Historia Huonya: Watoto wa Viongozi Wajifunze Unyenyekevu, Si Kiburi cha Madaraka
Na Rev Peter Simon Msigwa
Historia ya dunia imeandika kwa wino usiofutika kwamba hakuna kitu kilichoharibu familia za watawala haraka kuliko pale watoto wao walipoanza kuamini kuwa mamlaka ya wazazi wao ni mali ya familia. Dola si urithi wa ukoo; ni dhamana ya wananchi.
Karibu kila utawala uliodhoofika ulianza na dalili zilezile: watoto wa viongozi kuonekana kana kwamba wako juu ya sheria, marafiki wa familia kupewa upendeleo, taasisi za umma kuanza kuogopa majina badala ya kuheshimu sheria, na wananchi kuanza kuona kuwa haki haipatikani kwa usawa.
Historia ya Uday Hussein nchini Iraq ni onyo. Alipoamini kuwa jina la baba yake lilimpa haki ya kufanya atakavyo, aliijengea familia yake hofu badala ya heshima. Mwishowe, utawala ulianguka, na jina lililotegemewa kuwa chanzo cha nguvu likawa alama ya maangamizi.
Historia ya familia ya Muammar Gaddafi nchini Libya nayo ni fundisho. Walioonekana kutotikisika waligundua kwamba dola inaweza kulinda mtu kwa muda, lakini haiwezi kushinda historia. Serikali huanguka, tawala hubadilika, lakini kumbukumbu za matendo hubaki.
Hata tawala zilizodumu kwa muda mrefu zimeonyesha ukweli mmoja: pale taasisi zinapoanza kutumikia familia badala ya taifa, wananchi huanza kupoteza imani. Na wananchi wanapopoteza imani, hakuna jeshi, hakuna polisi, hakuna walinzi wala propaganda zinazoweza kuirejesha kwa nguvu.
Ndiyo maana watoto wa viongozi wanapaswa kuwa wa kwanza kuheshimu sheria, wa kwanza kuwa wanyenyekevu, na wa kwanza kukataa upendeleo. Hawapaswi kutegemea jina la wazazi wao, bali wajenge heshima kwa tabia zao wenyewe.
Kwa Tanzania, ujumbe ni rahisi lakini mzito:
Hakuna Mtanzania anayepaswa kuwa juu ya sheria. Si mtoto wa rais, si mtoto wa waziri, si mtoto wa tajiri, si mtoto wa mkulima. Katiba na sheria ndizo zinazopaswa kuwa kubwa kuliko majina ya familia.
Taifa lenye taasisi imara halihitaji familia yenye nguvu; linahitaji sheria yenye nguvu. Heshima ya viongozi hailindwi na walinzi wa silaha, bali na imani ya wananchi kwamba sheria inatumika kwa usawa.
Madaraka ni ya muda. Magari yenye ving’ora yatapita. Walinzi wataondoka. Vyeo vitaisha. Lakini historia itaendelea kuuliza swali moja tu:
Je, mlitumia nafasi mliyopewa kutumikia wananchi, au mlitumia wananchi kulinda nafasi zenu?
Historia huwa haina upendeleo. Haiangalii jina la familia, haijali cheo cha mzazi, wala ukubwa wa dola. Historia huhukumu matendo. Na hukumu yake ndiyo hukumu ya kudumu kuliko zote.
Maana ya Mwanaharakati
Mwanaharakati ni mtu anayechukua hatua za makusudi na za wazi ili kuleta mabadiliko katika jamii kwa kutetea haki, kupinga dhuluma, kupaza sauti kwa wanyonge, na kushawishi sera au maamuzi yanayogusa maisha ya watu.
Mwanaharakati hatoi maoni tu; huchukua hatua. Hatua hizo zinaweza kujumuisha:
Kusema hadharani dhidi ya dhuluma au ufisadi.
Kutetea haki za binadamu na usawa.
Kuandaa kampeni au harakati za kuleta mabadiliko.
Kuhamasisha na kuelimisha jamii.
Kushinikiza serikali au taasisi kutenda kwa haki.
Kutumia njia za amani na sheria kudai mabadiliko.
Kwa kifupi, mwanaharakati ni mtu anayesimama kwa ujasiri kutetea ukweli, haki na maslahi ya umma, hata pale kufanya hivyo kunapokuwa na gharama binafsi. Lengo lake si kupata umaarufu, bali kuona jamii inakuwa yenye haki, usawa, uwajibikaji na utu kwa wote.
@Roma_Mkatoliki Nakubali sana mwanangu Mkato. Mimi hii ngoma niliisikiliza na wanangu NON—STOP mule Segerea! U know the drill.
RIP Mwanangu Bataboy, mtoto wa Tabata! Hii ngoma ulikuwa unaiimba hadi unalia mwanangu.
Bad luck ulifia jela.
Keep resting in peace, my dawg Bataboy🙏🏽😭
Mwanasiasa asiye mwanaharakati ni tapeli anayesaka tonge kupitia kauli-mbiu na utam ulishi wa vyama. Mwanaharakati ana lake jambo la kulisimamia kokote aliko hadi mwisho wake. Ukiniuliza mie, dharau wanasiasa, heshimu mwanaharakati.
Hii ni michezo tunaijua sana! Huyu anasema mawakili wasiwe wanaharakati ukimuuliza kwanini? Hana jibu lakini ukweli ni kuwa wanahoji sana!
Mwingine anasema kufanya harakati ni ugaidi, hata walioanzisha hiyo sheria ya ugaidi wanashangaa tunavyoitumia!
Asiyemwanaharakati ni mfu!
Za Kikachero! Winga amesema hivii, ukimtoa FEITOTO yeye ndiye anayefuata kwa kuwa na mchango mkubwa kwenye timu kwahiyo amesema mahitaji yake ni mshahara wa Milioni 50 kwa mwezi na signing on fee ya Milioni 500 ili asaini mkataba mpya kwa matajiri! Mazungumzo yanaendelea…..
No Scotland, looking like no party. ❌
To qualify from the group stage, they just need:
1️⃣ 🇬🇭 to win by 3+ goals against 🇭🇷.
2️⃣ 🇨🇩 and 🇺🇿 to draw, or 🇺🇿 to win by up to 3 goals.
3️⃣ 🇦🇹 to beat 🇩🇿 by 2+ goals, or 🇩🇿 to win by 4+ goals.
They're not asking for much, really! 😅