Tomorrow! Don’t miss the Africa Unplugged: Summit Special Edition as we launch YouLead Summit 2025 – Breaking Barriers, Building Futures 🎉
📅 Thursday, 28th August 2025
🕖 7 PM EAT | 5 PM WAT
🔗 Join us live: [https://t.co/icpwqi497P]
Come celebrate past summit journeys and get inspired for this year’s edition. Rally your peers, friends, and colleagues—see you there.!
#AfricaUnplugged #YouLead25
Tomorrow! Don’t miss the Africa Unplugged: Summit Special Edition as we launch YouLead Summit 2025 – Breaking Barriers, Building Futures 🎉
📅 Thursday, 28th August 2025
🕖 7 PM EAT | 5 PM WAT
🔗 Join us live: [https://t.co/icpwqi497P]
Come celebrate past summit journeys and get inspired for this year’s edition. Rally your peers, friends, and colleagues—see you there.!
#AfricaUnplugged #YouLead25
Leo asubuhi katika kazi, niliposhiriki katika harambee ya ujenzi wa Kituo cha Kulelea Watoto wenye Usonji cha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kitakachojengwa Bagamoyo. Ninalipongeza Kanisa (KKKT) kwa kuamua kujenga kituo hiki kwa ajili ya malezi na makuzi ya watoto wetu. Hii ndiyo maana ya upendo na moja ya majukumu muhimu ya dini katika jamii yetu.
Katika kutambua, kutunga na kutekeleza sera zinazosaidia watoto wenye mahitaji maalum, Serikali imenunua vifaa tiba mbalimbali pamoja na kuwezesha uwepo wa wataalamu (wa lugha, elimu na tiba) kwa ajili yao. Kazi hii njema na sehemu ya jukumu la Serikali kwa wananchi inaendelea kuzaa matunda huku tukishirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo zile za dini.
Nimetumia pia wakati huu pamoja na watoto, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kuendelea kuwasihi viongozi wa dini na kila mwananchi kuhubiri amani, umoja, utulivu na kuliombea Taifa hasa tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Tanzania yashiriki maadhimisho ya Siku ya Denmark, yaahidi kuendeleza ushirikiano
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameongoza Watanzania na Wanadiplomasia waliko nchini katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Katiba ya Denmark iliyofanyika katika makazi ya Balozi wa nchi hiyo, jijini Dar es Salaam tarehe 05 Juni, 2025.
Siku ya Katiba ya Denmark, huadhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka kukumbuka kupitishwa kwa katiba ya kwanza ya kidemokrasia ya Denmark mwaka 1849 na huheshimiwa kama siku ya Kidemokrasia ya Taifa hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Kombo alitoa salamu za pongezi kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, na wananchi wa Tanzania kwa Mheshimiwa Mfalme Frederik X, wa Denmark na raia wake, kwa mchango wake katika kuimarisha ushirikiano wa uwili kati ya Tanzania na Denmark.
“Denmark ilikuwa nchi ya kwanza kuingia makubaliano ya misaada ya maendeleo na Tanzania baada ya kutunga sheria yake ya maendeleo ya kimataifa, hatua iliyoanzisha ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizi mbili, ambao umeendelea kukua katika maeneo ya utawala wa uchumi, afya, na maendeleo ya sekta binafsi,” alifafanua Mhe. Kombo.
Ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Denmark kuongeza uwekezaji wao katika sekta za afya, kilimo, viwanda, utalii, na nishati safi, pamoja na kujenga ofisi zao jijini Dodoma ili kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania .
Awali, Balozi wa Denmark nchini, Mhe.Jesper Kammersgaard, aliipongeza Tanzania kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika nyanja za kiuchumi, miundombinu na maendeleo ya kijamii na kuongeza kuwa mafanikio hayo yameihamasisha Denmark kuendelea kuimarisha uhusiano wake wa kirafiki na kindugu na Tanzania.
BALOZI SHELUKINDO AKUTANA NA BALOZI WA UBELIGIJI
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Ufalme wa Ubeligiji nchini, Mhe. Peter Huyghebaert, katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili maendeleo ya ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji na mwelekeo wa ukuaji wake.
Akizungumza katika mkutano huo, Balozi Shelukindo aliushukuru Ufalme wa Ubeligiji kwa ushirikiano wake wa kindugu na Tanzania ulioendelea kukua katika maeneo mbalimbali, tangu nchi hizi mbili zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1980.
Amesema jitihada zilizofanywa na Serikali ya Ubeligiji kupitia ushirikiano wa pande mbili, zimeleta mafanikio ya kuanzishwa kwa miradi wa maji, usafi wa mazingira, kilimo endelevu na mpango wa 'Wezesha Binti' (2023–2028) mkoani Kigoma, ambao umesaidia kuinua ujuzi na kuimarisha usawa wa kijinsia katika jamii.
Amesema mtazamo wa Tanzania kuhusu migogoro ya kikanda unaongozwa kikamilifu na Sera yake ya Mambo ya Nje, ambayo inasisitiza mazungumzo, diplomasia, na utatuzi wa amani katika kurejesha amani na usalama wa mataifa.
Kwa upande wake, Balozi Ufalme wa Ubeligiji nchini, Mhe. Peter Huyghebaert ameishukuru Tanzania kwa ushirikiano mzuri na nchi yake, huku akiahidi kuendeleza na kukuza ushirikiano huo kwa manufaa ya maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili, kwa misingi ya kulinda amani na usalama wa mataifa yote mawili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Abdullah Bin Zayed Al Nahyan, wakishuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano baina ya Shirikisho la Vyama vya Biashara na Viwanda vya UAE na Barazala la Taifa la Biashara kuhusu uanzishwaji wa Baraza la Pamoja la Biashara kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Tanzaniatarehe 05 Mei, 2025 Ikulu jijini Dar es Salaam.
🌍 Unlock Investment Opportunities in Tanzania & Zanzibar! 🌴💼
From the pristine beaches of Zanzibar to the bustling cities and fertile lands of mainland Tanzania — the future of smart investment is right here. 🏘️⛏️💻
Explore high-potential sectors:
🏨 Hospitality & Tourism
🏠 Real Estate
🌾 Agro-processing
🛠️ Infrastructure
⛏️ Mining
💻 Technology & Innovation
🐄 Livestock & Fisheries
Whether you're a local or international investor, TICO INT is your trusted gateway to East Africa’s booming markets.
📞 +255 757 993 030
Discover Tanzania📍
Your Top Investment Destination!
Tanzania offers a secure and rewarding investment landscape. Consider investing here and unlock a future filled with potential and growth.
#InvestInTanzania#OpportunityAwaits
🌴 Beachside Hotel for Sale in Zanzibar! 🏝️
An incredible investment opportunity awaits! This fully operational beachfront property features a range of luxurious accommodations—from Deluxe Ocean View Rooms to spacious Jungle and Beach Villas with private plunge pools. 🏠✨
Shower
✅ Sitting Areas & Mini-bars
✅ TV, Telephone, Safe Box
✅ Plunge Pools (Villas only)
✅ Tea & Coffee Making Facilities
✅ Free Wi-Fi
📍Located steps from the beach, this property is perfect for investors in the hospitality industry looking to tap into
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Medali ya Mother of the Nation Order kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan. Medali hiyo iliwasilishwa kwake na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mhe. Sheikh Abdullah Bin Zayed Al Nahyan Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2025.
Aidha, Medali hiyo ni moja kati ya Medali za juu kabisa kutoka kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Medali hiyo hutolewa kutambua mchango Kiongozi katika kuleta maendeleo endelevu kwa jamii yake. Serikali ya UAE imetambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. Samia katika kuwaletea Watanzania maendeleo endelevu ambayo yanaendana na Sera za UAE za maendeleo endelevu katika kijamii, uwezeshaji wanawake na ushirikiano wa kimataifa.
Sheikh Abdullah aliwasilisha salamu kutoka kwa Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mtukufu Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan na kuwatakia kheri wananchi wa Tanzania katika maendeleo pamoja na ustawi zaidi. Pia alisisitiza kuimarishwa zaidi uhusiano wa kudumu baina ya nchi hizo mbili na kusisitiza umuhimu wa kupanua ushirikiano katika sekta muhimu.
🌍 TICO INT.
Workers are the backbone of progress!
At TICO INT, we celebrate the hardworking men and women contributing to building Africa's investment future.
Let’s keep creating opportunities together!
📍