Nguvu ya kusini, Makamu mwenyekiti @HecheJohn akizindua misingi ya Chama. Baadaye atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa hadhara kilwa kivinje mkoani Lindi. Wakazi wa kilwa kivinje karibuni kwenye mkutano wa hadhara!
Bwana Sisty Nyahoza, amefika Makao makuu ya Chama, Jengo la Edwin Mtei, Mikocheni Dar Es salaam.
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa inafanya ziara ya kutembelea vyama vya siasa.
JESHI LA POLISI LIMEVAMIA NYUMBANI KWA MBYELLA (ANAYEUZA NGUO NA VIFAA VYA CHADEMA NA KUONDOKA NA TSHIRT, KOFIA, NGUO NA BENDERA ZA CHADEMA:
Nimepata taarifa kuwa usiku wa manane, Jeshi la Polisi limevamia nyumbani kwa Mbyella wakidai wanamtafuta kwa kosa la kutengeneza Tshirt zenye maandishi “free Tundu Lissu”
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, Mbyella mwenyewe hakuwepo nyumbani na Polisi walifanya upekuzi na baada ya kumkosa waliondoka kwa muda. Baadaye walirejea na Gari aina ya Fuso na kubeba nguo zote na vifaa vyenye nembo ya chadema ikiwemo Bendera za Chadema ambazo huwa anauza na kuondoka na mali hizo bila kutoa sababu zaidi.
Kwa mujibu wa mke wa Mbyella (anayeuza nguo na vifaa vya chama) nyumbani kwao kuna duka la kuuza vifaa hivyo ambavyo Polisi wameondoka navyo vyote.
Tunafuatilia kufahamu sababu hasa ya kuvamia nyumbani hapo na kuleta taharuki kwa mtu ambaye hata kama wangemhitaji Polisi, wangempatia wito na angefika kituoni kama Polisi walikuwa na jambo na Mbyella. Kuuza vifaa vya chama kama nguo, kofia, Bendera siyo kosa kisheria.
Kijiji cha Ndaga, Kata ya Ndato, wilaya ya Rungwe Mbeya. Huu ni mkutano wa kijiji tu. Halafu anatokea mtu eti anawaza kusitisha usajili wa Chama hiki. Akha ahaaaaaaaa!
MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKIKIZA KESI DHIDI YA Mhe LISSU, June 11,2026:
Mahakama ya Rufaa itasikiliza maombi ya Mkurugenzi wa mashitaka nchini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Tundu Antipas Lissu Alhamisi ya tarehe 11 June, 2026.
Haya ni yale maombi ya Jamhuri ambayo waliyapeleka baada ya Mahakama kuu kukubali pingamizi la Mhe Lissu dhidi ya maombi ya Serikali kuraka kuongeza maelezo ya nyongeza ya shahidi.
Jopo la Majaji 3 wa Mahakama ya Rufaa wamepangwa ambao ni, Mhe Mwalija, Mhe Jaji Muruke na Mhe Jaji Khamisi.
Hakikisha ujumbe huu umewafikia kwa wingi marafiki wa Demokrasia na Haki.
MUNGU NI MWEMA, MAHAKA KUU IMEKUBALI PINGAMIZI LA MAWAKILI WA CHADEMA- KESI YA MGAWSNYO WA MALINZA CHAMA IMEFUTWA RASMI LEO
Mahakama kuu ya Tanzania, Masijala ya Dar es salaam leo imetoa uamuzi kufuatia pingamizi la mawakili wa Chama waliloweka wakidai hati ya madai haikuonrsha lini mgogoro ulianza jambo ambo ni kinyume cha Sheria.
Awali pingamizi hili lilipowekwa Jaji Mwanga aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo alidai kwamba, wakati kesi ikiendelea itajulikana mbele ya safari ni lini hasa madai yalianza.
Ikumbukwe kwamba, Mahakama ya Rufaa baada ya kusikiliza hoja za majereo ilielekeza mahakama kuu ikaamue hoja hiyo mbele ya jaji mwingine ambapo kesi hiyo ilipangwa mbele ya Mhe Jaji D. Ngunyale.
Leo, Mahakama imetoa uamuzi na kukubaliana na hoja zetu kwamba kitendo cha waleta madai kushindwa kuonesha lini hasa madai yao yalianza kinainyima mahakama nafasi ya kujiridhisha kama kweli inayo mamlaka ya kusikiliza madai husika.
Kufuatia hali hiyo, kesi hiyo namba 8323/2025 imefutwa rasmi leo.
Nawashukuru marafiki wote ambao mumelia nasi kama chama kwa namna moja ama nyingine, hakika leo tumshukuru Mungu kwa pamoja.
MAHAKAMA KUU YAMZUIA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA CHADEMA:
Mtakumbuka barua ya Msajili wa vyama vya siasa kwa CHADEMA iliyotutaka kujieleza huku akitishia kufuta uwakili wa Chama kwa muda ama kukiroza faini chama.
Chama kilichukua hatua kadhaa, mosi tulikubaliana kujibu barua ya mashahidi wa vyama vya siasa kama ambavyo umma mlijulishwa.
Pili, Chama kilichukua hatua ya kwenda mahakamani kuomba ruhusa (leave) ili chama kiweze kuomba amri ya kumzuia msajili wa vyama vya siasa kuchukua hatua dhidi ya Chama.
Chama Kilifungua shauri, miscellaneous cause no 12812/2026 Mahakama kuu ya Tanzania, Masijala ya Manyara, Babati, kwa hati ya dharura.
Chama kiliomba, Amri ya upande mmoja kwanza, kwa kuwa msajili angechukua hatua. Baada ya kusikiliza hoja za upande wetu, Jaji I. C. MUGETA wa Mahakama kuu Masijala ya Manyara ametoa zuio la muda dhidi ya Msajili wa vyama vya siasa kuchukua hatua yoyote kwa chadema hadi Maombi ya CHADEMA yatakapo sikilizwa.
LISSU MAHAKAMANI TAREHE 25/05/2026:
Jumatatu ya tarehe 25.05.2026 Mhe Lissu atafikishwa Mahakama kuu Masijala ya Dar es salaam ambapo Maombi namba 12194/2026 ya kuunganishwa kwenye kesi ya mgawanyo wa mali yatatajwa.
Maombi hayo ya Mwenyekiti Taifa, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) dhidi ya Said Issa Mohamed na wenzake 4 yatatajwa tarehe 25.05.2026 saa mbili na dakika 45 mbele ya Mhe Jaji D. Ngunyale.
Mhe Lissu ameshapata wito huko Gerezani. Wananchi walioko Dar Es Salaamu na maeneo ya jirani, tukutane Mahakama kuu Jumatatu, mapema sana, Mwenyekiti wetu atakuwa pale.
Kaka @daviddjumbe aliyekuwa jana. Watekaji walimfunga pingu na akaumizwa kama inavyoonekana hapa. Amepelekwa Polisi kufunguliwa hizo pingu. David Djumbe ni Msaidizi wa @TunduALissu . Taarifa zaidi zitafuata.
KESI YA JINAI DHIDI YA MWANACHAMA WA CHADEMA LUCY SHAYO KUENDELEA KESHO MOROGORO:
Morogoro nako, kesi ya Jinai namba 22666/2025, inayomkabili Lucy simon Shayo itaendelea kwa upande wa Jamhuri kuleta shahidi wao wa pili.
Nawaomba marafiki wa haki pia kufika mahakama ya wilaya ya Morogoro kusikiliza mashahidi wa Jamhuri na maswali ya Dodoso.
KESI DHIDI YA CHADEMA, MAHAKAMA KUU KUTOA UAMUZI (RULING) KESHO TAREHE 20/05/2026:
Kesho, Mahakama kuu, Masijala ya Dar es salaam inatarajiwa kutoa uamuzi mdogo dhidi ya pingamizi la mawakili wa Chama kwenye kesi ya Madai ya Said Issa Mohamed na wenzake dhidi ya Bodi ya wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.
Itakumbukwa kwamba, Mahakama kuu baada ya kusikiliza pingamizi hilo, Iliana kutoa uamuzi kesho kuanzia saa sita mchana.
Endapo Mahakama kuu itaona pingamizi hili lina mashiko basi kesi hiyo itakuwa imeshia hapo, na kama ikitupilia mbali pingamizi basi shauri hilo litaendelea.
Wananchi mnaopenda haki na marafiki wa Demokrasia tukutane Mahakama kuu.