilisha uchaguzi wa mwaka 2019 na kuamuru urudiwe, ilitoa mfano wa umuhimu wa mahakama zinazoweza kufanya maamuzi kwa uhuru ndani ya mfumo wa kikatiba.
Masomo haya hayamaanishi kuwa mataifa hayo hayana changamoto. Yanaonyesha kwamba taasisi zinazofanya kazi kwa mujibu wa sheria zinaweza kusaidia taifa kushughulikia migogoro bila kuvunja utaratibu wa kikatiba.
Hakuna taifa linalodumu kwa sababu ya mtu mmoja. Viongozi wote hupita. Vyama hubadilika. Lakini taifa hubaki. Ndiyo maana jambo la muhimu zaidi si nani yuko madarakani leo, bali kama taasisi zetu zitabaki imara hata baada ya viongozi wa leo kuondoka.
Wananchi wana wajibu mkubwa katika kulinda msingi huo. Wajibu huo unaanza kwa kuheshimu Katiba na sheria, kushiriki katika uchaguzi na michakato mingine ya kiraia, kufuatilia utendaji wa viongozi, kuuliza maswali kwa hoja na kwa amani, kukataa rushwa na matumizi mabaya ya madaraka, na kutetea haki za wengine hata wanapokuwa na tofauti za kisiasa. Demokrasia haiishi siku ya kupiga kura; hujengwa kila siku kupitia uwajibikaji na ushiriki wa wananchi.
Viongozi wa dini wanapaswa kubaki sauti ya dhamiri ya taifa. Kazi yao si kusifia wenye mamlaka wala kuwafuata wapinzani, bali kusimama upande wa haki, ukweli na utu wa kila binadamu. Waandishi wa habari wanapaswa kutafuta ukweli kwa weledi. Wanasheria wanapaswa kuilinda sheria. Wasomi wanapaswa kuelimisha jamii. Na viongozi wa umma wanapaswa kukumbuka kwamba mamlaka ni dhamana ya muda, si mali ya kudumu.
Uzalendo wa kweli haupimwi kwa kiwango cha kumsifu mtawala wala kwa ukubwa wa ukosoaji. Uzalendo wa kweli hupimwa kwa utayari wa kulinda misingi inayolifanya taifa lidumu: Katiba, utawala wa sheria, taasisi huru, haki, uwajibikaji na utu wa kila mwananchi.
Taifa huanza kupona pale wananchi wanapoamua kwamba hakuna aliye juu ya sheria, hakuna taasisi inayopaswa kuwa juu ya Katiba, na hakuna maslahi ya kisiasa yanayopaswa kuwa makubwa kuliko maslahi ya taifa.
Kumshambulia Msigwa kwa kuikimbia CCM kumetatuaje tatizo la Oktoba 29, 2025?
Je, kumjadili Msigwa mchana na usiku kumerudisha imani ya wafadhili waliogoma kutoa fedha?
Je, kumlaumu Msigwa kumeshusha bei ya mafuta na gharama za maisha?
Je, kumshambulia Msigwa kumezuia au kupunguza ufisadi unaolalamikiwa na wananchi?
Je, kumerudisha ajira, kuimarisha uchumi na kurejesha heshima ya Tanzania kimataifa?
Hakuna taifa linalotatua matatizo makubwa kwa kutafuta adui wa kisiasa wa kumlaumu. Matatizo ya taifa yanahitaji majibu ya sera, uwajibikaji na uongozi, si propaganda.
Badala ya kujadili kwa nini mtu alihama chama, swali muhimu zaidi ni:
Nini kifanyike kurejesha imani ya wawekezaji na wafadhili?
Nini kifanyike kupunguza gharama za maisha?
Nini kifanyike kupambana na ufisadi?
Nini kifanyike kuponya majeraha ya kisiasa na kujenga maridhiano ya kitaifa?
Historia haikumbuki sana waliotumia muda mwingi kuwashambulia watu; historia huwakumbuka waliotatua matatizo ya watu.
Matatizo ya Oktoba 29, 2025 na athari zake kwa taswira ya Tanzania na uhusiano na washirika wa maendeleo yameendelea kujadiliwa kimataifa.
Kama unampenda Mhe. Lissu na unachukizwa na kitendo cha Nduli Idd Amin Mama kuendelea kumshikilia Mhe. Lissu gerezani kwa kesi ya mchongo ya uhaini.
Basi tukutane barabarani Julai 7 #77Tunatoka
Kadiri miaka inavyokwenda, nimejifunza jambo moja muhimu sana: maisha ya bandia ni maisha ya gharama kubwa sana. Gharama yake si fedha tu, bali pia ni gharama ya kiroho, kihisia, kisiasa na hata kimahusiano.
Ukweli ni rahisi kuishi nao. Uongo, kwa upande mwingine, unahitaji matengenezo ya kila siku.
Mwanasiasa anapoanza kujenga umaarufu wa bandia, unyenyekevu wa kuigiza, utajiri wa kuonyesha, au picha ya mtu mkamilifu asiye na dosari, anajikuta akitumia nguvu nyingi kuilinda taswira hiyo. Uongo mmoja huzaa mwingine, na maigizo ya leo huzaa maigizo ya kesho. Mwishowe, mtu haishi tena maisha ya kawaida; anaishi maisha ya kisiasa kila dakika. Na hilo linachosha sana.
Tatizo kubwa la siasa za dunia yetu ni kwamba mara nyingi tunathamini zaidi muonekano kuliko uhalisia. Watu wanajikuta wakitaka kuonekana wenye nguvu kuliko walivyo, matajiri kuliko walivyo, na wenye ushawishi kuliko walivyo. Ndiyo maana wakati mwingine tunaona misafara mikubwa, sifa za kulipwa, propaganda na maisha ya kifahari kupita kiasi. Mara nyingi si kwa sababu watu wanafurahia hayo, bali kwa sababu wanaogopa kuonekana wa kawaida.
Lakini taswira inapokuwa kubwa, gharama ya kuilinda nayo huwa kubwa zaidi.
Wakati mwingine watu wanaonekana kucheka mbele ya kamera, lakini ndani wamejaa hofu, wasiwasi na upweke mkubwa. Hawajui tena nani anawapenda kwa dhati, nani anawaogopa, nani anawasifia kwa maslahi, na nani anasubiri siku ya kuanguka kwao.
Nafikiri moja ya gharama kubwa zaidi za maisha ya bandia ni kupoteza amani ya ndani. Mwanadamu hakuumbwa kuigiza maisha milele. Nafsi huchoka kubeba mtu ambaye si yeye halisi.
Ndiyo maana naamini kwamba uhalisia ni nafuu kuliko maigizo. Kiongozi wa kweli hahitaji kuigiza kila siku. Anaweza kukosea kama binadamu mwingine yeyote, lakini hahitaji kuishi kwa ajili ya kuwalazimisha watu waamini picha ambayo si ya kweli.
Na kuna jambo ambalo historia imenifundisha. Wakati mwingine mtu aliyekaa ndani ya msafara mkubwa, akiwa na walinzi na heshima zote za dunia, anaweza kukosa amani kuliko mtu anayepita pembeni kwa miguu.
Kwa sababu amani haitokani na ukubwa wa msafara, wala haitokani na ukubwa wa cheo. Amani hutokana na dhamiri safi, ukweli wa ndani, na kuishi maisha yanayofanana na wewe halisi.
Mwisho wa yote, watu hawatakumbuka sana ukubwa wa magari yetu, wala ukubwa wa majumba yetu. Watakumbuka kama tuliishi kwa ukweli, kama tulikuwa waaminifu kwa dhamiri zetu, na kama tulitumia nafasi tulizopewa kuwatumikia watu kwa uadilifu na hofu ya Mungu.
Kwa nini watawala huwa hawajifunzi kwa watawala waliopita?
Anaandika Rev Peter Simon Msigwa
Hili ni swali ambalo wanahistoria, wanafalsafa na wanateolojia wamekuwa wakijiuliza kwa karne nyingi. Mara nyingi si kwamba watawala hawajui historia; tatizo ni kwamba nguvu na mazingira yanayowazunguka huwafanya waamini kwamba wao ni tofauti na waliowaangulia.
Sababu kadhaa ni hizi:
1. Kila mtawala huamini “kwangu haitatokea”
Muammar Gaddafi, Saddam Hussein, na watawala wengi kabla yao waliona wengine wakianguka lakini waliamini mfumo wao ungeendelea milele. Madaraka hujenga hisia ya kutoshindwa.
2. Watu wa karibu huwaficha ukweli
Watawala wengi huzungukwa na watu wanaosema kile wanachotaka kusikia badala ya ukweli. Taratibu, sauti za kukosoa huzimwa na kiongozi huanza kuamini kwamba anapendwa na kila mtu.
3. Mafanikio ya awali huzaa kiburi
Kiongozi anapofanikiwa katika mambo kadhaa, anaweza kuanza kuamini kwamba kila anachofanya ni sahihi. Kiburi huanza kuchukua nafasi ya hekima.
4. Historia haisomwi kwa moyo wa kujifunza bali wa kujihesabia tofauti
Watawala wengi huangalia anguko la wengine na kusema:
“Walishindwa kwa sababu walifanya makosa fulani, mimi ni tofauti.”
Lakini kanuni za maadili, haki na uwajibikaji hubaki zilezile.
5. Hofu ya kupoteza madaraka
Kadiri mtu anavyokaa madarakani, ndivyo hofu ya kuyapoteza inavyoongezeka. Hofu hiyo humfanya aone wapinzani kama maadui, ukosoaji kama usaliti, na nguvu kama njia ya kujilinda.
6. Tatizo la dhamiri iliyonyamazishwa
Dietrich Bonhoeffer aliandika kwamba tatizo kubwa si uovu pekee, bali ujinga unaotokana na mfumo unaomfanya mtu kuacha kufikiri kwa dhamiri yake mwenyewe. Mtu mwenye mamlaka makubwa anaweza kuanza kuamini kwamba kwa sababu ana nguvu, basi ana haki.
7. Historia hujirudia kwa sababu binadamu hubaki vilevile
Teknolojia hubadilika, lakini tamaa ya madaraka, kiburi, hofu na sifa hubaki. Ndiyo maana mifumo mingi huanguka kwa sababu zilezile zilizowaangusha waliotangulia.
Kwa hiyo, swali si kwa nini watawala hawasomi historia, bali kwa nini binadamu akiwa na nguvu nyingi huwa na tabia ya kuamini kwamba sheria za historia hazimhusu.
Kama alivyoonya George Santayana:
“Wale wasiojifunza kutokana na historia, wamehukumiwa kuirudia.”
Na kama alivyoandika Lord Acton:
“Mamlaka yana tabia ya kuharibu, na mamlaka kamili huharibu kabisa.”
Ndiyo maana viongozi wenye hekima hawajifunzi tu kutokana na ushindi wao, bali hujifunza pia kutokana na makosa na anguko la waliowatangulia. Hekima ya kweli si kuamini kwamba wewe ni tofauti na historia, bali kutambua kwamba wewe pia unaweza kuwa sehemu yake.
‼️🚨HUYU NDO AWADHI JUMA HAJI AMBAE ALITOA ORDER YA ‘SHOOT TO KILL’ OKTOBA 29.‼️
Kwa msiomfahamu Awadhi Juma Haji yeye ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, yani Operesheni zote ambazo zinafanywa na Jeshi ya Polisi huyu ndo incharge Mkuu bila yeye kuidhinisha hakuna Operation inafanyika, huyu ndo Idd Amin Mama anamuandaa kuwa IGP baada ya Wambura.
Kama mtakumbuka kabla ya Oktoba 29, niliwahi kupost kuhusu uwepo wa Wanajeshi 500 wa Uganda ambao Idd Amin Mama aliwakodi kwa Mseven ili waje kutuuwa Oktoba 29, nikaweka na list ya majina feki ambayo walipewa, vyeo feki pamoja na Mikoa/Miji ambayo walipangiwa kwenda kuuwa Watanganyika siku ya Oktoba 29, 2025.
Sasa huyu Awadhi ndo ambae alikuwa anaratibu safari ya hao Wanajeshi wa Uganda tangu Wanatoka Uganda, wanapita border ya Mutukula huko Kagera mpaka wanafika Dar es salaam, yeye ndo aliwapangia hao Wanajeshi wa Uganda maeneo ya kwenda na walienda huko kabla ya Oktoba 29 so Watanganyika ambao mlikutana na Wauaji ambao walikuwa hawajui kiswahili ndo hao Waganda na aliyewapangia waje huko kwenu ni huyu Awadhi Juma.
Sasa turudi kwenye hoja ya msingi Oktoba 29, baada ya Maandamano kushika kasi kila kona ya Nchi, Serikali haram ya Nduli Idd Amin Mama ilizima mtandao, ikakata umeme sehemu kubwa ya Tanzania then IGP Wambura akatangaza hali ya hatari na kusema kwamba kufikia saa 12 jioni watu wote wawe majumbani kwao kwasababu kuanzia muda huo Jeshi la Polisi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama watakuwa barabarani kwa ‘KAZI MAALUM’
Kabla IGP Wambura hajatoa Tangazo lake tayari yeye na Awadhi Juma, Idd Amin Mama alikuwa keshawapa maelekezo ya kuuwa watu na Awadhi alikuwa ameshaweka standby vikosi vyote ambavyo walikuwa wameviandaa kwa ajili ya kuuwa Watu Oktoba 29.
Baada ya IGP Wambura kutoa hilo Tangazo lake haram, Awadhi Juma ndo akatoa order ya SHOOT TO KILL ambapo aliambia vikosi vyao vyote kwamba, kuanzia saa 12 jioni mtu yeyote ambae watamkuta barabani wapigeni risasi, ndipo vikosi vyao viliingia barabarani na kuanza kuuwa kwa risasi kila mtu ambae walimkuta barabarani bila kujali ni nan au anafanya nini, walipomaliza kuuwa watu barabarani wakaingia mpaka kwenye majumba ya watu na kuanza kuwafyatulia risasi.
Kuna Askari wanasema kwamba siku ya Oktoba 29, baada ya kufanya Operation ya kuuwa Watanganyika wenzetu, kuna baadhi ya Polisi waliogopa kuuwa so muda ulivofika wakurudi kwenye “MAKUTANO YAO” kwa ajili ya kujipanga na mashambulizi ya siku ya pili yani Oktoba 30, Awadhi na wasaidizi wake walikuwa wanakagua silaha, Askari ambao ilionekana wametumia risasi chache walipewa adhabu na ambao hawakutumia risasi hata moja wao waliwekwa lockup, walikuja kuachiwa baada ya Nduli Idd Amin Mama kujiapisha
Awadhi na vikosi alivokuwa anaviongoza, walifanya operation ya kuuwa Watanganyika kwa siku tano mfululizo, waliuwa Watanganyika zaidi ya elfu kumi, waliuwa asubuhi, waliuwa mchana, waliuwa usiku bila huruma, walifanya yote hayo kumlinda Nduli Idd Amin Mama ili aendelee kubaki madarakan bila kupigiwa kura na Wananchi.
Ile siku ya Oktoba 29, baada ya vikosi vyao kuuwa Watanganyika wenzetu, walipoona miili ya ndugu zetu imefurika kwenye Hospital zote, waliagiza wahudumu wa afya waliokuwepo zamu siku hiyo wasitoke kazini mpaka siku watakapomaliza operesheni yao na baada ya tangazo hilo kuna wahudumu wa afya walipokonywa simu zao lengo lilikuwa ni kudhibiti taarifa kuhusu majeruhi na idadi ya waliouwawa.
Baada ya miili kufurika kwenye Hospitals mpaka mingine wakakosa pakuiweka, usiku magari ya JWTZ yalikuwa yanapita kwenye Hospital za Serikali na kusomba miili ya ndugu zetu, waliiba maelfu ya miili ya Watanganyika na miili mingi ambayo walikuwa wanaiiba ni ile ambayo waliipiga risasi kichwani na tumboni kisha wakaenda kuizika kwenye Makaburi ya Halaiki kama mizoga.
Machi 2026, Awadhi Juma alifanya ziara ya kutembelea Mikoa yote ya Tanganyika na kuwapongeza maRPC kwa kazi waliyofanya Oktoba 29, yani aliwapongeza kwa kuuwa kwa risasi Watanganyika zaid ya elfu 10.
Leo majira ya mchana Polisi watano wakiwa na silaha za moto walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa CHASO Mkoa wa Mwanza AdvocateSailence Mwakasala na kumkamata kinguvu kisha wakaondoka nae.
Mpaka sasa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza wamegoma kusema kosa lake ni nini na wanamshikilia katika kituo kipi cha Polisi.
NB. Gari ambayo walitumia wakati wanamkamata ni namba T 113 DVU Toyota Hilux halafu mmoja wa hao Askari alikuwa amevaa sare za The Polisi.
#FreeSailenceMwakasala
KAMA HUKUPATA NAFASI KUSOMA
"Anaandika Baba Askofu Bagonza
YUDA AMECHOKOZWA; ASICHOKOZEKE❗️❗️❗️
Yuda wa Biblia alimsaliti Bwana Yesu. Siamini kama mleta hoja anamaanisha msalitiwa katika hoja yake ni sawa na Bwana Yesu!?!? Ipo siku tusiyoijua, “Yesu” huyu aliyefumbwa katika hoja hii, atafananishwa na “Mtume” asiyelinganishwa. Hapatatosha. Mleta hoja hajachagua vizuri maneno yake na mifano yake. NIMEMSAMEHE BURE.
Sakata hili lina mapichapicha sita ya hatari.
1. Msemaji aliwahi kuchokonoana na Rais wake huko kwao mpaka akajiuzuru. Mama yetu akamchukua, akamteua. Ina maana Rais yule na Mama yetu hawako shwari? Je Mama ni Yuda wa Rais yule kwa kuwa alimchukua mleta hoja?
2. Mleta hoja ni Mzanzibari, anamnanga Yuda Mtanganyika. Hii ni kero au ufa katika muungano? Alikosekana Mtanganyika wa kumrudi Yuda Mtanganyika?
3. Mleta hoja anasali Ijumaa; anamnanga anayesali Jumapili kwa kutumia picha ya (Yuda) anayeomba huruma makanisani. Tuseme katumwa na msikiti?!
4. Maneno yake yameingia kwenye Hansard. Bunge halikukanusha. Je ni bunge zima linamwita Makamu kuwa ni Yuda?
5. Naibu Spika alipomwongoza ajikite kwenye hoja, wabunge walipiga makofi. Walifurahia Naibu Spika kuingilia au walimshangilia mtoa hoja. Je makofi hayo ni mashangilio ya tumbili wa Kijaluo anayeshangilia pori linaloungua bila kuwaza atalala wapi usiku?.
6. Hoja imetolewa siku Rais ameondoka nchini na kwa mujibu wa katiba, Makamu ndiye Mkuu wa nchi wa zamu. Mtoa hoja anamaanisha hamtambui Makamu kama Mkuu wa nchi wa zamu?
Kwa vyovyote, kuna dalili mbaya. Matiti ya binti wa Kijaluo yakiishaota, hayafichiki na hayarudi nyuma.
7. Wakristo wanaamini usaliti wa Yuda ulileta wakovu. Bila usaliti, Yesu asingekufa. Bila kifo, asingefufuka; na bila kufufuka, wokovu usingepatikana. Hakuna wokovu bila usaliti. Waliookoka wameisaliti dhambi ili wawe huru. Mleta hoja kakosea. Hakuna Yuda na hakuna Yesu katika hoja yake. Zilikuwa ni saa za jioni; Dodoma mapito ni mengi, hatujui alipitia wapi kuja bungeni.
8. Kisiasa, CCM bila tishio la upinzani wa nje, inayumba. Tulishauri mapema sana Lisu aachiwe ili aiunganishe CCM, tukapuuzwa. Angeachiwa mapema, CCM ingeungana na kusahau tofauti zake za ndani ili kukabiliana na upinzani. Hivi sasa wapo wana CCM wanamtamani Lisu ili awasaidie kuona thamani ya umoja wa chama chao. Hamjachelewa.
9. Mama alikuja na “R” nne. Moja ya “R” hizo ni REFORMS, yaani mabadiliko. Lisu akamuunga mkono Mama kwa kusema “Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi” (NO REFORM, NO ELECTION). Akakamatwa kwa uhaini wakati aliunga mkono falsafa ya 4R! Mbadilishie mashtaka mseme alikosea kumuunga mkono Mama!
10. Wenye madaraka punguzeni nguvu, ongezeni hekima. Ruto alitumia nguvu, sasa ana nguvu lakini urais (Presidency) ni dhaifu. Kambarage alitumia nguvu na hasira Januari 30, 1984, Mpaka anaondoka duniani, jambo hilo lilimtesa. Trump alimnanga Pence hadharani, akaangushwa na Biden kwenye uchaguzi. Rais na Makamu hawatenganishwi kirahisi. Si mnatuimbia maridhiano!? Ridhianeni, wapambe tukose kazi.
Kama Yuda alichokoza; aliyechokozwa asichokozeke. Kama Yuda amechokozwa; asichokozeke.
Wajaluo bhana! Eti, hata anayepotea ana anakokwenda."
Tatizo kubwa la Tanzania leo si ukosefu wa wasuluhishi wa migogoro ya ndoa. Tatizo kubwa ni mifumo dhaifu ya utawala.
Wakati serikali inakabiliwa na tuhuma nzito za ukiukwaji wa haki za binadamu, rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa uwajibikaji, wananchi walitarajia kuona viongozi wakuu wakijikita katika kujenga taasisi imara na kurekebisha mifumo inayozalisha matatizo hayo.
Ni jambo jema kiongozi kusikiliza matatizo ya wananchi. Lakini nchi haiwezi kuendeshwa kwa kutatua kesi moja moja za watu.
Kiongozi anaweza kusuluhisha ndoa moja leo, lakini kama mfumo wa haki una matatizo, kesho kutakuwa na ndoa nyingine mia moja zenye migogoro.
Anaweza kusaidia mfanyabiashara mmoja leo, lakini kama mfumo wa rushwa haujabadilika, kesho wafanyabiashara elfu moja wataendelea kuteseka.
Anaweza kutatua mgogoro wa kiwanja kimoja leo, lakini kama taasisi za ardhi zinaendelea kuwa dhaifu, migogoro mingine elfu itaendelea kuzaliwa.
Tofauti kati ya mwanasiasa wa kawaida na mwanamageuzi ni kwamba mwanasiasa hushughulika na matokeo, lakini mwanamageuzi hushughulika na chanzo cha matatizo.
Rushwa si ugonjwa; ni dalili ya ugonjwa.
Ufisadi si tatizo la kwanza; ni matokeo ya tatizo kubwa zaidi.
Chanzo chake mara nyingi ni:
taasisi dhaifu,
ukosefu wa uwajibikaji,
ukosefu wa uwazi,
sheria kutotumika kwa usawa,
na mkusanyiko mkubwa wa madaraka sehemu moja.
Hapa ndipo tunapopata somo kubwa kutoka kwa Kanuni ya Jethro (Jethro Principle) katika Kutoka 18.
Musa alikuwa akihukumu kila kesi mwenyewe. Alisikiliza kila mgogoro, mkubwa na mdogo. Alikuwa akijaribu kuwa mahakama, polisi, msuluhishi na kiongozi kwa wakati mmoja.
Jethro alipofika alimwambia:
“Hili jambo unalolifanya si jema. Hakika utajichosha wewe na watu hawa walio pamoja nawe.”
Suluhisho la Jethro halikuwa kumsaidia Musa kusikiliza kesi nyingi zaidi.
Suluhisho lilikuwa kujenga mfumo.
Aliagiza wachaguliwe viongozi wa makumi, hamsini, mia na maelfu ili washughulikie mambo ya kawaida, huku Musa akibaki kushughulikia masuala makubwa ya kimkakati.
Kwa lugha ya kisasa, Jethro alikuwa anasema:
Kiongozi mkuu hafanikiwi kwa kufanya kila kitu mwenyewe. Hufanikiwa kwa kujenga taasisi zinazofanya kazi hata bila uwepo wake.
Tatizo la Afrika kwa ujumla si ukosefu wa viongozi wenye nguvu.
Tatizo ni ukosefu wa mifumo yenye nguvu.
Nchi nyingi zimejenga viongozi wakubwa kuliko taasisi zao.
Matokeo yake ni kwamba kila jambo linasubiri Rais, Waziri Mkuu, Waziri au Mkuu wa Mkoa.
Barabara inasubiri maelekezo ya juu.
Mgogoro wa ardhi unasubiri maelekezo ya juu.
Hata migogoro ya familia wakati mwingine inasubiri maelekezo ya juu.
Hiyo si dalili ya uongozi imara.
Ni dalili ya taasisi dhaifu.
Katika taifa lenye mifumo imara, mwananchi hapaswi kusafiri mamia ya kilomita kwenda kulalamikia Waziri Mkuu ili kupata haki yake.
Anapaswa kuipata haki hiyo katika ngazi ya kijiji, kata, wilaya au mahakama kupitia taasisi zinazofanya kazi kwa ufanisi.
Kazi ya viongozi wakuu wa taifa si kuwa wasuluhishi wa kila mgogoro.
Kazi yao ni kuhakikisha kuna mfumo unaozuia migogoro mingi kutokea na unaotatua migogoro inayotokea kwa haki na kwa haraka.
Wananchi hawahitaji tu viongozi wanaoweza kusuluhisha matatizo ya watu binafsi. Wanahitaji viongozi wanaoweza kujenga mifumo ambayo itafanya matatizo hayo yasitokee kwa kiwango kikubwa.
Historia haikumbuki viongozi waliotatua matatizo ya mtu mmoja mmoja. Historia huwakumbuka viongozi waliojenga taasisi imara, waliosimamia haki, na waliobadilisha mfumo kiasi kwamba hata baada ya wao kuondoka madarakani taifa linaendelea kusimama.
Kwa sababu mwisho wa siku, taifa haliendelezwi na uwezo wa viongozi wake kufanya kila kitu. Taifa huendelezwa na uwezo wa mifumo yake kufanya kazi hata viongozi hao wanapokuwa hawapo.
Ukimtukuza mtu kuliko mfumo, utapata mashujaa wachache na matatizo mengi.
Ukijenga mfumo kuliko mtu, utapata taifa imara na maendeleo ya kudumu.
Katika demokrasia:
Mahakama ni kubwa kuliko Jaji Mkuu.
Bunge ni kubwa kuliko Spika.
Taifa ni kubwa kuliko Rais.
Katiba ni kubwa kuliko chama tawala.
Hii ni kwa sababu taasisi zinapaswa kudumu, wakati viongozi ni wa muda.
1. TAIFA NI KUBWA KULIKO RAIS
Rais ni kiongozi wa muda.
Taifa ni la kudumu.
Rais anaweza kukaa madarakani miaka 5, 10 au 20.
Lakini taifa linaendelea kuwepo kabla yake na baada yake.
Mfano:
United States imekuwa na marais wengi sana.
Wamekuja:
Ronald Reagan
Bill Clinton
Barack Obama
Donald Trump
Lakini Marekani imebaki kuwa Marekani.
Rais ni mtumishi wa taifa.
Taifa si mali ya Rais.
Ndiyo maana katika demokrasia, kumpinga Rais si sawa na kulichukia taifa.
Na kumuunga mkono Rais si sawa na kuwa mzalendo.
Uzalendo ni kuipenda nchi hata pale unapokosoa serikali.
2. SERIKALI SI TAIFA
Hili ndilo eneo ambalo watu wengi huchanganyikiwa.
Serikali ni chombo kinachosimamia nchi kwa kipindi fulani.
Taifa ni wananchi wote pamoja na historia, ardhi, taasisi na mustakabali wao.
Kwa mfano:
Leo serikali inaweza kubadilika.
Lakini:
Tanzania inabaki Tanzania.
Bendera inabaki ile ile.
Wananchi wanabaki wale wale.
Historia inabaki ile ile.
Kwa hiyo:
Kuikosoa serikali si kuisaliti nchi.
Na:
Kuisifu serikali si lazima iwe kuipenda nchi.
Swali muhimu ni:
“Je jambo hili linafaidisha taifa?”
si “Je jambo hili linaifurahisha serikali?”
3. CHAMA TAWALA SI SAWA NA NCHI
Hili ni somo muhimu sana kwa Afrika.
Katika demokrasia:
Chama tawala ni mshindi wa uchaguzi.
Hakimiliki taifa. Hakimiliki serikali milele.
Hakimiliki uzalendo.
Taifa ni mali ya:
waliokichagua chama tawala,
wasiokichagua chama tawala,
na hata wale ambao hawakupiga kura.
Ndiyo maana katika nchi zilizoendelea kisiasa:
Ukikosoa chama tawala huonekani adui wa taifa.
Unaonekana sehemu ya demokrasia.
Tatizo linaanza pale chama tawala kinapoanza kuonekana kama taifa lenyewe. Hapo demokrasia huanza kudhoofika.
4. KATIBA NI KUBWA KULIKO CHAMA TAWALA
Katiba ndiyo mkataba mkuu wa taifa.
Katiba ndiyo inayotoa mamlaka kwa:
Rais, Bunge Mahakama.
Sio Rais anayeipa Katiba nguvu.
Ni Katiba ndiyo inayompa Rais nguvu.
Sio chama tawala kinachounda taifa.
Ni Katiba ndiyo inayoweka sheria za namna taifa litakavyoendeshwa.
Katika demokrasia iliyokomaa:
Kama chama tawala kinataka jambo ambalo Katiba hairuhusu,
Katiba ndiyo hushinda.
Kwa sababu Katiba inawakilisha taifa lote.
Chama kinawakilisha wanachama wake.
5. BUNGE NI KUBWA KULIKO SPIKA
Spika ni kiongozi wa muda.
Lakini Bunge ni taasisi ya kudumu.
Leo kuna Spika mmoja.
Kesho atakuwepo mwingine.
Lakini Bunge linaendelea kuwepo.
Hii ndiyo sababu taasisi ni muhimu kuliko watu.
Mtu anaweza kuondoka.
Taasisi inapaswa kubaki imara.
6. MAHAKAMA NI KUBWA KULIKO JAJI MKUU
Jaji Mkuu ni mtumishi wa Mahakama.
Sio Mahakama mali ya Jaji Mkuu.
Kesho Jaji Mkuu akistaafu:
Mahakama inaendelea.
Hii ndiyo maana ya utawala wa sheria.
Sheria inapaswa kuwa kubwa kuliko watu wanaozisimamia.
TATIZO KUBWA AFRIKA
Katika nchi nyingi za Afrika watu hufikiri hivi:
Chama = Taifa
Serikali = Taifa
Rais = Taifa
Kukosoa Serikali = Kuisaliti nchi
Hiyo ndiyo sababu mjadala wa kisiasa huwa mgumu.
Kwa sababu watu wanafikiri wanalinda taifa wakati mara nyingi wanakuwa wanalinda serikali au chama.
Lakini katika demokrasia yenye afya:
Taifa ni kubwa kuliko serikali.
Serikali ni kubwa kuliko chama.
Katiba ni kubwa kuliko serikali.
Sheria ni kubwa kuliko viongozi.
Dhamira ni kubwa kuliko utii wa kipofu.
Kwa lugha rahisi sana
Ukiniuliza tofauti kati ya nchi, taifa na serikali ningesema:
Nchi ni ardhi, mipaka na mamlaka yake.
Taifa ni watu wake, historia yao, utamaduni wao, taasisi zao na mustakabali wao.
Serikali ni timu ya muda iliyopewa jukumu la kuendesha taifa kwa kipindi fulani.
Ndiyo maana unaweza kubadilisha serikali bila kubadilisha taifa.
Lakini ukiharibu taifa, hata serikali nzuri haiwezi kulirudisha kwa urahisi.
Kwa hiyo kiongozi wa kweli hapaswi kuuliza:
“Je hili linaisaidia serikali?”
Bali: “Je hili linaimarisha taifa, taasisi zake, na vizazi vijavyo?
Kwa finishing aliyofanya msomi @TitoMagoti kwa yule kikatuni kwa heshima tumpe 👇🏻
Retweet 1K & Like 2K kabla ujalala ewe mpenda haki katika taifa letu Tanganyiaka #freetundulissu ✌️✊
Suala linalohusu na/au kuhatarisha maisha ya watu lazima tulipe umakini stahiki.
Propaganda ya waandamanaji kulipwa na Ford Foundation ni uongo wenye hatari.
Ulikuwa mkakati wa dola kujisafisha dhidi ya mauwaji.
Madenge, kwa kujua, alitumika kusambaza propaganda hiyo.
🧵🧵
Leo #MariaSpaces tunajadili: Kimeumana CCM - vikwazo, nguvu ya umma #FreeTunduLissu
Tunaona milio imeanza kutoka mafedhuli wauaji wakiongelea masuala ya vikwazo zitakazo waathiri binafsi
Nguvu ya umma inaelekea kushinda huku CCM wakihaha
#FreeTunduLissu lini? Leo saa 2 uck
MADENGE TUNAOMBA MAJIBU YA MASWALI HAYA NI VERY LOGICAL
Kwenye space ni vurugu tu hakukuwa na kuelewana @rollymsouth maswali yangu ntayaweka hapa hata ambao hawakuwa kwa space ile ulipata nafasi yajibu
1. Baada ya tweet ile nakumbuka ulisema utatoa ufafanuzi ambao umetoa leo Lakin wengi wanasema hawajaelewa, fafanua zaidi kwanini hata baada ya tweet uli kaa kimya sana ? Kama umejitenga fulan na harakati au kusema Kama awali!
2. Umesema kuwa una urafiki na watawala kwa mambo nje ya siasa! Hatukatazi maana na sisi tunao Ila je umetumia influence yako kufikisha ujumbe kuwa watanzania wanaumia
3. Kwakuwa Tweet Yako inatumika kama ku legalize kilichotokea 29/10/2025 Je kwanini wanapoendelea kuitumia usitoe special note kuwa tweet yako inatumika vibaya Hiyo note uka I pin kabisa ?? Kwamba hata akina @mwigulunchemba1 wanaoitumia au SERIKALI wanaoitumia uwaonye kwamba dhamira ya tweet ile sivyo inavyotumika?
4. Kuna dogo anasema ulienda Dodoma kukutana na mkubwa mmoja huko @munyamambogo , na analalamika mmemshusha space asiendelee kuongea japo umekanusha , je huyo dogo akileta ushahidi utakosoa?
5. Umesema ile tweet ya kuwashukuru ford ilikuwa ni wazo umepewa na Jamaa wa South Africa mwenye followers wachache ili angalau ford washukuriwe kwa kusaidia harakati, nawe uka tweet bila kuwaza Mara mbili madhara yake! Je (A) unaweza tupa handle ya account Hiyo? (B) unaweza ku share ujumbe huo kwa ku screenshot akiomba u post? Ili tuone maudhui na tarehe husika ?
6. Wafuasi wengi wa Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA mbowe walipinga msimamo wa Lissu wa No reforms na No election! Nawe ulikuwa mmoja wa wafuasi wake, na wakawa na wivu zaidi baada ya kuona kauli ile wananchi wameipokea na Uchaguzi haukufanyika, na wengine wako CHAUMMA wanasema CHADEMA ndo wahusika wa vurugu zile, huoni nawe unaweza unganishwa na mitazamo ya kina Yerico kwamba ulitweet vile kufifisha maana ya wananchi kudai haki yao Kikatiba? Wenda nawe hukutaka suala la wananchi kufanikiwa?
NAULIZA MASWALI YA MSINGI
TUNAOMBA MAJIBU
PLZ MNAO COMMENT ULIZENI MENGINE,
Watanzania tusikubali wauwaji wakajificha nyuma ya neno sovereignty ili kukwepa accountability ya mauaji ya October 29. TUSIKUBALI WAUAJI WAKABADILI NARRATIVE YA OCTOBER 29…
NI LAZMA IANZE KAMPENI KABAMBE. LAZMA ATOKEE MTU HUKO TITKOK/ISTAGRAM/FACEBOOK AWAONGOZE WATANZANIA KWENYE KAMPENI YA KUMUOMBA DONALD TRUMP AINGILIE TENA KWA KISHINDO KIKUBWA ISSUE YA MAUAJI YA OCTOBER 29…….