Kuelekea Baraza kuu la kihistoria..
Nimesikia sauti yenu, Asanteni sana Watanzania kwa upendo mkubwa.
Ushindi wetu uko karibu sana..
Msiogope, tutashinda.
Siku ambayo CHADEMA “itafutwa”, ndiyo siku ambayo YESU KRISTO ATARUDI. Najua SHETANI na MAWAKALA 👇 wake wanajitahidi sana KUBAHATISHA SIKU HIYO, lakini wanajisumbua bure. CHADEMA ni MPANGO WA MUNGU.
CHADEMA ina watu
Watu Wana CHADEMA rohoni
Huyu anafanya hii kazi sio kwa ujira maana ndio Kwanza CHADEMA imefunguliwa
Shughuli kama hii CCM ni mpaka mtu apate asali
Kuna siku mtaelewa kwa nini nasema kuwa tunapoteza muda ila mabadiliko yanawezekana kirahisi kwa sababu #WenyeNchiWananchi - tunacheleweshana tu!
But anyway hii njia ilikuwa lazima tupite ili sote tuamke - sema it came with a very heavy price tag!
Ila #TutaelewanaTu
😁😁💪🏽🔥
Anzeni Kanda Maalum
Ni raha sana kutokubali ku compromise! Yaani maamuzi ya kwenu si ile ya kusikilizia na kupangiwa kama vyama vikaragosi vingine!
Simameni hapohapo!
#TutaelewanaTu#FreeTunduLissu
Tanzania haki ni adimu sana kuonekana kama kakakuona vile!
Ndo maana ikitokea hata kwa kuchelewa au kwa mbali shangwe lake ni kubwa sana!
Haki ni adimu kama akili za wale 😂😂😂
Naandika kwenu MAWAKILI wetu. Hakuna anayewalipa. Hakuna anayewaahidi kesho iliyo salama. Lakini bado mnaamka kila siku na kuchagua kusimama upande wa haki kimya kimya bila kelele bila makofi.
Mnakesha mkisoma, mkitafiti mkisafiri mbali mkibeba mzigo wa wasiwasi ambao wengi hawawezi kuuelewa. Wakati wengine wanatafuta raha nyie mnachagua wajibu. Wkt wengine wananyamaza nyie mnabeba sauti za haki.
Hii si kazi hii ni wito. Demokrasia haifi kwa siku moja hufa taratibu pale watu wema wanapochoka kusimama. Na nyie mmeamua kutochoka. Historia haiandikwi na waliokuwa na nguvu bali na wale waliokuwa na ujasiri wa kusimama pale ilipokuwa ngumu.
Mnaweka misingi ambayo hata kama haitatambulika leo itasimama kesho kama nguzo ya taifa lenye haki. Mnaumizwa, mnapuuzwa wakati mwingine mnaogopwa lakini bado mnasimama. Huo ndio ujasiri wa kweli. Huo ndio uzalendo usio na matangazo.
God bless you na wengine wote wenye hari kama zenu kote Nchini.
Much Love MAWAKILI WETU
Asante Wakili Jebra. Uamuzi wako wa siku ile wa kujiondoa kuendelea kusikiliza kesi, baada ya Jaji Mwanga kupuuza sababu zako za kuomba hairisho la muda mfupi ili kuhudhuria mazishi, haukuwa wa kawaida. Ilikuwa ni mpango wa Mungu. Kwani usingechukua hatua hiyo, ungehalalisha zuio batili na leo lingeonekana halali.
God bless you Bro!!
Nimetoka Ukonga kumtembelea Tundu Lissu.
Tumepata nafasi ya kujadili kwa kina mwenendo wa kesi zote zinazoendelea na zile zilizo pending. Amenieleza pia kuwa jana, tarehe 15 Aprili 2026, alikutana na Mhe. Lazarus Chakwera na kuwasilisha kwake masuala muhimu yafuatayo:
Kesi ya Uhaini inayomkabili ni kwasababu ya msimamo wa No Reforms No Election, Kesi zote zinazomkabili yeye na chama zifutwe, na kwamba yuko tayari kwa mazungumzo akiwa mtu huru yeye pamoja na chama.
Matukio yote ya Oktoba 2025 yafanyiwe uchunguzi huru kupitia chombo cha kimataifa, mfano SADC.
Kuwepo kwa mazingira wezeshi ya mazungumzo ya kweli pamoja na utekelezaji wake.
Uwajibikaji wa kitaasisi kwa yaliyotokea Oktoba 2025, mfano, Ofisi ya Msajili, INEC na TCRA, alisisitiza umuhimu wa kurejea Ripoti ya Jaji Nyalali (1992).
Mabadiliko katika vyombo vya ulinzi na usalama, alisisitiza kurejea Ripoti ya Jaji Chande (2023).
Mabadiliko ya mfumo mzima wa uchaguzi, ikiwemo kufutwa kwa INEC na kuundwa kwa chombo kipya huru, akisisitiza kurejea ripoti za waangalizi wa uchaguzi (1995-2025), pamoja na Ripoti za Jaji Warioba na Jaji Nyalali.
Katiba Mpya
Nimempatia pia uamuzi wa Mahakama ya Rufani uliotolewa jana kuhusu chama kuendelea kufanya kazi amesema "watu wajiandae, muhimu nijue mkutano utafanyika wapi a day after Ukonga"
Paul Kisabo
Wakili
Ndugu wanachama wa CHADEMA na Wapenzi wa Demokrasia Nchini.
Chama chetu kimefunguliwa rasmi kufanya shughuli za siasa. Hii ni fursa muhimu katika kuendelea na mapambano ya haki, uhuru na uwajibikaji katika Taifa letu.
Lakini ukweli usioepukika ni huu
hatuna ruzuku hata ya SENTI MOJA.
Hii ina maana kwamba uhai, nguvu na uendelevu wa CHADEMA uko mikononi mwetu sisi wenyewe.
Hatuna budi kuchukua jukumu.
Hatuna budi kusimama.
Hatuna budi kuchangia.
Kila Mwanachama na kila mpenda Demokrasia ana wajibu wa moja kwa moja, kuchangia CHADEMA.
Usione mchango wako ni mdogo.
Usisubiri mwingine achukue nafasi yako. Kila senti unayotoa ni nguzo ya kusimama kwa chama hiki.
Tujenge utamaduni wa kuchangia bila kusukumwa. Tujenge tabia ya kusaidia chama kila wakati. Hapo ndipo tutakapopata uhuru wa kweli wa kisiasa na kiutendaji.
Mimi nipo, na nimeanza.
Na wewe pia ni wakati wako sasa.
Chukua hatua.
Anza kuchangia.
Simama na CHADEMA.
Kwa pamoja, tutakijenga chama imara na Yaifa lenye HAKI.
Tuchange tu kwa namba maalumu za CHAMA na Akaunti za Benki ili kujenga uadilifu wa Taasisi Imara.
Mikakati zaidi inakuja baada ya vikao kuanza.
Asanteni.
‼️FUNZO‼️
Gen Z Nepal waliandaa clips fuoi kuonyesha maisha wanayoishi watoto wa viongozi ya magari, nguo na saa ghali huku familia za maskini zikiteseka na kuishi maisha ya dhiki! Ufisadi mkubwa wa viongozi ulikuwa chanzo! Serikali ikaamua kufunga mitandao, vijana wakaamua wamechoka wameingia barbarani!
Watawala wetu wanasema watanzania ni waoga na wajinga na ndo viongozi wa Nepal walivyojiliwaza na walikuwa wanaringisha mali zao bila woga! Leo tunaona watoto wa viongozi wetu wanaendesha magari ya mabilioni na kujipost wakati watoto wanakaa chini kwenye matope shuleni!
Jamani KIBRI! Jambo baya sana!
Eniwei #TutaelewanaTu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Mhe. Lissu anamuuliza Katuganga nani anaevunja amri ya mahakama kati ya Wakili Mkuu wa Serikali na team yake yote ambao wamewaweka wazi wote.
Kile walichoambiwa na Mahakama Kuu wasikifanye ndo wamekifanya, mwenye kosa ni nani hapo mimi au wao?
Walishawaweka hadharani wao.
Nisingejua makazi yao, makabila yao na mitaa yao. Wameleta wenyewe.
Halafu hapa wanasema wakitajwa hawatafika.🤣🤣🤣🤣
Majaji wanateta kidogo hapa.
Ngoja tusubiri.
Kumenuka.
Kazi ishakuwa ngumu hapa.😂
Majaji wanateta.
Kimeumana.
Jaji: anawasha kipaza sauti kinapiga kelele hakiwaki. Vurugu tupu mahakamani.
Anasema tumewasikia.
Mahakama inasema tayari kuna amri ya mahakama hii hii hiyo amri inaendelea kuwa valid kama ambavyo ilivyo.
Kwahiyo tuiheshimu tu hiyo amri maana haijatenguliwa.
Anatuomba pia tuwe watulivu hapa mahakamani.
Mhe. Lissu : Anasema sasa niendelee. Sitawasoma hao watu.
Nawaomba muangalie kwenye rekodi maelezo ya shahidi P2,3,4,5,6,7,8,9,1 na 11.
Maelezo yao yanafuatana na maelezo yote hayo yanakiuka amri ya Jaji Mtembwa kuna mahali wametoa namba za simu, mitaa kazi, familia, hadi idadi ya wake na watoto wamesema.
Amri ilisema wafiche mambo hayo.
Anasimama tena KATUGA anasema pingamizi linahusu mahakama hii haina mamlaka kusikiliza shauri hili.
Anachotuletea hapa ni kama anatoka kwenye point ya kisheria.
Naona mwenzetu anachallenge namna information inavyokuwa challenged.
Tunaweza mkamatia mbali sana tukimuacha hivi au tusimkamate kabisa.
Mahakama 🤣🤣🤣
Katuga anasema tunaweza chukua siku saba au sita.
Anamkaribisha Wakili Job wa serikali anasema upande wetu turejee kwenye shauri la Mahakama ya rufaa Civil Application No 656/2021 ilisema
Pingamizi linapaswa kuwa la kisheria huyu mtu (Lissu) mkimuacha ataenda mbali sana.
Angalieni namna ya kumdhibiti, atatuacha nawaambieni waheshimiwa majaji.
Mhe Lissu : Hoja ya pingamizi lao haina msingi wowote kisheria.
Kama niliyosema jana mahakama hii haina mamlaka juu ya shauri hili on the face of records kuna irregularities.
Kwahiyo kusema kwamba hizo zinaonekana kwenye rekodi ya mahakama zisisemwe hiyo hoja haina maana yoyote.
Pia hiyo kesi waliyoitaja wangejua kesi maarufu ni Mukisa Biscuits anataja citation yote kutoka kichwani anasema hiyo kesi inasema PO ni nini?
Sasa wao wanacite kesi gani sijui hapa. Haya mambo yapo kwenye Mukisa.
Jamaa hii kichwa yake sijui ikoje. 🤣🤣
Ningekuwa naingiza mambo mapya lakini nazungumzia kuhusu makaratasi ambayo nimepewa jana hapa mahakamani wanayakataaje sasa?
Dr. Nshalla ameenda kuongea na Lissu kidogo wamemaliza.
Na majaji nao wanateta.
Mahakama iko kimya majaji wanateta kuna POLISI moja hapa simu yake imepiga wimbo wa BONGE LA DADA ameona sana aibu. 🤣🤣🤣
Lissu anasema sasa nimetaja sheria kuhusu namna committal proceedings inavyopaswa kufanya. Hizi rules ni zao wamezitengeneza juzi hapa wao wenyewe sio mimi.
Tusipozungumzia makosa yao ambayo hawataki nizungumzie wanataka tuzungumzie makosa ya nani? Either nazungumzia nini kama hoja yao iko sahihi maana yake yote yafutwe. Ninachosema ni kwamba toka jana nilikuwa nazungumzia nini? Basi kama ni hivyo futeni hadi niliyosema jana.
Jaji anamuuliza KATUGA kama ana rejoinder.
Katuga anasema anachokufanya yeye ni kwamba yuko aggrieved na maamuzi ya mahakama kwahiyo naomba tena Mahakama jamani Mheshimiwa imuelekeze. Tumeona hadi yamejadiliwa hadi maamuzi ya mahakama kuu. Muelekezeni kuendana na kilichopo tu tafadhali.
Naomba Wakili Mrema aongezee, anasimama na kusema tunatofautiana nae kwasababu baadhi ya mashahidi aliowasema kwamba wangekuwa ni mashahidi wake kwenye proceedings hawapo na amesema kanuni ametungiwa yeye lakini hazipo kwneye proceedings.
Huyu mtu asipodhibitiwa anaingiza mambo mengi hapa. Yanatuvuruga sisi. Hayapo kwenye makaratasi. Anachomeka sana vitu. Anasema jambo moja ukizubaa anachomeka mengine tisa. Adhibitiwe.
Part 6 itaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako.