Uongozi wako imara, umefugungua Tanzania kuwa lango kuu na tegemeo kwa nchi zinazotuzunguka, imekuwa kimbilio la mitaji mikubwa, uwekezaji na biashara za kimataifa, Umoja na mshikamano unaouhubiri ndio TUNU ya Taifa letu.
Rais @SuluhuSamia TUNASIMAMA NA WEWE BEGA KWA BEGA. ๐น๐ฟ
Waziri w Mambo ya Ndani y Nchi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Kamishna wa Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kushirikiana na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi kufanya operesheni y kudhibiti na kukomesha vitendo vy utapeli wa mtandaoni pmj na wizi wa simu.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo akipokea Taarifa ya utekelezaji wa matengenezo ya barabara Itoni -Ludewa- Manda km 211.4 sehemu ya Mlima Kimelembe Km151-154 kutoka kwa Meneja Tanroads Mkoa wa Njombe bi Ruth Mosses Shalluah Februari 17, 2025
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Innovo ya nchini Uingereza Bw. Paul Woodman pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya MECCO Bw. Nasser Sheikh, Ikulu Dodoma
MAJALIWA AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KWENYE KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA ISHIRINI YA HESLB
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Februari 17, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu
GERSON MSIGWA: KUELEKEA MIAKA MINNE YA UONGOZI WA SERIKALI INAYOONGOZWA NA DKT SAMIA SULUHU HASSAN SERIKALI ITAELEZA NINI IMEFANYA KWA WANANCHI
Alisema "Tutatumia kipindi hiki kuwaeleza watanzania Serikali ya Awamu ya Sita imefanya nini katika kipindi cha miaka minne"
RC MAKONDA AONGOZA KAMPENI YA USAFI NA UPANDAJI MITI SIKU YAKE YA KUZALIWA
RC Arusha, Mhe. Paul Makonda, ameongoza kampeni maalum ya usafi wa mazingira na upandaji miti huko Meru. Tukio ambalo limefanyika leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ashiriki Mkutano wa Kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 15 Februari, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 14 Februari, 2025 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa kawaida wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)
Excellencies and distinguished guests, delegates, partners and friends, welcome to Tanzania for the Mission 300 Africa Energy Summit to be held in Dar es Salaam on the 27th and 28th of January 2025. This summit marks a historic moment in our collective efforts to accelerate energy access across Africa, and to take bold actions to power our continents's future.
Karibuni sana.
@tonytogolani Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hayati Ali Hassan Mwinyi, Hayati Idris Abdul-Wakil, Hayati Rashid Mfaume Kawawa, Hayati Dkt Omar Ali Juma, Jaji Joseph Sinde Warioba na Dkt Salim Ahmed Salim
Katika mchezo wa bao na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mbunge) mjini Songea, nikianza ziara yangu ya kikazi mkoani Ruvuma leo Jumatatu, Septemba 23, 2024.
Kheri ya kutimiza Miaka 60 kwa Jeshi letu Watanzania, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Katika siku ya leo tunayo kila sababu ya kujivunia kama Watanzania kwa kuendelea kuwa na Jeshi imara, la ulinzi, lenye weledi, utayari na nidhamu ya hali ya juu na linaloheshimika ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Katika siku hii pia tunawakumbuka na kuwaenzi Marais na Maamiri Jeshi Wakuu waliopita, Wakuu wa Majeshi, Makamanda na Wapiganaji wote waliotangulia mbele za haki tunapoadhimisha miaka sitini ya chombo hiki walichokipenda na kukithamini sana.
Nikinukuu maneno ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere akihutubia Jeshi letu Septemba 1 mwaka 1964; โMoyo kwanza kabla ya silaha.โ Kwa moyo wao waliotangulia na moyo wenu Makamanda na Wapiganaji mliopo, taifa letu limeendelea kuwa imara, mipaka yetu imeendelea kuwa salama na wananchi wetu wanaishi kwa amani katika nchi yao iliyo huru.
Utii wenu, nidhamu yenu na utayari wenu kwa nchi yetu ndio msingi wa Watanzania kuendelea kuwaamini na kuwa na matarajio makubwa nanyi. Ilindeni imani hiyo kwa nguvu kubwa, tena kwa nguvu kubwa sana. Endeleeni kufanya kazi zenu mkijua kwamba Amiri Jeshi Mkuu nipo nanyi kwa hali zote.
Ahsanteni kwa utumishi wenu.
Mungu Ibariki Afrika.
Mungu libariki Jeshi letu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Nimewasili jijini Beijing nchini China kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika.
Aprili 26 mwaka huu, Tanzania na China zilitimiza miaka 60 ya mahusiano ya kidiplomasia. Imekuwa miaka 60 ya mahusiano ya kimkakati yenye tija kwa pande zote mbili na urafiki katika nyakati zote.
Kama ilivyokuwa ndoto ya waasisi wetu, jukumu letu ni kuhakikisha tunaendeleza mahusiano haya yaweze kuleta tija zaidi hasa katika maendeleo ya sekta muhimu za uchumi wetu.
Congratulations, @DocFaustine, on your election to serve as the next @WHOAFRO Regional Director โ it is a great privilege, and a very great responsibility. I and the entire @WHO family in Africa and around the world will support you every step of the way.
#RC74AFRO
Ahsanteni sana Morogoro.
Panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu nitarejea tena kuona hatua kubwa tunazoendelea kupiga kwa pamoja hapa na kwenye mikoa yote nchini katika kuinua hali ya maisha kiuchumi, miundombinu, afya, elimu, maji, nishati na matumizi ya ardhi.
Imekuwa siku njema ya kazi katika Wilaya za Gairo na Kilosa mkoani Mogorogoro ambapo pamoja na mambo mengine nimezindua rasmi matumizi ya Hospitali ya Wilaya ya Gairo, Daraja la Berega [kuunganisha Kilosa, Gairo, Kiteto na Kilindi] na kuzungumza na wananchi.
Faraja kubwa kuona namna miradi ya maendeleo wilayani inavyosaidia kubadili maisha ya wananchi wetu.