Professional in Automobile Engineer || Fleet Manager || Entrepreneur ||project manager || Graphic Designer || Never loose hope || Do not give up ||You can do it
6 REASON WHY YOU SHOULD TRUST GOD:
1. He knows you by Name
2. He will fight for you
3. He thinks about you
4. He has plans for you
5. He is your refugee
6. He is always with you
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 112
Anaendelea Wakili wa Serikali Thawabu Issa
Hii Meta Data ni nini hasa?
Meta Data ni Data about Data. Yaani picha mjongeo ni Data ndani ya Picha mjongeo kuna Data nyingine ambazo ni taarifa. Hzio taarifa zinaweza kuwa tarehe, jina na kadhalika. Taarifa hizo mjongeo zilizopo kwenye picha mjongeo ndio tunaita Meta Data.
Anasimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali huyu Baba ni mstaarabu kwakweli. Yeye muonekano wake hana nouma. Anaongea kistaarabu sana. Hana arrogance yoyote. Kwa kumuona tu haoneshi kuwa kisirani kama mawakili wengine wa Serikali.
Anasema kwa sasa ni saa saba naomba tupate break watu wakapate Chakula.
Majaji wanaandika kidogo.
Wanamuuliza Mshitakiwa. Anasema sina pingamizi.
Wanaandika kidogo. Wanasema sasa twendeni break tukutane baada ya lisaa limoja kutoka sasa. Tumeishia hapo kwa sasa. Tukirudi Shahidi ataendeelea kutoa ushahidi wake kwa maana ya EXAMINATION IN CHIEF ITAENDELEA.
Kumbuka jina la Shahidi ni SAMWEL ELIBARIKI KAAYA alkiongozwa na Wakili wa Serikali Thawabu Issa.
Tukutane baadae kidogo.
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 109
Katuga: Uliulizwa kuhusu suala la Notebook kama hiyo notebook umeileta. Je kwanini hujaileta.
Lissu anasimama napinga hilo swali la sikufika huko hakutoa sababu za kwanini hakuileta.
Katuga: Mhe. Jaji alimzuia shahidi asiendelee kutoa maelezo kwanini hakuleta.
Jaji: Hayo mambo ni mapya hatuwezi kukuruhusu. Uliza swali lingine.
Katuga: uliulizwa nani aliyechapisha ulisema ni wewe siku nyingine ukasema sifahamu na leo pia umesema ni yeye kupitia Jambo Tv. Sasa sisi tunataka ufafanuzi
Kaaya: Kupitia Jambo TV alichapisha maudhui yaliyopo kwenye hati ya mashitaka kitendo cha yeye kuwaalika wanahabari na kutoa maudhui yale ni tayari alikuwa ameridhia kutoa maudhui yale mtandoani.
Katuga kila baada ya swali moja anafanya vikao na mawakili wenzake sita hapa Mahakamani. Hii Re Examination yao imekuwa ngumu sana aiseee. Wanahangaika halafu ni kama shahidi anawajibu namna ambavyo walikuwa hawatarajii. Hawayafurahii majibu ya shahidi wao kabisa.
Katuga: Waheshimiwa Majaji naomba tuishie hapa kwenye maswali ya ufafanuzi kwa shahidi wetu. 😂
Hadi majaji wamecheka hapa kimya kimya. Hii re examination ilikuwa ngumu sana. Mhe. Lissu kamshona shahidi hadi upande wa Jamhuri wameshindwa kujua Shahidi atoe ufafanuzi wa jambo gani.😀
Jaji shahidi unaruhusiwa kuondoka. Tunakushukuru kwa ushahidi wako.
Insp. John Kaaya amejaribu kutoka kwa speed kidogo amejikwaa hapa kwenye kiti ametaka kumdondokea Askofu Mwamakula maana amekaa nae karibu na kizimba pale. 😂
Watu wamecheka inaonekana huyu Polisi alikuwa amechoka sana hii kazi kwakweli. ametoka kama haamini kweli amemaliza huu msala.
Amesima Renatus Mkude anasema tunae Shahidi wa tatu ambae ni SAMWEL ELIBARIKI KAAYA.
Jaji sasa huyu shahidi nae aje tuendelee.
Ananingia hapa Askari Mfupi wa kimo, ana kipara na ndevu nyinginyingi kidogo ambazo hazina afya zile ndevu kipilipili.
Jaji unaitwa nani?
Naitwa Samwel Elibariki Kaaya.
Mkaguzi wa Jeshi la Polisi.
Anaangalia kwa chini chini kwa kumuangalia tu muonekano wake inaonekana ana roho ngumu sana.
Anasema ana miaka 39.
Dini yangu ni Mkristo.
Anapelekewa Biblia aweze kuapa.
Anaishika mkono wa Kulia na amenyanyua juu.
Naapa ushahidi nitakaoutoa ni wakweli ewe Mwenyezi Mungu nisaidie.
Renatus Mkude anasimama naomba aongozwe na Thawabu Issa Wakili wa Serikali.
Huyu Thawabu Issa Wakili wa Serikali ndo yule alijifanya kurusha ngumi juzi kati anajikuta Rashid Matumla.
Amesimama ana kipara kama cha ushahidi.
Thawabu: Uongee kwa Sauti shahidi.
Jaji: Na wewe Wakili ongeza sauti sasa.
Thawabu: Kitengo gani upo?
Samwel Kaaya: Kitengo cha picha Kamisheni ya Uchunguzi sayansi jinai.
Sasa I tabidi huyu Shahidi nimuite Samweli maana na yeye ni Kaaya kama aliyetoka.😂
Thawabu: Kinajihusisha na nini kitendo hicho.
Samwel: Kitengo hicho kinajihusisha upigaji picha wa matukio mbalimbali lakini pia kurekodi matukio mbalimbali ya uhalifu. Kurekodi picha mjongeo za watuhumiwa wa uhalifu.
Thawabu: Upo kama nani kitengoni hapo?
Samwel: Niko kama mtaalamu wa picha baada ya kuteuliwa na DPP na kutangazwa na gazette la serikali GN. No. 745/2022.
Thawabu: Majukumu yako ni nini?
Samwel: Kupiga picha, kurekodi matukio ya uhalifu, kufanya uchunguzi wa picha mbalimbali kwa maana ya picha mjongeo na mnato.
Elimu yangu imegawanyika katika makundi mawili.
Elimu ya Kipolisi mwaka 2013/2014 nilihudhuria mafunzo ya awali ya Polisi. Recruit Course chuo cha Polisi Moshi CCP. Na mwaka 2014 nilimaliza na kutunukiwa Certificate of Competence.
Huko CCP Moshi nilijifunza criminal Laws, Evidence Law, Criminal Procedure, Bionnet, Parade Training, Parade la kutuliza ghasia, Self defense kwa maana ya Judo na Karate na Medani za Kivita.
Thawabu: Ulitunukiwa nini?
Samwel: Cheti cha Umahiri.
Thawabu: Kingine nini?
Samwel: Nilipata cheo cha awali cha Police Constable.
Part 110 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 107
Mhe. Lissu: Uchaguzi wa 2019 Serikali za mitaa CCM ilipata asilimia 98 ya wenyeviti wa Vijiji?
Kaaya: Sina Kumbukumbu
Mhe. Lissu: Je unafahamu uchaguzi mkuu wa 2020 ndio ulikuwa na wagombea wengi wa ubunge kuenguliwa kuliko chaguzi yoyote toka uchaguzi uanze?
Kaaya: Ukikosa sifa unaenguliwa tu.
Mhe. Lissu: Wewe ni fundi viyoyozi mambo ya sifa unayajulia wapi? Haya jibu swali langu.
Kaaya: Sikuwahi kufanya huo utafiti.
Mhe.Lissu: Kwamba wagombea 63 kati ya 244 walienguliwa wa ubunge?
Kaaya: Sijawahi kuwa mwanaCHADEMA.
Mhe. Lissu : Hata magazeti husomi ndugu yangu?
Kaaya: Sifahamu mimi.
Mhe. Lissu: wagombea wa udiwani 1150 kati ya 3900 walienguliwa mwaka 2020 unafahamu?
Kaaya: Sina takwimu mimi. Sijui.
Mhe. Lissu: Wagombea wa CCM 872 wa udiwani walipita bila kupingwa kutokana na kuenguliwa kwa wapinzani kwa mujibu wa taarifa rasmi ya tume?
Kaaya: Sijawahi kuisoma hiyo taarifa.
Kaaya: Waheshimiwa Majaji mimi nilisikia wagombea walipita bila kupingwa lakini idadi ya 28 sikumbuki.
Mhe. Lissu: Mimi nasoma ndio maana najua walikuwa 28 wewe unatengeneza Viyoyozi.
Kaaya: Mimi ni askari Polisi sio fundi viyoyozi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo hukusema hapa kuwa umesomea Air Condition? wewe ndio ulituambia haya mambo ya viyoyozi au nani alituletea?
Kaaya: Nilisema basi yaishe.
Mhe. Lissu: Kwahiyo toka 1995 hakuna mgombea hata mmoja wa CCM amewahi kuenguliwa kwa kukosa sifa?
Kaaya: Unaweza kuwa sahihi.
Mhe. Lissu: Waangalizi wa AU wa uchaguzi umewahi kuwasikia? AU election expert mission walitoa ripoti inayolalamikia kuenguliwa kwa wapinzani?
Kaaya: Nimewasikia lakini ripoti sikuisikia.
Mhe. Lissu: Je jumuiya ya Ulaya walituma EU election observation mission walituma waangalizi pia na kulalamikia kuenguliwa kwa wapinzani?
Kaaya: Silijui kiukweli.
Mhe. Lissu: Ongeza sauti basi unamnong'oneza nani?
Kaaya: Sijui
Mhe. Lissu: Je waangalizi kutoka jumuiya ya madola ambao ni Commonwealth observer group walitoa ripoti kulalamikia vitendo vya kuengua wapinzani?
Kaaya: Kweli.
Mhe. Lissu: Watizamaji wa Umoja wa Afrika walipendekeza kuwa serikali iondoe vikwazo vya kiuchaguzi kabla ya uchaguzi wa 2025?
Kaaya: Sina uhakika kabisa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama unafahamu mashirika ya kiraia walituma waangalizi Tanzania?
Kaaya: Walitumwa kwenda wapi?
Mhe. Lissu: Kuja Tanzania.
Kaaya: Basi msemaji wa Serikali anazo hizo taarifa.
Mhe. Lissu: Msemaji wa Serikali ni shahidi namba ngapi?
Kaaya: Sijui
Mhe. Lissu: Shahidi hapa ni wewe jibu swali langu.
Kaaya: Sijui.
Mhe. Lissu: Sasa unajua watizamaji wa ndani pia wa Uchaguzi huu wapo nao wamekuwa wakitizama uchaguzi miaka yote wanaitwa Tanzania Election Monitoring Committee ikijumuisha viongozi wa dini na chuo kikuu cha Dar es salaam (TEMCO)?
Kaaya: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Je umewahi kusoma ripoti ya hao TEMCO hata moja?
Kaaya: Sijawahi kuziona hata kwa sura wala kuzisikia.
Mhe.Lissu: so huwezi kufahamu mashirika haya kuwa nayo yamelalamikiwa mfumo wa uchaguzi na kuondolewa kwa wapinzani?
Kaaya: Sifahamu na sio majukumu yangu.
Mhe. Lissu: Sasa mimi kulalamikia uchaguzi unasema nasema uongo kwanini wakati huna unalojua?
Kaaya: Kusema Rais ndio niliona kuna shida.
Mhe.Lissu: Uchaguzi wa mwaka huu mgombea Urais wa ACT Wazalendo ameenguliwa na Tume ya Uchaguzi?
Kaaya: Hajakidhi vigezo.
Mhe. Lissu: Kaenguliwa na tume au hajaenguliwa?
Kaaya: Kaenguliwa na tume kweli.
Mhe. Lissu: Je Mwenyekiti wa Tume na Majaji waliokataa kesi jana wote si wateuliwa wa Rais?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: sasa ulitegemea Mpina apate haki kutoka wapi kama wote aliokuwa anategemea wampe haki ni wateule wa Rais?
Kaaya: Ingekuwa ngumu sana kiukweli.
Part 108 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 16, 2025
Jana tuliishia part 105 so leo tunaendelea na-;
Part 106
Muda huu ni saa tatu asubuhi.
Tumefika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es salaam.
Hali ya Mahakama ni nzuri.
Tunawashuhudia Waandishi wakichukua picha mgando na mnato kwa watu mbalimbali waliopo hapa Mahakamani.
Askari Magereza wale wa Kikosi Maalum yaani KM wako hapa ndani ya Chumba cha Mahakama wanazunguka zunguka kama wanakagua lindo vile.
Wasaidizi wawili wa Majaji tunawaona wako hapo mbele, Mwanamke mmoja na Mwanaume Mmoja kwa wasiofahamu hawa wanaoitwa Wasaidizi wa Majaji kitaaluma ni Mahakimu Wakazi.
Cheo chao ni sawa na Mahakimu waliopo Kisutu pale hawa hufanya kazi ya kuwasaidia majukumu ya kufanya research mbalimbali za masuala ya kisheria.
Wameingia hapa Majaji watatu kama kawaida ambao ni Jaji Dunstan Ndunguru, James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde. Wakiwa kwenye magauni yao nasikia yanaitwa majoho mekundu.
Limesomwa shauri hapa na karani na amesimama Renatus Mkude Wakili Mkuu wa Serikali na ametambulisha wenzake muda huu, anasema upande wa Jamhuri wako tayari.
Mhe. Lissu ameulizwa yuko tayari na anaomba akumbushwe shahidi aliishia wapi kujibu maswali yake.
Amekumbushwa anasema anaomba aanze sasa.
Mhe. Lissu: Shahidi umeamka salama?
Kaaya: Nimeamka salama Mheshimiwa Lissu.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ulieleza kwamba fomu No. 145 kwamba haikusomwa wakati wa committal Kisutu?
Kaaya: Sikuwepo Kisutu.
Mhe. Lissu: Je umeileta hapa Mahakamani?
Kaaya: Sijaileta pia.
Mhe. Lissu: Sasa turudi tulipoishia jana. Maelezo yako Polisi ulitoa maneno mengi ikiwemo "Baadhi ya maneno mengine aliyotamka Rais alitoa maelekezo kuwa hakikisheni wapinzani hawaendi kokote....."
Naomba majaji shahidi apewe Exhibit D1 ili twende pamoja.
Sasa shahidi baada ya kelele nyingi za wapinzani kuenguliwa akiwemo Nchimbi alisema mambo kuhusu uchaguzi.
Je unafahamu Mchengerwa Waziri wa Tamisemi alisema wakikata rufaa wagombea walioenguliwa watarudishwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: je unafahamu Mchengerwa aliongeza muda wa rufaa ili watu wakate rufaa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Unafahamu wagombea angalau wa Chadema kwa maelefu walikata rufaa ndani ya huo muda wa rufaa ambao uliongezwa na Mchengerwa?
Kaaya: Sikumbuki.
Mhe. Lissu: Rufaa za Uchaguzi wa serikali za mitaa zinasikilizwa na Kamati za Wilaya?
Kaaya: Sina kumbukumbu.
Mhe. Lissu: Je unafahamu wenyeviti wa kamati za rufaa za Wilaya ni Makatibu tawala wa Wilaya ambao ni wateule wa Rais?
Kaaya: Sina Uhakika.
Mhe. Lissu: wote waliokata rufaa waliorudishwa hawafiki hata 10?
Kaaya: Hilo silifahamu.
Mhe. Lissu: Ila maneno yangu unasema ya uongo kuhusu uchaguzi wakati wewe kila kitu hujui?
Kaaya: Kimya.
Mhe. Lissu: Sasa watu wanaosimamia uchaguzi wote wa serikali za mitaa ni watu wa Rais kama nilivyokuonyesha mimi nakosea wapi?
Kaaya: Rais akishachaguliwa anafanya kazi kwa niaba ya Serikali na sio Chama chake.
Mhe. Lissu: Kwahiyo akikosea na mimi nikimpinga nikisema anafanya mambo ya hovyo kuengua watu wa Chadema nakosea wapi? Hapo anakuwa ameacha kuwa mwana CCM?
Kaaya: Haachi kuwa Mwanaccm.
Mhe. Lissu: Sasa wewe fundi wa Viyoyozi hebu tuambie kazi za Mwenyekiti wa CCM anazifanya nani kipindi akiwa Rais?
Kaaya: Anaendelea kuzifanya mwenyewe.
Mhe. Lissu: unafahamu zaidi ya asilimia 98 ya wenyeviti wa mitaa waliochaguliwa ni wa CCM?
Kaaya: Sifahamu.
Mhe. Lissu: Je unafahamu kwamba mwaka 2014 kwenye Uchaguzi wa Vijiji na mitaa ambao wagombea wa upinzani hawakuenguliwa walipata asilimia 33 ya viti vyote vya serikali za mitaa?
Kaaya: Sina Takwimu hizo.
Mhe. Lissu: Je unafahamu mwaka 2014 asilimia zaidi ya 20 walienda kwa upinzani ulienda kwa upinzani?
Kaaya: Hilo nilisikia.
Mhe. Lissu: Uchaguzi wa 2019 ambao wagombea walienguliwa wa upinzani CCM ilipata wenyeviti wa mitaa 100%?
Kaaya: Sikumbuki.
Part 107 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
Feeling profound sadness for those dying of natural causes but nothing for the young Tanzanians and East Africans you’re killing is wild! Release Polepole and all the hundreds you have disappeared and we will believe you have a heart to feel sadness for anyone. #EndAbductionsEA #JumuiyaNiYetu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 91.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama hicho cheo cha special seargent kipo kwenye vyeo vya Police hapa Tanzania.
Kaaya: Nilisema nimehudhuria mafunzo ya Special seargent na sio cheo cha special Sergeant.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji someni mlichoandika mtusaidie alisema nini tafadhali sana nawaombeni.
Jaji: anasoma hayo maelezo na kusema kuwa alipandishwa cheo cha rank ya Special Sergeant.
Mhe. Lissu: sasa tuambie katika muundo wa jeshi la polisi kama hicho cheo kipo?
Kaaya: Hicho cheo kipo ndio maana hayo mafunzo yalikuwepo na nilihudhuria.
Mhe. Lissu: Je huo ushahidi wa Special seargent uko wapi kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Waheshimiwa Majaji hayapo.
Mhe. Lissu: Ni kweli kwamba ulisema ulipokamilisha hayo mafunzo ulipewa cheti cha kushiriki hayo mafunzo na useme kama umeandika kwenye maelezo yako?
Kaaya: Ni kweli nilisema na ni kweli kuwa hayapo kwenye maelezo yangu. Nilisema hapa mahakamani pekee.
Mhe. Lissu: Je ni kweli au si kweli ulisema mwezi October 2021 ulipelekwa kwenda kusomea assistant Inspector kule Moshi?
Kaaya: Ni kweli
Mhe. Lissu: Yako wapi hayo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Hayapo.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli kwa ushahidi wako baada ya mafunzo ya assistant Inspector ilipofika Feb. 2022 ukafuzu na kupata cheti cha mahudhurio.
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Hivi kwanini huongezi sauti?
Kaaya: Sawa nitaongeza.
Mhe. Lissu: haya jibu swali?
Kaaya: Hayo maelekezo hayapo kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Mhe. Lissu: waeleze Majaji kama ni kweli tarehe 09/10 ulisema hapa mwezi June 2025 ulipandishwa cheo na kuwa full Inspector kwasababu ya utendaji kazi mzuri?
Kaaya: Ni kweli Majaji.
Mhe. Lissu: waeleze sasa hayo mambo mema kama yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Na yenyewe hayapo.
Mhe. Lissu: Ulienda kwenye mafunzo ya miezi miwili kuanzia Januray hadi March 2020 ulijifunza forensic investigation in modern science?
Kaaya: Nilisema lakini hayapo kwenye maelezo yangu ya Polisi.
Mhe. Lissu: Ni kweli au sio kweli kwenye ushahidi wako wa Tar. 09/10 ulisema ulipata mafunzo ya SISSCO certified support in Cyber security?
Kaaya: Ni kweli nilisema.
Mhe. Lissu: yako wapi kwenye maelezo yako?
Kaaya: Hayapo
Mhe. Lissu: Sasa kwanini hutoi sauti Polisi?
Kaaya: Natoa.
Mhe. Lissu: Haya toa basi.
Kaaya: sawa natoa.
Hii leo ni kama ule wimbo wa nauliza UTATOA, HUTOI.😄😄😄
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli ulisema vilevile ulisomea computer Hacking katika chuo cha Unique Academy pale Upanga?
Kaaya: Nilisema kweli hapa Mahakamani.
Mhe. Lissu: Ulisema kama umesomea computer Hacking?
Kaaya: Sikusema.
Mhe. Lissu: kwamba mafunzo yalichukua miezi miwili yaani week 8?
Kaaya: ni kweli nilisema ila kwenye haya maelezo hapa sijaandika.
Mhe. Lissu: Ulisema ili mtu yeyote kuweza kutumia mitandao ya Kijamii mtumiaji huyo anatakiwa kujisajili kwa kuweka taarifa zake ili zionekane na watumiaji wengine?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Piia ulisema ukiwa unajisajili unapata username jina lako, password na email address unaviweka?
Kaaya: Ni kweli ila sikusema unaweka nilisema unaandaa.
Mhe. Lissu: basi ni sawa jibu sasa swali langu kama hayo maelezo yapo kwenye hayo maelezo yako ya Polisi.
Kaaya: Hayapo kabisa.
Mhe. Lissu: baada ya kuandaa yote hayo unaingia kwenye uwanja wa mtandao husika kwa kadri ya maelekezo utakayopewa?
Kaaya: Ni sahihi nilisema hapa lakini kwenye maelezo niliyotoa Polisi haupo, usije sema nisome wakati sikuandika.
Mhe. Lissu : ulisema kuhusu ukurasa wa mtumiaji yaani user page?
Kaaya: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Je upo kwenye maelezo yako ya Polisi?
Kaaya: Haupo
Mhe. Lissu: Baada ya hapo ulisema hivi kwamba kwenye YouTube ukiingia, unaweka username na email address na password na baada ya hapo unajaza taarifa.
Kaaya: Sikusema neno kuandaa.
Part 92 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako ujumbe uende mbali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 83
Job Mrema: Tarehe 07/04/2025 nini kilitokea?
John Kaaya: Nakumbuka nilikuwa zamu kazini. Wakati naendelea na majukumu ya kila siku. Alinipigia afande SSP George majira ya asubuhi akinielekeza niende Ofisini kwake.
Ulivyofika ofisini ikawaje?
Kaaya : Alinikumbusha kuhusu ile taarifa niliyompelekea aliniamuru nirudi Ofisini ninapofanyia kazi za doria mtandaoni na kupakua video ile katika ukurasa wa Jambo TV niipakue na baadae nimpelekee.
Nilivyopokea amri ile nilirudi ofisini kuifanyia kazi.
Nilipofika ofisini niliandaa vitendea kazi vyangu kama vile computer na notebook. Nilikagua utendaji kazi wa computer yangu na nilichukua police notebook yangu na kuchukua ile link na kuinakili kwenye program maalumu kwa ajili ya kupakua yale maudhui.
Job Mrema: Halafu ikawaje?
John Kaaya: Niliandaa Flash mpya aina ya XIOXIA yenye ukubwa wa GB 8 niliiweka kwenye computer na kuifanyia virus scanning na baadae nikaifanyia formating ili kuondoa data yoyote iliyomo mle kwenye flash.
Ndipo nikaichukua ile video na kuihifadhi katika flash hiyo.
Job Mrema: wakati unaipakua hiyo video ilikuwa na muonekano gani?
John Kaaya: ilikuwa na watizamaji elfu 52 na waliocomment mia tatu.
Kingine nilibaini ile video ilichapishwa tar. 03/04/2025 kwenye ukurasa wa Jambo TV.
Job Mrema: Kuhusu maudhui yake ulifanya nini?
John Kaaya: Niliweza kuisecure flash ile kwa ku encrypt na password.
Nilichukua pia PF 145 ambayo ni Exhibit label na niliilabel kile kielelezo na kukipa alama DM.
Radio call la askari limeanza kuita humu ndani mahakama imesimama kidogo.
Majaji hawajasema kitu wanasema haya tuendeleeee. 😂😂
Kuna mambo majaji wanakausha ila Katuga huwa ni mnoko sana angekuwepo angeweza msingizia hata Chadema yeyote hapa maana anatuchukia sana.😀
Job Mrema: Baada ya kufanya labelling uliendelea na hatua gani nyingine?
John Kaaya: Niliondoka ofisini na kuonana na afande SSP GEORGE na kwamba nimeshapakua na kuyahifadhi.
Hiyo ilikuwa ni tarehe 07/04 majira ya saa 9 mchana baada ya kufika ofisini kwa George nilionana nae na kumjulisha kwamba maelezo aliyonipa nimekamilisha.
Baada ya kumjulisha afande George alichukua diary yake na kunijulisha kuwa ameshafungua kesi ambayo ina Reference No. DSMZ/CID/PE.101/2025
Pia aliniambia niorodheshe hiyo kesi namba kwenye kile kielelezo ambacho niko nacho yaani flash aliniambia niandike maelezo yangu nimpatie.
Job Mrema: nini kikafuata?
John Kaaya: Aliniambia nikipeleke kielelezo kwa ACP Malugala mtunza vielelezo. Nilijaza namba ya jalada kwenye kielelezo. Nilichukua kielelezo DM na kukipelekea kwa ACP Malugala.
Job Mrema: Tar. 08/04 kilitokea nini sasa?
John Kaaya: Nilikuwa zamu kazini na nikiwa naendelea na majukumu yangu.
Alinipigia afande SSP George akiniamuru niende Ofisini kwake, nilisitisha shughuli zangu na kwenda kuonana na Afande George.
Job Mrema: Nini kiliendeleaa ulipofika?
John Kaaya: Nilimkuta yupo na Mpelelezi.
alinikumbusha kuhusu tukio la Tarehe 07/04/2025 kuhusu uwasilishaji wa kielelezo kwake.
Aliniambia nimpatie yule mpelelezi password katika kielelezo DM.
Nilichukua POLICE NOTEBOOK yangu kwa ajili ya kujikumbusha password yangu na kuinakili kwenye notebook ya mpelelezi niliyoamuriwa nimpatie.
Job Mrema: Je hiyo video ya tarehe 04/04/2025 utaitambuaje ukiiona?
John Kaaya: Hiyo video naweza kuitambua kwa maudhui yanayotamkwa, mzungumzaji amevaa kombati ya Kaki, nyuma ya mzungumzaji kuna rangi za Bendera ya Taifa pia itakuwa kwenye flash disk.
Job Mrema: Kwani Maudhui yaliyokuwepo kwenye hiyo video ni yapi?
Hawa watu wanatupotezea muda kabisa wanaulizana maswali yale yale yani, Wanakera sana.
John Kaaya: Anaanza kusema yale maudhui ya Lissu.
Part 84 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 82
John Kaaya: Pia aliposema Mahakamani hakuendeki ila Mahakama ni chombo cha kutoa haki na kutoa maamuzi ya mambo mbalimbali yanayobishaniwa.
Hivyo anavyojulisha umma kwamba hakuendeki ni kutoa taarifa ya uongo kwa umma na kuitishia serikali 😂
Kaaya ana akili hata kidogo huyu yani Mahakamani hakuendeki eti ni kuitishia serikali.😀😀😀
Job Mrema: Baada ya kuitizama hiyo video nini kingine ulikisikia.
John Kaaya: Lissu alisema Tutaenda kuzuia uchaguzi, tutazuia uchaguzi kwasababu wanasema tunahamasisha uasi na tutaenda kuuvuruga sana sana.
Natamani mngekuwa mnamuona huyu shahidi aiseee, kituko cha mwaka.😀
John Kaaya anaendelea: Kwa matamshi hayo niliyosema waheshimiwa majaji niliona kuna viashiria vya jinai.
Uchaguzi huandaliwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria hivyo kuzuia uchaguzi kwa kuhamasisha uasi bila kufuata utaratibu ni kosa.
Haya yote aliyafanya lengo lake ni kuitisha serikali ambayo ndio msimamizi mkuu wa Sheria na kulinda amani.
Nilichogundua TANZANIA haitakuja kushinda kesi yoyote kimataifa kama mashahidi wetu ndio hawa na Mawakili wetu wa serikali ndio hawa akina Job Mrema kama nchi tunasafari ndefu.🥹
Anaendelea hapa John Kaaya: Baada ya kuona hayo maudhui nilichukua POLICE NOTEBOOK yangu na ku note maudhui hayo niliyosema na nilinote link ambayo hayo maudhui yanahusika.
Hapa namaanisha ni ukurasa wa Jambo TV pamoja na mtoa maudhui ndugu Tundu Lissu.
Job Mrema: Kila muda unasema Tundu Antipas Lissu unamfahamu yuko wapi?
John Kaaya: anasema namfahamu na yupo hapa mahakamani.
Job Mrema: Yuko wapi?
John Kaaya: Yule pale anampungia.
Majaji wanasema ukipunga mkono maana yake umemuonesha nani?
Watu wanacheka. 😀😀😀
Shahidi ananona aibu kumuonesha Lissu kwa kidole.
Hawa watu wanawasababishia watu watende dhambi wasizotaka.
Huyu shahidi kiukweli usikute hajataka kabisa kuja kufanya hii kazi maana namuona kama hana amani😂
John Kaaya anaendelea: Baada ya kuona hayo nilimjulisha mkuu wangu wa kazi ambae ni mkuu wa kitengo cha doria mtandaoni.
Job Mrema: Hiki kitengo kipo ofisi gani?
Kaaya: Kipo ofisi ya DCI.
Job Mrema: Hiyo picha mjongeo alimaliza kuitizama muda gani?
John Kaaya: Nilimaliza kuyatizama kwenye majira ya saa nne asubuhi siku ya tarehe 04/04/2025.
Job Mrema: Ulitoa taarifa kwa mkuu wako wa kazi ulitoa taarifa saa ngapi?
Jibu: Nilipomaliza kuitizama ndio nilitoa taarifa kwa mkuu wangu wa kazi.
Job Mrema: ulivyotoa taarifa ulipata matokeo gani?
John Kaaya: Nilielekezwa kwenda Polisi kanda maalumu Dar es salaam kwa ajili ya kwenda kumjulisha Afande SSP George. Juu ya maudhui yale.
Job Mrema: Utekelezaji wa majukumu yako ikawaje?
Kaaya: Nilisimama kutekeleza majukumu mengine nilienda kuonana na Afande George ambae kwa siku ile alikuwa ni Naibu Kamanda wa Upelelezi Kanda ya Dar es salaam na ilikuwa tarehe hiyo hiyo Tar. 04/04/2025.
Job Mrema: Ikawaje?
John Kaaya: Nilivyofika nikamkuta Afande George na kumjulisha dhumuni la ujio wangu kwake.
Nilimwambia nimeelekezwa na mkuu wa kitengo cha makosa ya mtandao kuwa nije kukupa taarifa ya nilichokiona huko mtandaoani.
Baada ya kumjulisha alinielekeza, nimuonyeshe picha mjongeo zile na nilimuonyesha kupitia simu janja yake kwa kuingia kwenye ukurasa wa Jambo TV.
Job Mrema: Ikawaje tena?
John Kaaya: Basi nilichezesha picha mjongea ile kwa kumuonyesha baadhi ya vipande nilivyobaini vina viashiria vya jinai.
Hapa nazungumzia ile video ya tundu lissu uso kwa uso na watia nia majimboni No reforms, no election.
Job Mrema: Nini kikafuata?
John Kaaya: Afande George alichukua Police Notebook yake na kujaza taarifa kuhusiana na picha mjongeo ile na baada ya kuchukua baadhi ya taarifa muhimu, aliniamuru kurudi eneo langu la kazi kuendelea na majukumu mengine.
Part 83 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 69
Mhe. Lissu : Ulisema kwenye ushahidi wako kwamba Tar. 09/04 ulipigiwa simu na DCP Ramadhani Ng'anzi kuwa alikuwa amekamatwa Mbinga na angesafirishwa usiku huo huo?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa waeleze majaji kama amri ya kunikamata mimi ilitoka kwako au kwingineko?
Mhe. Lissu : Ilitoka kwingineko.
Mhe. Lissu : Yalitokea Dodoma kwa akina Kingai?
George: Hilo sijui.
Mhe. Lissu : Kwahiyo ni kweli mawasiliano yako na Kingai yalikuwa yanapitia kwa Ng'anzi?
George : Mimi sijui kama ilitokea huko.
Mhe. Lissu : Sasa turudi kwenye PGO.
Ni kweli au si kweli askari polisi wanaatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuelewa kanuni kwamba Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayotumia kanuni ya utawala wa sheria?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Order 1(2)C yapo kwenye PGO hayo niliyosema yapo huko kwenye PGO?
George: NI SAHIHI YAPO.
Mhe. Lissu : Askari Polisi wote wanatakiwa kwa muda wote wanatakiwa kuheshimu haki za binadamu na uhuru uliowekwa na Katiba?
George: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu O.1(3) ya PGO ndio hayo yapo?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Je haki ya kutoa maoni ni pamoja na mambo mnayoyasimamaia kama haki za msingi kwa binadamu?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Haki mnayoitakiwa kuiheshimu muda wote ni kuhakikisha kila mtu kuishi kwa uhuru bila kosa lolote?
George: Ni kweli pia.
Mhe. Lissu : Haki ya kutoa mawazo yake hadharani na kujiunga na vyama vya siasa au mashirika?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Haki ya kufaidi haki za msingi za binadamu kwa mujibu wa ibara ya 27?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa ni kweli au si kweli PGO inaposema Tz ni nchi ha kidemokrasia ya vyama vingi?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Sasa kama ni nchi ya mfumo wa vyama vingi ni sahihi Inategemea nini au utaratibu wa Polisi?
George: Inategemea sheria.
Mhe. Lissu : Ni haki kuunda Chama na kupinga serikali?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Ni halali kwa mtu yeyote kupinga Chama kinachotawala?
George : Itategemea kitu gani kwa njia halali inaruhusiwa.
Mhe. Lissu : Kuitisha mikutano ya hadhara au mikutano ya ndani si ni sahihi?
George: Ni sahihi kabisa, kutaka kuwa na mkutano ni shida vitisho.
Mhe. Lissu : Sasa waeleeze Majaji katika maelezo yako kuna mahali kokote ambapo ulieleza kwamba hawa watu wana haki ya kukutana na kusema mambo yao?
George: Hilo sikuandika.
Mhe. Lissu : Kuna mahali kokote ulisema Tundu Lissu na Chadema wana haki ya kutaka mabadiliko ya Katiba?
George: Sikusema kwenye maelezo yangu
Mhe. lissu : Ulisema pia kuwa Majaji ni watu wa Rais na ni Maccm kwahiyo mahakamani hakuendeki?
George: Ni sahihi.
Mhe. Lissu : Kwa ufahamu wako Rais ndie anateua Majaji wa Mahakama kuu?
George: Ndio sahihi.
Mhe. Lissu: Kwa ufahamu je majaji wa Mahakama ya Rufani?
George: Anateua pia.
Mhe. Lissu Jaji Mkuu Je?
George: Anateua pia.
Mhe. Lissu: Je ndie anateua Jaji Kiongozi?
George: Ni sahihi pia.
Mhe. Lissu : Anateua Wasajili wa Mahakama kuu na mahakama ya rufani?
George: Ni kweli.
Mhe. Lissu : Kwa ufahamu wako Rais ndie anayeteua Mwanasheria Mkuu wa Serikali?
George: Ni sahihi hadi DPP anateua Rais.
Mhe. Lissu : Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiteuliwa anaakuwa Mbunge ni kweli?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu : Mbunge yeyote wa nchi hii ni lazima awe mwanachama wa Chama cha siasa?
George: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu Sasa waeleze majaji kama unamfahamu Jaji Eliezer Feleshi Mbuki?
George: Namfahamu ndio.
Mhe. Lissu : Kama Eliezer Feleshi Mbuki alikuwa Mwanasheria mkuu wa serikali na Mbunge wa bunge la JMT?
George: NI KWELI.
Mhe. Lissu : Kwahiyo alikuwa mwanachama wa CCM?
George: Hilo sina uhakika.
Mhe. Lissu : Je unamfahamu Jaji Frederick Werema marehemu?
George: Namfahamu.
Mhe. Lissu : Na yeye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali?
George: Ndio
Part 70 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 63
Mhe. Lissu : ulisema hizo video zilikuwepo kwenye mitandao mingine?
George: P ndio alisema.
Mhe. Lissu : Je hukuwa na interest kujua umechapisha kwa mitandao mingine?
George: Sikuwa na interest mimi.
Mhe. Lissu : Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya Mahamba.
George: Mimi sikusoma.
Mhe. Lissu : kwahiyo kumbe hukusoma maelezo ya Amin Mahamba?
George: Sikusoma ndio.
Mhe. Lissu : Hizi video clip zilifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu cyber forensic analysis?
George: Ni kweli kabisa zilifanyiwa.
Mhe. Lissu : Eribariki Kahaya ndio alifanya kazi hiyo?
George: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu : ni sahihi Kahaya alisema camera iliyotumika ni aina ya Sony
George : Maelezo yake sikusoma na yeye ni shahidi atakuja kutoa.
Mhe. Lissu : Na Kaaya alisema hayo maneno yakiwekwa mtandaoni na Jambo Tv?
George: Mimi sikusoma maelezo yake.
Mhe. Lissu : Waeleze Kama ulisoma maelezo ya Andrew Churu. Yule askari wa Dodoma.
George: Ya Andrew Churu sikusoma, mimi ilisoma ya P.
Mhe. Lissu : maelezo yako uliandikiwa na nani?
George: Niliandika Mwenyewe.
Mhe. Lissu : Je kabla ya kuandika maelezo hayo uliomba ushauri wa kisheria wa mwanasheria yoyote?
George: Sikuomba ushauri kokote.
Mhe. Lissu : Naomba usome kifungu cha 11(4) cha CPA. Ulisema umeandika kifungu cha 11(3)?
George: Ni kweli.
Mhe. Lissu : Ni sahihi hicho kifungu hakiruhusu mtu kujiandikia mwenyewe?
George: Kinaruhusu unaweza kujiandikisha. Kama nilivyoeleza hakuna kifungu kinachozuia na mimi ni Police officer nilijiandika mwenyewe.
Mhe. Lissu : Nani aliyekuonya? Nani aliyekukanya? Section 10(3) of CPA.
George: NI MIMI MWENYEWE NDIO NILIJIKANYA.
Watu wanacheka.😂😂😂😂
Mhe. Lissu : Nani alithibitisha pale chini baada ya maelezo yako?
George: Ni Mimi Mwneyewe, nilijiandika, nikajikanya na kujithibitisha mwenyewe.
Mhe. Lissu : ulisema mimi nina kiapo cha JKT nilitoa kinyume na kiapo changu?
George: Ni kweli nilisema hivyo.
Mhe. Lissu : Je wewe umewahi kwenda JKT?
George: MIMI SIJAWAHI KWENDA JKT.
Mhe. Lissu : Nilikwenda JKT kambi gani?
George: Mwaka 1989 ulianzia mafinga iringa na baadae ukaenda Itende Mbeya ukapewa namba fulani anaitaja hapa. Ulifuzu na kupewa cheti.
Mhe. Lissu : Je ulikuwepo mwaka 1989?
George: Sikuwepo.
Mhe. Lissu : Je ulikuwepo Itende?
George: Sikuwepo hata Itende ila wewe umegombea urais taarifa zako zinajulikana.
Mhe. Lissu : ulikiona cheti changu cha Itende?
George: Nimeona copy yako.
Mhe. Lissu : Sasa waeleze Majaji kama hayo uliyosema yapo kwenye maelezo?
George: Hayapo.
Mhe. Lissu : Kama nilienda jeshini miaka 39 mimi ni mwanajeshi?
George: Wewe ni askari wa akiba.
Mhe. Lissu : Soma ibara ya 147(4)
Mnakaa huko mnadanganyana hamjui mambo mnajifanya mnajua.
Jaji anasema Mshitakiwa tafadhali.
George anasoma Katiba sasa Mwanajeshi maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au kudumu katika jeshi la polisi, lawananchi, au la magereza au polisi.
Mhe. Lissu : Sasa waeleze majaji kama mimi nimeajiriwa kwa muda katika mojawapo ya hayo majeshi.
George : Wewe umeajiriwa na JKT.
Mhe. Lissu : Je kwenda JKT mwaka 1989 na 1990 je nilikuwa nimejajiriwa?
George: Hukuwa umeajiriwa.
Mhe. Lissu : nilivyomaliza nilikuwa nimeajiriwa?
George: Hukuwa umeajiriwa.
Mhe. Lissu : Kwenye Katiba kuna maneno askari wa akiba?
George: Hayapo kabisa kwenye Katiba.
Mhe. Lissu : Waeleze kama umewasilisha hati ya kiapo cha utii cha kwangu hapa mahakamani?
George: Sijakiwakilisha mimi, sijaleta hapa.
Mhe. Lissu : Je mtu yeyote aliyepitia JKT anakuwa mwanajeshi milele? Askari wa akiba anatambulika kikatiba?
George: Anatambulika.
Mhe. Lissu : Hawa maaskari wa akiba wana masharti na askari wengine?
George: Ndio.
Mhe. Lissu : Je Kikwete Ruten Kanali ni mwanajeshi alikuwa?
George:Ndio alikuwa mwanajeshi.
Part 64 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako