Tanzania Initiative For Social And Economic Relief
@TISER_NGO
TISER is a local Tanzanian NGO registered to operate all over Tanzania. We are determined to build a resilient society through local initiatives and interventio
Epusha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, mama anapaswa kuhakikisha analala ndani ya chandarua chenye dawa ili kumkinga yeye pamoja na mtoto dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria. Hongera waziri wa Afya @ummymwalimu kwa kusisitiza jambo hili.
#WorldMosquitoDay
Leo ni siku ya mbu duniani. Shirika la TISER linaendelea kuwasisitiza Watanzania wote kuendelea kulala ndani ya chandarua kilichotiwa dawa ili kuepuka magonjwa yanayoenezwa na mbu kama vile Malaria, Zika, Dengue na homa ya Chikungunya. @ummymwalimu@WHO#WorldMosquitoDay
Leo ni siku ya utu duniani (The World Humanitarian Day). Asasi ya TISER inaadhimisha siku hii muhimu kwa kusisitiza matendo ya utu na kuwakumbuka mashujaa ambao walijitolea/wanajitolea maisha yao, muda wao au rasilimali zao kuokoa maisha ya wengine.
#WorldHumanitarianDay
Picha ya pamoja ikijumuisha wajumbe wa kamati ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi Milama, watendaji wa kijiji na watumishi wa Asasi ya TISER.
#PeaceBuildingAndConflictResolution
Watendaji wa Asasi ya @TISER_NGO pamoja na watendaji wa vijiji wakiwa katika kikao cha kamati ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi katika kijiji cha Milama wilayani Mvomero.
Huu ni tekelezaji wa mradi wa kuboresha amani na utatuzi wa migogoro ya ardhi chini ya ufadhili wa @FCSTZ
Wanawake ni kundi lenye mchango mkubwa katika kukuza kilimo na kuhakikisha usalama wa chakula na lishe bora.
Ili kuboresha uzalishaji wao, wadau wanapaswa kuwawezesha wanawake kupata mbolea, mitaji na pembejeo muhimu za uzalishaji katika kilimo.
#MwanamkeNaKilimo
Serikali na wadau wengine wanapaswa kuhakikisha mkulima ananufaika na mazao yake. Ili kumlinda mkulima, madalali na wachuuzi wanyonyaji lazima kudhibitiwe.
Kilimo ni uti wa mgongo kwa uchumi wetu hasa kwa wakazi wa vijijini. Wakulima wanapaswa kulindwa na kuthaminiwa.
Wakulima wana haki ya kunufaika na mnyororo wa thamani wa mazao yao. Ili kufanikisha jambo hilo, Asasi ya @TISER_NGO inawahamasisha wakulima kusindika mazao yao ili kuyaongezea thamani.
#OngezaThamaniYaMazao
Agosti 12, 2018 Asasi ya TISER iliandaa mkutano maalum uliojumuisha viongozi wa kisiasa wa wilaya ya Mvomero, viongozi wa kidini pamoja na viongozi wa jamii za wakulima na wafugaji kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi. Mgeni rasmi akiwa DC wa Mvomero :
https://t.co/3rydpk6lvb
Vijana ni nguzo ya jamii yoyote duniani. Sera na mipango yoyote inapaswa kuzingatia ustawi na maendeleo ya vijana.
Asasi ya TISER inawatakia vijana wote maadhimisho mema ya wiki ya vijana duniani.
Under the partnership and financial support from @FCSTZ, TISER NGO have been actively engaging in conflict resolution between farmers and pastoralists in Mvomero district, Morogoro.
#Azakinakilimo
Kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, shirika la TISER linaendelea kuwahamasisha wakulima kuongeza thamani ya mazao yao ili waweze kunufaika zaidi na mnyororo wa thamani.
Ujenzi wa viwanda vidogo vya kusindikaa mazao ya wakulima ni muhimu katika kuongeza thamani.
#NaneNane2020
#NaneNane celebrates and recognizes the important contribution of farmers in the agricultural sector in #Tanzania Happy Nanenane Day.
Tunawatakia watanzania wote maadhimisho mema ya sikukuu ya Wakulima.
#AzakiTanzania#FursaYaKilimo
Kilimo ni sekta muhimu katika mapambano dhidi ya umaskini. Kilimo cha mazao ya chakula pia ni nguzo muhimu ya katika kuboresha lishe na afya ya jamii.
Asasi ya TISER inawatakia wakulima na watanzania wote kwa ujumla maadhimisho mema ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane.
#Nanenane2020
Kupitia mradi wa Udumishaji wa Amani na Utatuzi wa Migogoro unaofadhiliwa na @FCSTZ . Asasi ya @TISER_NGO imeendelea kuhamasisha wafugaji kutumia ufugaji wa kisasa kwa kutumia mabanda (zero grazing) ili kuepusha migogoro ya ardhi na wakulima.
Baadhi ya jamii za kifugaji wilayani Mvomero zimekuwa zikilalamikiwa kwa kuwatumia watoto katika shughuli za uchungaji wa mifugo. Tabia hii inatajwa kama mojawapo ya vyanzo vya migogoro ya ardhi kutokana na uwezo mdogo wa watoto hao kudhibiti mifugo hiyo. 1/2 UZI ....
Kizazi bora cha kesho kinapaswa kuandaliwa na kizazi cha leo. Shirika la @TISER_NGO kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tunaendelea kuhamasisha umuhimu wa kuwekeza katika elimu za watoto wa mijini na vijiji bila ubaguzi wa jinsia zao. Elimu ni ufunguo wa maisha yao.
Michezo ni mojawapo ya njia za kukuza amani na utulivu katika jamii. Shirika la @TISER_NGO
limeendelea kutumia michezo kama njia ya kuzileta pamoja jamii za wakulima na wafugaji wilayani Mvomero kwa ufadhili wa @FCSTZ. Tazama video hii:
https://t.co/blmR5O4IfB
Asasi ya @TISER_NGO inaendelea kutoa elimu ya namna bora ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID19 kwa wakazi wa kata na vijiji mbalimbali za Wilaya Mvomero. Kwa ufadhili wa @FCSTZ
Mkurugenzi wa Taasisi ya @TISER_NGO Ndugu Otana Nicholas akitoa mafunzo kwa washiriki wa semina ya kuwajengea uwezo wanawake katika kushiriki kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi katika kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero.
Mradi unatekelezwa na @TISER_NGO kwa ufadhili wa @FCSTZ