@mpambazi Tuache kutetea ujinga, hayo ndio mambo yamemrudisha nyuma huyo kijana. Yeye sio wa kwanza kuulizwa asichokipenda na ipo namna nzuri ya kujibu na mengine yakaendelea.
@MarekaMalili Hii njia wanayotumia mbaya sana, kibaya siku hizi ukiwa na M1 unaweza mchafua mtu ndani ya siku moja asiamini kupitia wanaojiita influencers.
Pauline Gekul baada ya kupewa dhamana ya polisi saa tano usiku kituo cha polisi Babati Mjini, ameachia hii video fupi ikimuonyesha Hashimu Ally Philemon akifanyiwa mahojiano na Gekul na watu wake. Hashimu suruali yake imeshuka chini (yupo uchi).
Polisi Manyara, huu ni ushahidi, Pauline Gekul alimuweka chini ya ulinzi Hashimu Ally Philemon, akamtesa na kumlazimisha kukiri alipewa dawa ya kumwaga eneo lake la biashara. Pauline anapata wapi mamlaka ya kuweka watu chini ya ulinzi?
Mbunge, Naibu Waziri, Msomi kutoka chuo kikuu cha UDSM na UDOM, unawezaje kuamini masuala ya ushirikina na kuamua kumtesa kwa kumwekea chupa makalioni mwananchi wako kwa tuhuma za kutumwa kumwaga dawa kwenye parking ya magari yako?
Kwa video hii aliyoachia mwenyewe, Pauline anajinyonga kwa kamba yake mwenyewe. Tuhuma za Hashimu Philemon kuwekewa chupa makalioni zinathibitika kwa tafsiri za awali kumuona Hashimu akihojiwa na Gekul akiwa amevuliwa suruali yake.
Tunajua, Kamanda wa Polisi - Manyara, George Katabanzi unamfichia Pauline Gekul maovu yake, na tangu mwanzo umeonyesha kumlinda, umegoma kupokea malalamiko ya Hashimu lakini umepokea malalamiko ya Gekul kwamba wanataka kumuua.
UMMA wa Babati Mjini unatakiwa kusikiliza sauti kutoka nyikani na kumkataa Pauline Gekul kwa vitendo kama polisi wanamlinda na CCM wakimtetea na kumsafisha. Gekul amefanya vitendo vya kinyama sana ambavyo mtu timamu hawezi kufanya.
MMM, Martin Maranja Masese